Pongezi WanaMtwara! Pongezi Serikali ya CCM!

Pongezi WanaMtwara! Pongezi Serikali ya CCM!

Mtwara hooooooyeeeeeeeeee! Hawa ndo washindi.Mzee wa kulia na liwalo na liwe alikuwa hana jinsi mbele ya kauli mbiu "GESI KWANZA UHAI BAADAE"
 
Katika hali inayoonekana ni ya kushangaza ni vyombo vya habari kuendelea kuiripoti ziara ya pinda ya kuja mtwara eti kwamba amefanikiwa kuumaliza mzozo wa gesi na kutuliza taharuki kwa wananchi kwa ujumla wake,

hivi ni vitu vya ajabu sana,tujiulize pinda katika ujio wake kaongea na wananchi au kaongea na wawakilishi?,na je ana uhakika gani ya kwamba hao wawakilishi wakija kwa wananchi kuleta mrejesho watapata kueleweka na kuaminika?,

Pinda katika mazungumzo yake kajaribu kuelezea ya kwamba taarifa ambayo wananchi walipewa haikuwa sahihi na
kwamba mchakato wa kusafirishwa kwa gesi sharti kiwanda cha kuchakatwa gesi kijengwe mtwara katika kijiji cha madiba, ili mabaki yatokanayo na ujenzi huo yazid kuvutia viwanda mbali mbali kutoka kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, sawa,hii si mara ya kwanza kwa serikali hii kutoa ahadi kama hizo,imetoa ahadi kama hizo kilwa,lakini hadi leo hii hakuna chochote kilichofanyika huku gesi hiyo ikiendelea kusafirishwa,

Ieleweke wazi ya kwamba gesi hii n nyingi na wanamtwara na kusini kwa ujumla msimamo wao ni kuhakikisha gesi hii inanufaisha watanzania wote na si Dar es salaam pekee,

Ruvuma hawana umeme wa kutosha,hawapo katika grid ya taifa,tabora,kigoma n.k huko kote hawana umeme wa uhakika na hawapo katika grid ya taifa,lini sisi mtwara na hao wenzetu tutaingizwa kwenye plan kuu ya grid ya taifa kwa kutumia rasilimali gesi hii,pinda kashindwa kutolea ufafanuzi hilo.

Ni kukosa hekima kwa pinda na wengine kusema ya kwamba amefanikiwa kutuliza vurugu za kusini,kwani kusini tuna vurugu zisizo na mashiko?kabla ya pinda kuja huku watu walikuwa tayari na utulivu huku wakiendelea na shughuli zao za kila siku,pinda kaja na yake tuh,na wananchi hakuna chochote walichoipata kwa ujio wa pinda,

Pinda kasema ya kwamba..

1.kiwanda cha kuchakata gesi kitajengwa kijiji cha madiba na kwamba gesi hiyo haitasafirishwa hadi kujengwa kwa kiwanda hiko,swali kwake ni kwamba plan ya kujenga hiko kiwanda iliwepo au haikuwepo?na kama ilikuwapo kwanin haikusemwa,walikuwa walificha nini?,kiwanda kitajengwa ili kisafirishe gesi hiyo,,sasa cha kujiuliza plan ya gesi ni ndan ya miez 18,sasa je hicho kiwanda kinachosemwa kitajengwa ndan ya hiyo miez 18 pia au imekaaje kaaje?

2.plan ya ujenz wa bomba ipo au haipo?kama ipo watanzania hawapingi plan ya ujenz huo tuh.,la hasha,wanataka kujua mkataba huo ukoje?mbona uko kisiri?bunge halijui chochote kuhusu mkataba huo,je hauna ufisadi?una maslahi ya nchi au kwa watu binafsi?
Sio mara moja ama mara mbili kuona nchi hii ikiingia kwenye mikataba mibovu inayopelekea watu kuish maisha ya udhalili.
Pia,plan ya bomba kama ipo,mbona hajajibu ipi ni bora kati aya kusafirisha umeme na kusafirisha gesi kwa maslahi ya nchi hii?

Ndugu zangu tusiwe ni watu wa kukubali kupokea majibu mepesi mepesi kwa hoja zinazostahili majibu ya uhakika kama yahusuyo gesi yetu,pinda alichokifanya ni kuja kuitetea serikali na boss wake,na SI kuja kusimama kwa masilahi ya wananchi,hilo lieleweke wazi.
Hakuna wa kutengua ile kauli ya jk kwamba gesi lazima itoke kwa namna yoyote ile zaid ya mwenyewe jk,hawa wote kina pinda ni wachumia tumbo tuh,,

tunawatadharisha hao wawakilishi waliokwenda kuongea na pinda kwamba wao hawawez kutusemea sisi,,na kama wanataka kutusemea sisi basi watusemee mambo yenye mantiki na sio blah blah kama hizo na pinda wao,tbc siku zote ilikuwa haitaki kuliport habari hii leo inapokuja kusema ya kwamba pinda kafanikiwa kutuliza mgogoro wa kusini,mgogoro upi?

Wao wameanza lin kuutangaza mgogoro huu?ni unafiki tuh,tena wa hali ya juu..
Sasa hao wawakilishi wa asasi mbali mbli,wanaharakati na viongoz wa dini wawe makini kwa hilo,sisi hatuendeshwi kwa hulka za kishabiki,bali tunaendeshwa kwa hoja za maana na fact za kueleweka,tunawasubiri waje watupe mrejesho,kama wamesaliti tutaanza na wao kwanza.

Kwa ufupi,hatuna imani na pinda kwa ahadi zake,na hakuna alichokiongea tuh,na yeye hajaongea na wananchi,kaongea na hao wawakilishi ambao wanaweza wakasimamia ukweli ama upotofu.

Na kwa kuwa speaker wa bunge mama makinda kaahidi kuteua tume ya bunge ili ije kutusikiliza na kwenda kupeleka hoja hii bungeni,sisi tunatamka rasmi ya kwamba tuna imani na hiyo kamati inayokuja na si huu ujio wa pinda,pinda kazid tuh kupinda pinda na kujipindua pindua,aende zake na hatuna imani nae,,

hili suala haliwezi kuisha kirahis rahisi kama wanavodhania,sisi tunahoja za maana,wao wanazikwepesha na kuleta ahad ambazo siku zote wamekuwa si wenye kuzitekeleza..

Tegemeeni kuskia mengi sana kutoka huku,the game is not over..!

Gesi kwanza uhai baadae...
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Zile hoja zilijibiwaje? zile zilizowasilishwa na maimamu?:majani7:
 
Suala la gesi ya Mtwara limehitimishwa na waziri mkuu kwa kubaliana na wana Mtwara kwakile walichokuwa wanakidai
Baadhi ya vyombo vya habari vimenukuu kuwa waziri mkuu amesuluhisha jambo hili, kimsingi haikuwa suluhu kwa maana ya vyombo hivyo vya habari vinavyotaka kutuaminisha bali ilikuwa ni kutekeleza kile wanamtwara walichokitaka
katika dhahama hii kuna watu wameathirika kwa njia moja au nyingine napenda kuwapongeza wote walioshiriki kwa umoja wao hadi ushindi wa wazi ukapatikana
ILA KUMBUKENI SAFARI BADO NI NDEFU NA SERIKALI YETU C YA KUAMINI MOJA KWA MOJA
 
mafilil acha propaganda kama wenzio wa lumumba, tatizo lenu bado ni akili ndogo kutaka kutawala akili kubwa, na nyie mnd=adhani watanzania wa leo ni sawa na wa 2000? Na ma ccm jaribuni kutafuta suluhisho la matatizo ya wananchi sio kila siku kulilia upinzani tu unaharibu nchi wakati nyie ndo waanzisha matatizo. Kama mgewasikiliza wanamtwara hayo yote yangetokea? Huo ni mwanzo na mwezi ujao ni zamu ya kahama/shinyanga.wananchi wameshawajua na utapeli wenu
 
hongera lakini utaratibu huu wa kila kitu kutatuliwa na viongozi wa ngazi ya juu kabisa sijaupenda,wizara ya nishati na madini mnamfanya nini? hili halikuwa la waziri mkuu naibu waziri wa wizara husika unge weza kufanya hili lakini umeshindwa
 
Endelea kujidanganya, ila ujue ni too late wananchi washawatambua kua maccm sio binadamu wa kawaida,. Mtwara washaagana na boti hili lililo oza la ççm
 
kila siku tuna soma tu kutokana na utatuaji wa masuala muhimu kama haya ni lini tuta fanya mtihani wake na tutafauru bila ya kurudia mtihani
 
Serikali inawajali hadi watu wafe!
Serikali inawajali, na huo mpango unadhani ungesitishwa bila maandamano ya Umma!
 
Historia imeandikwa leo Mtwara kwa kitendo ya pande mbili kufukia mashimo na kufikia muafaka wa kusahau yaliyopita kwa kuanza ukurasa mpya wa kusameheana kuanza harakati za kujenga nchi yetu. Kuna wati hapa jamvini walitegemea muafaka hautafikiwa ili wanufaike kisiasa, hongereni wana Mtwara kwa kuweka mbele utaifa pamoja na kuheshimu viongozi kutoka CCM ambao mliwapa kura za kishindo.
Funzo liwafikie viongozi wa vyama vya upinzani ambao mlitumia suala la Mtwara (gesi) kujiimarisha kisiasa mkoani Mtwara na mikoa ya Kusini kwa ujumla. Poleni upepo umeshabadilika CCM bado ni changuo la mikoa ya Kusini.
Twashukuru hatimaye wana Mtwara wamepata ukweli kuwa serikali yao inawajali, inawapenda na ina nia nzuri kwa manufaa ya Mtwara na Lindi.
Mbulula kweli wewe..! Mimi ni Mwana wa Ntwara, hakuna muafaka wa maana uliofikiwa. Mziki upo pale pale gesi haitoki Ntwara mpaka kieleweke.! Wapelekee uongo huu mbulula wenzako
 
Mleta mada ni ule mtambo wa kupika majungu aliosema Kinana?
haya majitu nadhani baba yao fitina na mama yao majungu, lakini hamna nafasi tena kwa ccm kuaminiwa, kifupi hawafai, angalia ahadi zilizotolewa mtwara kwa siku moja tu utajua shetani ana kadi ya ccm
 
I wish Mirembe could also open up a college. We have a lot of instructors and possible students too !!

Historia imeandikwa leo Mtwara kwa kitendo ya pande mbili kufukia mashimo na kufikia muafaka wa kusahau yaliyopita kwa kuanza ukurasa mpya wa kusameheana kuanza harakati za kujenga nchi yetu. Kuna wati hapa jamvini walitegemea muafaka hautafikiwa ili wanufaike kisiasa, hongereni wana Mtwara kwa kuweka mbele utaifa pamoja na kuheshimu viongozi kutoka CCM ambao mliwapa kura za kishindo.
Funzo liwafikie viongozi wa vyama vya upinzani ambao mlitumia suala la Mtwara (gesi) kujiimarisha kisiasa mkoani Mtwara na mikoa ya Kusini kwa ujumla. Poleni upepo umeshabadilika CCM bado ni changuo la mikoa ya Kusini.
Twashukuru hatimaye wana Mtwara wamepata ukweli kuwa serikali yao inawajali, inawapenda na ina nia nzuri kwa manufaa ya Mtwara na Lindi.
 
Historia imeandikwa leo Mtwara kwa kitendo ya pande mbili kufukia mashimo na kufikia muafaka wa kusahau yaliyopita kwa kuanza ukurasa mpya wa kusameheana kuanza harakati za kujenga nchi yetu. Kuna wati hapa jamvini walitegemea muafaka hautafikiwa ili wanufaike kisiasa, hongereni wana Mtwara kwa kuweka mbele utaifa pamoja na kuheshimu viongozi kutoka CCM ambao mliwapa kura za kishindo.
Funzo liwafikie viongozi wa vyama vya upinzani ambao mlitumia suala la Mtwara (gesi) kujiimarisha kisiasa mkoani Mtwara na mikoa ya Kusini kwa ujumla. Poleni upepo umeshabadilika CCM bado ni changuo la mikoa ya Kusini.
Twashukuru hatimaye wana Mtwara wamepata ukweli kuwa serikali yao inawajali, inawapenda na ina nia nzuri kwa manufaa ya Mtwara na Lindi.
Kama ni ahadi zilikuwepo na ndo zilizosababisha wana-Mtwara wafanye waliyoyafanya. Alichofanya Pinda ni kurudia ahadi za awali, na kuongeza mpya ila safari hii kila mtanzania amejuwa nini kimeahidiwa. Sasa kama hazitatimizwa, ni kwamba atasababisha na mikoa mingine wafanye kama walivyofanya wa kusini. Kumbukeni ahadi za mwanzo wenye kumbukumbu nazo walikuwa wachache sana ndani ya TZ. Lakini baada ya yaliyotokea, zimekuwa wazi kwa kila mtu.. KAMA HUNA UFAHAMU, HUO NI MTEGO MKUBWA AMBAO UTAFYATUKA BAADA YA MUDA MFUPI TU.

Si mnakumbuka ahadi za JK wakati wa kampeni 2010? Meli victoria etc. Zitarudi kwa mtindo huo... kama kulikuwa na mazoea ya kutamka halafu yasifanyiwe kazi, mwisho ndo huo umefika
 
Historia imeandikwa leo Mtwara kwa kitendo ya pande mbili kufukia mashimo na kufikia muafaka wa kusahau yaliyopita kwa kuanza ukurasa mpya wa kusameheana kuanza harakati za kujenga nchi yetu. Kuna wati hapa jamvini walitegemea muafaka hautafikiwa ili wanufaike kisiasa, hongereni wana Mtwara kwa kuweka mbele utaifa pamoja na kuheshimu viongozi kutoka CCM ambao mliwapa kura za kishindo.
Funzo liwafikie viongozi wa vyama vya upinzani ambao mlitumia suala la Mtwara (gesi) kujiimarisha kisiasa mkoani Mtwara na mikoa ya Kusini kwa ujumla. Poleni upepo umeshabadilika CCM bado ni changuo la mikoa ya Kusini.
Twashukuru hatimaye wana Mtwara wamepata ukweli kuwa serikali yao inawajali, inawapenda na ina nia nzuri kwa manufaa ya Mtwara na Lindi.

we acha kukejeli watu wamtwara! Muue halafu mseme serikali inawajali! Kivipi kama sio unafki! '? Naona mnacheza na wanamtwara!
 
Historia imeandikwa leo Mtwara kwa kitendo ya pande mbili kufukia mashimo na kufikia muafaka wa kusahau yaliyopita kwa kuanza ukurasa mpya wa kusameheana kuanza harakati za kujenga nchi yetu. Kuna wati hapa jamvini walitegemea muafaka hautafikiwa ili wanufaike kisiasa, hongereni wana Mtwara kwa kuweka mbele utaifa pamoja na kuheshimu viongozi kutoka CCM ambao mliwapa kura za kishindo.
Funzo liwafikie viongozi wa vyama vya upinzani ambao mlitumia suala la Mtwara (gesi) kujiimarisha kisiasa mkoani Mtwara na mikoa ya Kusini kwa ujumla. Poleni upepo umeshabadilika CCM bado ni changuo la mikoa ya Kusini.
Twashukuru hatimaye wana Mtwara wamepata ukweli kuwa serikali yao inawajali, inawapenda na ina nia nzuri kwa manufaa ya Mtwara na Lindi.

Kwa kile kinachoonekana kushindikana kwa suluhu juu ya mgogoro wa gesi, hali inaonekana kuwa bado ni tete mbali na jitihada za Waziri Mkuu kuja kutatua mgogoro huo. Baada ya taarifa yake ya majumuisho aliyoitoa jana jioni hapa Mtwara inaonekana bado kuacha maswali mengi miongoni mwa Wananchi. Hali asubuhi ya leo imekuwa ni tofauti kidogo kulinganisha na jana. Leo kila unapopita majadiliano na mazungumzo yao ni juu ya hotuba ya jana ya majumuisho juu ya hoja za mgogoro wa gesi. Inaonekana watu bado wanamashaka na msimamo wa serikali.

Nimebahatika kuongea na wananchi wachache juu ya jambo hili lakini wote wameonekana kutosadiki msimamo wa Serikali kwa kile wanachodai ni propaganda za kisiasa na uhalisia wa mambo. Wakisisitiza katika hili walihoji; "Hivi wewe ndugu yangu, kama msimamo wa serikali ilikuwa ni kusafirisha gesi iliyosafishwa, je kipi kilkistahili kuanza kujengwa kati ya kiwanda cha kusafisha na bomba la kusafirishia gesi?"

Mwingine akahoji; "Unawezaje kukubali kusafirisha umeme kupelekwa Songea ambako ni mbali na kushindwa kupelekwa Dar es salaam ambako ni karibu? Wapi kutakuwa na gharama kubwa zaidi? Tunajuwa janja yao ilipo kwa hiyo, msimamo wetu uko palepale kwamba kama shida yao ni umeme basi usafirishaji wa gesi kwa bomba haiwezekani. Ni kipi kinachowafanya kung'ang'ania usafirishaji huo kama si wizi?"

Kwa hakika inaonekana bado kuna jambo serikali inapaswa ilifanye zaidi ya hiki kinachoaminika ni suluhu inayotangazwa tangu jana, kwani nadhani bado suluhu hiyo haijaingia masikioni mwa watu. Mikanganyiko ni mingi, wengi wanahoji pia juu ya sababu hasa ya Waziri Mkuu na jopu lake kubwa kuja huku; je ilikuwa ni kusikiliza hoja na misimamo ya Wanakusini au kutoa msimamo wa Serikali kwamba lazima gesi isafirishwe kwa bomba? Bado hoja ni nyingi kwakweli.

Wananchi wamekwenda mbali zaidi na kuponda hoja kuhusu kuchelewa kumalizika kwa ujenzi wa barabara, maeneo ya Somanga. Kwani kwa mujibu wa Waziri Mkuu ni kwamba; barabara imechelewa kukamilika ujenzi wake kwa sababu ya kufariki kwa Mkandarasi. Hoja hii inapingwa kwa kuhoji kipindi tangu barabara hiyo ilipoanza kujengwa na kifo cha Mkandarasi huyo, kwamba hakuna uhusiano wowote. Wanatole mfano hapa kwamba itawezekanaje msiba ushindwe kumaliza ujenzi wa barabara kipande cha Kilometa 60 ndani ya zaidi ya miaka kumi?

Ni wazi kabisa kwamba, mbali ya taarifa zinazotolewa juu ya kumalizika kwa mgogoro huu lakini ukweli ni kwamba hali bado ni tete na kunahitajika busara zaidi kutafakari jambo hili zaidi ya kusimamia misimamo ambayo itatuletea matatizo. Inatupasa tutafute suluhu ya kudumu ili hata kile kinachotegemewa kufanywa kiweze kuleta tija kwa nchi yetu na si machafuko.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Wabariki Watanzani.

Hassani Samli,
Mtwara.
+255717340671
samlihassani@yahoo.com
 
Baada ya kuua, kuchoma boma na mali za makada wenu ndo mnatambua kuwa Mtwara kuna watu wanaopaswa kusikilizwa! Wapinzani na wanamtwara ndio wameshinda maana Pinda kasema yaliyokuwa yakihubiriwa na wapinzani. KWELI HAKI HAIOMBWI BALI INADAIWA (Lema) Kwa hiyo bomba ndio basi?
Sio kweli mkuu, bado kuna ubabaishaji wa hali ya juu hapa. Tatizo Pinda anadhani wanaMtwara wana upeo hafifu. Kwa kifupi Pinda aliongea na wawakilishi wa wanaMtwara ambao wengi wao hawajaridhishwa na ahadi za kibabaishaji zilizotolewa na Pinda. Moja ya point ambayo wengi wanaona ina dalili za ubabaishaji ni pale Pinda aliposema kwamba eti mtambo wa kuchakata gesi utajengwa eneo linaloitwa Madimba (eneo lililopo karibu na Msimbati, inakotoka gesi ghafi) halafu bomba litajengwa toka hapo Madimba, ambapo asilimia kumi na sita (16%) ya gesi iliyochakatwa itasafirishwa kupitia bomba hilo ambalo litaunganishwa na bomba linalotoa gesi Songosongo kwenda Dar.. Kauli hii imeamsha maswali mengi sana kwetu sisi wanaMtwara. Hapa tunaona kuna udanganyifu mkubwa sana unaotaka kufanyika katika hili. Istoshe tunajiuliza 'hivi kwa nini ikiwa chanzo cha mgogoro ni ujenzi wa hilo bomba, Pinda na timu yake waone kwamba pamoja mambo mengine, lakini issue ya ujenzi ni kitu kinachotakiwa kupigiwa chapuo namna hii?' Tunadhani hapo pia kuna kitu abnormal kinachoendelea katika mradi huu. Lakini kwa vile wamesema kuna tume ya bunge inakuja sisi hatuna papara na hili, majibu yetu yatapatikana baada ya kukutana na hiyo tume na kusikia mrejesho wa hiyo tume huko bungeni.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Pinda kasema ya kwamba..

1.kiwanda cha kuchakata gesi kitajengwa kijiji cha madiba na kwamba gesi hiyo haitasafirishwa hadi kujengwa kwa kiwanda hiko,swali kwake ni kwamba plan ya kujenga hiko kiwanda iliwepo au haikuwepo?na kama ilikuwapo kwanin haikusemwa,walikuwa walificha nini?,kiwanda kitajengwa ili kisafirishe gesi hiyo,,sasa cha kujiuliza plan ya gesi ni ndan ya miez 18,sasa je hicho kiwanda kinachosemwa kitajengwa ndan ya hiyo miez 18 pia au imekaaje kaaje?

Pia mimi nado sijaelewa kinachoanza ni kipi: Kujenga kwanza kiwanda cha kusafisha gesi au bomba la kusafirishia hiyo gezi itakayosafishwa na hicho kiwanda?

Hili suala la kujenga kiwanda cha kusafisha gesi ndiyo kwanza nalisikia sasa.

Wasipokuwa makini kuna dalili ya watu wa Kusini kuingizwa choo cha stendi.
 
Back
Top Bottom