"Pongezi Rais Magufuli Kuwa Mkweli Daima. Tuanzishe Church of Africa, Tuoe Wake Wengi, Tuzae Watoto Wengi?"

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,506
113,626
Wanabodi,
Rais Magufuli ametetea dhana ya wake wengi kwenye msiba wa Masaburi, kama ilivyoripotiwa hapa,

Naanza na swali,
"Baada ya rais Magufuli, kutetea hoja ya wake wengi, jee kuna ubaya Watanzania tukijua, yeye mhe. Rais wetu, ana wake wangapi official na unofficial zaidi ya the official one ambaye ndie the 1st lady?.

Nyerere alikuwa na mke mmoja Mama Maria na watoto 8, wote wa mke mmoja. Mwinyi alipoingia urais alikuwa na wake 2, Mke mkubwa Bi Khadija, na mke mdogo Bi Sitti, na Kitwana Kondo akampa binti, ila kwa vile tumerithi serikali ya kikoloni inayotambua mke mmoja tuu, the official 1st lady alichaguliwa ni Mama Sitti, hivyo hao wake wengine wanakuwa counted kama vimada which is not fair!, idadi ya watoto haitajwi. Mkapa ana mke mmoja Mama Anna na ana watoto wawili, both boy, Steve na Marinyo (Nico). JK alioa akaacha kisha akaoa tena Mama Salma, ana watoto 8, wa Salma ni 3. Jee JPM ana wake wangapi besides 1st Lady Janet?, na je ana watoto wangapi jumla zaidi ya Jesco, bila kujali mama zao ni kina nani?", maana tusije kuwa tunayasema tuu ya wenzetu, lakini ya kwetu, hatuyasemi hadi siku ya siku?!. Mimi kwa upande wangu nina wake wawili officially na mpango kando mmoja!. Mke wa Kanisani amehamia US ni citizen kule na anaishi kule, mwingine ni wa kwa DC, anaishi Bongo na nina watoto 8, ambapo jumla ya wamama 3 wamepokezana, kwa uwiano wa 2+3+3!.

Kufuatia wanaume wengi wa Kiafrika kuwa na ama na wanawake zaidi ya mmoja ama kuwa na ndoa moja lakini wana watoto wa nje, jambo ambalo ndilo mila za Kiafrika, na ndio asili yetu, kufuatia ukweli huu wa rais Magufuli alioutoa kwenye msiba wa Masaburi, jee mnaonaje tukiangalia posibility ya kuanzishwa kanisa la Afrika, The Church of Africa, litakalotambua ndoa za wake wengi maana ndio asili yetu Afrika, na tuzae watoto wengi kama machifu wa zamani, au wafalme kama kina Sulemani na Mswati?.

Preamble
Kama kawaida yangu, kwenye mazuri huwa napongeza na kwenye mabaya huwa nakosoa, miongoni mwa sifa kuu za pekee za Rais wetu kipenzi, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, ni kuwa mkweli daima na kuusema ukweli jinsi ile ile ulivyo, na huusema popote bila kujali ni wapi, ni mkutanoni, ni kanisani, ni msikitini na hata msibani, na pia huwa hajali madhara ya ukweli huo utamfurahisha nani, utamuudhi nani, au utamuumiza nani, au una madhara gani, au kama ataeleweka au hataeleweka, as long as ni ukweli, yeye atausema tuu ukweli huo ali mradi huo ndio ukweli wake halisi.

Magufuli ni Bold Kama Nyerere.
Huko nyuma niliwahi kusema mahali kuwa, rais Magufuli ni bold kama Nyerere, kwenye kuusema ukweli, wao watasema kweli bila kujali the consequences.
Watu wa aina hii, wanaitwa "Very Bold", they just call a spade a spade!. Kiongozi mwingine wa taifa hili aliyekuwa mkweli wa kihivi ni Nyerere. Kanuni yake ilikuwa "Nitasema kweli daima, fitna kwangu ni mwiko" na ikafanywa ni moja ya ahadi za mwana TANU, hivyo kwenye eneo la kusema kweli daima, rais Magufuli ni kama Nyerere, ni mkweli daima na anastahili pongezi!.
Magufuli Kama Nyerere:Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, Ni ...
Kweli Kubwa.
Miongoni mwa kweli kubwa kuliko na kali ya mwaka, ni kweli iliyotolewa jana na Rais Magufuli, kwenye msiba wa Masaburi, alipotoboa ukweli wa tabia za asili ya sisi Waafrika kuwa na wanawake wengi, japo kitendo cha Rais Magufuli kumkosoa msemaji wa familia ya Masaburi alipo sema kuwa marehemu Masaburi ameacha mke mmoja, lakini rais Magufuli akasema, marehemu Masaburi ameacha wake wanne au watano na watoto zaidi ya 20!. Huu ni ukweli uliopitiliza kwa sababu, hata kama mtu ana wake 10, msemaji wa familia, akisema marehemu ameacha mke mmoja, then, officially mke ni mmoja!. Hivyo kitendo alichokifanya rais Magufuli katika msiba huo, sii kizuri, kwa sisi tunaolewa masharti ya viongozi wetu wa dini kwenye mazishi, ili uzikwe Kikristu, lazima itangazwe kuwa marehemu ameacha mke mmoja, hata kama in reality ameacha wake zaidi ya mmoja!, baada tangazo hilo la rais, kama padri aliyeendesha mazishi hayo, angekuwa bold, angeweza kukataa kuzika Kikristu!. Japo sijui kwenye mazishi ya Sokoine sijui ilielezwa nini, lakini marehemu Edward Moringe Sokoine, aliacha wake wawili, mmoja wa kanisani na mwingine wa kimila na wote wanatambuliwa na wanaishi boma moja!. Nyerere pia aliwahi kuzungumzia mambo ya wake wawili wa Sir George Kahama, na kusema "mwenzangu George Kahama, alikwisha endelea endelea, alikuwa na akina mama wawili", hivyo kuwa na mwanamke zaidi ya mmoja ni maendeleo!.

Akitetea wanawake wengi, kwenye msiba huo, Rais Magufuli amesema kuwa ameteta na Kikwete na wao, yeye Magufuli na Kikwete walitamani kuwa na wanawake wengi kama Masaburi!, (hii maana yake waliteta) na kutolea mfano Mfalme Suleiman, aliyekuwa na wake 800, na masuriya 200!. Asante rais Magufuli, kulizungumzia hili, hivi ndivyo haswa sisi Waafrika tulivyo!.

Naomba kukatia hapa kwa faida ya wasomaji wanaopenda kusoma makala fupi.
My Story
Mikoa ya Kagera, Mwanza na Mara, Shinyanga, Shimiyu, na Geita, ni mikoa ya Kanda ya Ziwa, na kwa wanaume wa kanda hii, ambao ni wakamilifu, it is an open secret kuwa na mwanamke zaidi ya mmoja. Mimi nimetokea kanda hii, Baba ndiye Msukuma, na mama ni kutoka sehemu nyingine, wakati nafunga ndoa, miongoni mwa mambo mama alionisisitizia, ni kuniomba na kuniombea kwa Mungu, nisiwe na tabia kama za baba zangu!, na mama akafunguka kuwa baba yako na baba zako wote hakuna mwenye mke mmoja!. Na kusema baba alikuwa na wanawake wengi!. Wazazi wangu wote wawili walikuwa watumishi wa serikali wakifanya kazi bomani. Hivyo walikuwa wakihamishwa mikoa mbalimbali, mama akaniambia baba yako karibu kila mkoa walikomhamishia, ameacha watoto. Wasukuma wanapenda sana watoto, na Kisukuma hakuna mtoto wa nje, wala mtoto ndani, kwetu mtoto ni mtoto!, na hata ukipita tuu mahali kwenye zile one night stand, ukija kuambiwa goli liliingia, hatukataagi watoto wala hatupimagi DNA DNA kuthibitisha, hivyo hata tukisingiziwa sisi poa tuu!.

Mimi mwanzoni, sikumwelewa mama kwa sababu hao watoto wanaosemwa kila mkoa, sikuwahi kuwaona, ila hilo la baba kuwa na wanawake wengi, nililijua nilipoanza kupata akili maana mimi nilikuwa ni besti wa baba, nikienda nae viwanja vyake vyote, na utambulisho ulikuwa huyu ni anti wako, usimwambie mama yako!.

Msiba wa Baba,
Siku ulipotokea msiba wa Baba, ndio nilielewa mama alisema nini, maana sijui hata walikotokea, ila kiukweli, watu walimiminika!, wamama na watoto wao! na kiukweli palitaka kuchimbika, ila thanks God, tulimaliza salama haswa kwa kuzingatia kumbe Mzee aliandika kila kitu, na mpaka leo na mpaka kesho, mimi kama kaka mkubwa wa familia, bado nina wahudumia baadhi wadago zangu wasio na idadi kutoka kwa wamama wengine!' na hapa natoa wito kwa sisi wababa, andikeni wasia!, na kama umefyatua huku na kule, wapeni Mama zao mitaji waweze kujitegemea kulea viumbe vyenu na sio unafyatua tuu, siku ukiondoka duniani, unawaachia wengine misala ya kubeba mizigo yako!.

Nadhiri ya Mke Mmoja
Kufuatia hali hiyo, zaidi ya ombi la mama na sala ya mama kuhusu wanawake wengi, na mimi mwenyewe nikajiwekea nadhiri ya kuwa na mke mmoja tuu na watoto wawili, au watatu na mwisho wanne!. Nikaamua kuishi kizungu!, baada tuu ya ndoa nchini Tanzania, mimi na wife tukahamia UK, kisha US, kule US wife ndiye anakazi mimi nikawa baba wa nyumbani!. Kuna baadhi ya makabila baba kuwa baba wa nyumbani wamaweza, na kuna baadhi ya makabila hawawezi!, ndio maana kuna watu wanaweza kuwa Marioo au vi benten, na kuna watu hatuwezi!. Kiukweli kabisa mimi nilishindwa!, hivyo japo haikuwa rahisi-lakini nikarudi home bongo, na kuendesha maisha ya long distance relationship!.

Long Distance Relationship.
Pia kuna makabila ya wanaume wanaoweza kuendesha maisha ya long distance relationships, na kuna makabila hatuwezi!, moja ya makabila haya ambayo hatuwezi kuendesha maisha ya long distance relationships kwa upande wa wanaume, ni watu wa Kanda ya Ziwa, mambo ya long distance relationship kwa wanaume wa Kisukuma, hatuwezi!. Japo maneno ya mama nayakumbuka, na ahadi ya kutokuwa kama baba, naikumbuka, lakini kuishi bila huduma fulani nilishindwa!, sijui hawa mapadiri wetu wa Katoliki wanawezaje?!, mimi nilishindwa!, na katika kupata huduma hizo, kuna matunda haya na yale, yalipatikana!.

Japo Watoto, Hupangwa, lakini Wengine Hutokea Tuu Bila Kupangwa!.
Kwa kawaida watoto ambao hupangwa, mara nyingi ni wale wa kwenye ndoa, ila katika haya na yale mengine mengine ya mwenye nyumba kusaidiwa kutokana na kukaa mbali, lengo huwa nizile huduma, hakuna kupanga kutengeneza watoto, bali ni au kukosekana umakini, au kutegeshewa, na mtoto akitokea tuu, huyo mama hugeuka mke!. Tayari tulikuwa na watoto wawili, huku nikaongeza mmoja na kule akaongezeka mmoja, mara wanne!, huku na kule, huku na kule mara akaongezeka tena mmoja, mara mwingine!. Wife akaconfirm kufanikiwa kupata green card, hivyo sasa ameamua kubaki US, na mimi sijaamua kuubadili Utanzania wangu, na Usukuma wangu, hivyo kuamua kuishi Tanzania US ni visitation only.

Mkistu Mkatoliki, Mume Tanzania, Mke Marekani, Huu Ndio Mpango wa Mungu?.
Nikiwa Mkristu Mkatoliki, suala langu la mume kuishi Tanzania na mke kuishi Marekani, likatinga rasmi kwenye Jumuiya ndogo ndogo, na likafika hadi kwa paroko, nikawekwa mtu kati katika kikao cha maisha ya Kikristo kuwa ama mkeo lazima arudi, au kama harudi, then wewe lazima uishi maisha yanayompendeza Mungu, kwa kuutoa sadaka mwili wako, kuheshimu kiapo chako cha ndoa, kwa kutopata huduma popote hadi mkeo arudi, au wewe uende!.

Nikawaeleza ndivyo tulivyokubaliana, then nikatakiwa kuamua moja, kama mtu ameishakuzalia watoto watatu, mwenye nyumba kagomea US, kwa nini usimkaribishe rasmi nyumbani?!. Paroko akatoa kibali na kutakiwa kufuata taratibu fulani fulani za kikanisa, mtu akakaribishwa rasmi nyumbani!. Kwa sasa idadi ni vijana 8, wamama watatu, wamesaidiana, wawili wameolewa kwa ndoa moja ya kanisani, moja kwa DC. Japo sijafikisha idadi kama ya Masaburi, lakini kiukweli, ukweli aliouzungumza rais Magufuli Magufuli kumzungumzia Masaburi, unatuhusu wengi, na rais Magufuli ametuzungumzia wengi!.

Kuna Wengi Mke Mmoja, Mume Mmoja ila ... na Watoto...
Kuna wengi wanaishi kama mimi, na waliyokuwa wanaelewa nazungumzia nini, mpaka leo siruhusiwi kushiriki meza ya Bwana kwa vile mke rasmi wa kanisani yuko mbali!. Tufike mahali tuachane na haya makanisa ya tabia za kizungu, tuanzishe makanisa yetu ya Kiafrika yanayotambua Uafrika wetu na kutukubali hivi hivi tulivyo!.
Serikali Iutambue Uafrika Wetu wa Wake Wengi.
Kufuatia ukweli huu kutamkwa na rais wetu, jee mnaonaje sasa ikiwa ni wakati muafaka wa kupitiwa upya kwa kanuni za utumishi wa umma za kizungu tulizorithi kwa wakoloni wazungu, kwa kuondoa ule uzungu wa mtumishi kuwa mke mmoja officially na watoto wanne tuu wanaotambulika rasmi, mtu akiwa na mke zaidi ya mmoja, atambuliwe rasmi na aruhusiwe kuwa na wake zake wote, na hata mialiko isiwekewe limit ya Mr & Mrs tuu, hata title ya first lady, ibadilishwe, waitwe first ladies, na hata ikibidi kuandamana nao wote kwenye ziara za kimataifa, tuandamane nao, ili kuwatendea haki sawa wake wote, sio mmoja kutambulika rasmi, na wengine kuonekana kama vimada!.

Tuanzishe The Church of Africa, Tufunge Ndoa Za Wake Wengi Kanisani?.
Na kama tulivyotaka kuanzisha United States of Africa, huu ni wakati muafaka wa sisi Tanzania kuangalia posibility ya kuachana na hizi dini za wazungu za mke mmoja, mume mmoja kama Roman Catholic, na Anglican Church, tuwe the pioneers tuanzishe The African Catholic, au African Church, turuhusiwe kuoa wake wengi kanisani, after all, sheria ya Mungu ni sheria ya Musa, na hakuna mahali popote kwenye vitabu vitakatifu vimepiga marufuku ndoa za wake wengi!, hoja hizi zimeletwa na katika mafundisho tuu ya wale mitume 12 wa Yesu, na wale mitume sio manabii, wanachozungumza sio lazima kiwe kimetoka kwa Mungu!.

Hongera Magufuli, Kufukia ya Masaburi, Funguka na Yako.
Hongera sana, Rais Magufuli kutamani kuwa na wanawake kama Masaburi, najua Watanzania wengi pia wanatamani kuwa na wanawake wengi, na watoto wengi kama tulivyohimizwa kufyatua, na katika kuonyesha kuwa yeye sio tuu ni mkweli, bali pia awe open, Kikwete yuko open, anajulikana ana watoto 8, kama mimi tuu, sasa kwa kuitumia ile sheria mpya ya the right to information, japo Magufuli ametamani kuwa na wanawake wengi kama Masaburi, jee kwa sasa rais Magufuli ana wanawake wangapi na watoto wangapi?!.

The Right To Privacy Vs The Public Interest, Will The Right to Information Help?.
Japo hili ni swali la maisha binafsi ya rais wetu, yaani rais wetu pia anayo his right to privacy, lakini kwa kiongozi yoyote anayelipwa by the tax payers money, hana hiyo right to privacy, ni the tax payers have the right to know, his public life as well as his private conduct, kwa sababu mambo yoyote rais anayoyafanya, anayafanya kwa kutumia fedha zetu, tunamlipa mshahara ambao haukatiwi kodi, tunamlisha, tunamvisha na kumhudumia yeye na familia yake nje ya mshahara wake, kwa sasa yeye ndio kiongozi wetu, hivyo Watanzania, we have the right to know his public life as well as his private life, wake wangapi, watoto wangapi, ili tumtathmini na ikibidi tumtolee mfano wa kuiga mfano wa maisha yake.

RIP Masaburi na Asante Kutusaidia Wenye Wake Wengi, Kwa Wake Hao Kutambuliwa rasmi, ambapo the significance ya utambuzi huu, sio tuu imewapa heshima kutambulika rasmi hapo msibani tuu, sasa imewapa justification kuwa part and parcel ya inclusion kwenye mirathi ya marehemu mume wao.

Wasalaam.

Paskali
 
Sawa.

Kwa sababu wanawake waliumbwa kwa ajili yetu, tuwaoe wengi ili tufurahi.

Hebu fikiria jinsi Mfalme Suleiman alivyowakusanya watu wazima 700 wenye akili zao na akawa anaishi nao na anawafanya anavyotaka. Amazing!!

Ila alibarikiwa hekima nyingi na mwishowe akaona ni ubatili mtupu.

Hakuna kilichobadilika kulinganisha na enzi hizo, kwa maana hata leo hii ukiwa na 'hela' bado unaweza kuwakusanya wanawake na kuwafanya chochote unachotaka.

Sasa Karne kibao zimepita toka enzi hizo, wasio na hekima bado wanashindwa kuuona huo ubatili aliouona Mfalme Suleiman!.
 
alichofanya Magufuli kwenye msiba wa Masaburi ni kuteleza kama anavyoteleza kwenye speech mbali-mbali.
ni kama alivyosema magari yanayoingia kwenye njia ya mwendo kasi yakamatwe na tairi zifunguliwe ziwe chanzo cha mapato ya polisi au traffic police wapewe 5000/= ya kubrash viatu kila wakimkamata dereva mzembe.

okey kanisa letu tulipe jina gani?
 
Pale Butiama nasikia marehemu Wanzagi (kaka mkubwa wa Mwalimu Nyerere)alianzisha au alikuwa muumini wa kanisa linaloruhusu polygamy.Wanaolijua wajaribu kutujuza ili wenye kupendelea Kuwa wafuasi wa kanisa Hilo wajongee
 
Pale Butiama nasikia marehemu Wanzagi (kaka mkubwa wa Mwalimu Nyerere)alianzisha au alikuwa muumini wa kanisa linaloruhusu polygamy.Wanaolijua wajaribu kutujuza ili wenye kupendelea Kuwa wafuasi wa kanisa Hilo wajongee
The last church na Mdogo wao Kiboko ndo alikuwa anaemsaidia. Watu wengi sehemu za Kisorya walijiunga toka Sabato kwenye early 80s. Hawa ni kama Mormons wa US. Pale makutano ya morroco kuna kanisa nadhnai ndo hilo?
 
Hapa hata sikubaliani nawe kabisa.

Mnaotaka kuyafanya muendelee huko huko, kimya kimya tena.

Mke wa kwanza na wa kanisani atabaki kuwa mke wa mwanaume huyo. Wengine wote hawana usemi kumzidi, labda wawe walipeana talaka.
 
Mh. Rais ni mwana-Afrika halisi, ukweli tuuseme tu hakuna Mwafrika mwenye mke mmoja labda tu asiye na mali au nafasi.
Tuliingizwa chaka na wazungu, Mwafrika asili yake ni kuoa wanawake wengi iwezekanavyo.
Kauli ya Mh. Rais inathibitisha kuwa hata manabii wa zamani kama Mfalme Suleimani na wengineo walikuwa ni watu weusi.
 
Pasco sometimes unachanganya madesa, unaposema 'tuanzishe Kanisa la Afrika' linaloruhusu kuoa wake wengi, una hakika kuwa hakuna Makanisa yanayoruhusu wake wengi?

Uunataka kusema nani aanzishe hilo Kanisa? Kwa taarifa yako hata wewe waweza kuanzisha na utapata wafuasi wengi tu, hasa huko Kanda ya Ziwa na kwa wafugaji; andika Katiba na nenda kasajili Kanisa lako pale Wizarani kwa Mwigulu Nchemba, ni rahisi tu.


Vv
 
Back
Top Bottom