Pongezi kwa Shirika La Reli Tanzania (TRC)

Pongezi kwa Shirika La Reli Tanzania (TRC)

Kidenga

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2018
Posts
278
Reaction score
767
Nimewiwa kutoa pongezi za dhati kwa shirika la reli Tanzania (TRC) kwa huduma nzuri.

Kwa wale mliopata bahati kusafiri na tren ya mwendokasi na dhani mmejionea hudumazao. Yani kuanzia kujali muda, mazingira na hata kutoa taarifa. Ukweli mmekidhi viwango vya kimataifa.

Kwa mara zote nilizosafiri na treni ya SGR sikuwahi kuona mnapoteza hata dakika moja kwenye kuanza safari. Pia kwenye kufika tofauti inaweza kuwa dk 1-5. Hii ni nidhamu ya hali yabkipekee. Natamani kuona ubora huu huu hata baada ya miaka 5 ijayo.

Nashauri Shirika lihakikishe linaendele kusimamia sheria na taratibu lililo jiwekea bila kupepesa macho. Hii ni kwa taratibu kwa upande wa abiria pamoja na wafanyakazi wake.

Inakuwa ni fahari kwa sisi Watanzania kuweza kuwa na huduma nzuri na zinazokidhi vigezo kama za SGR. Hongera sana kwa serikali katika kusimamia uwekezaji huu mkubwa.

Kwa TRC wananchi wamewapokea , please msiwaangushe. Endeleeni kuongeza maarifa na ujuzi.


OMBI KWA SERIKALI

Ikiwezekana Mradi wa SGR uweze kufikia pande zote za Tanzania. Yani Kaskazini , Mashariki, Magharibi na kusini. Tukiweka nia inawezekana. Tunaweza anza kidogo kidogo.

Najaribu kuwaza siku ambayo mtu ataweza kutoka DSM na kufika Arusha chini ya Masaa Manne. Nawaza jinsi uchumi utakavyokuwa kwa kasi.
 
Mkuu...
Unataarifa kuhusu deni la taifa kupaa hadi 116 trillions...🤔
 
Kila mtu ana deni hata wewe unadaiwa. Kama haudaiwi jua umekufa. Sasa kama wewe mimi tunadaiwa sembuse nchi?
 
Back
Top Bottom