Pongezi kwa Jeshi la Polisi kwa Kurudisha Kizuizi- Lushoto

Determinantor

Platinum Member
Mar 17, 2008
57,739
92,165
Wakuu,
Nimefurahishwa sana na kitendo cha Jeshi la Polisi kusikia kilio changu na kurudisha kizuizi cha Polisi Pale Barabara ya Mombo- Lushoto. Hili ni eneo hatari sana na kumeshakua na matukio mengi sana ya uporoji tena wa kutumia silaha. Eneo lile ni jembamba sana na hakuna hata network. Niliweka bandiko Kizuizi cha Polisi Lushoto kirejeshwe upesi na kueleza kuwa sababu zile haziklua thabiti ukilinganisha na msaada mkubwa, hatimae kimerudishwa. Asanteni sana Jeshi la Polisi.

IMG_20170101_153806.jpg

OMBI: Kamateni na Magari yaliyofunga taa ambazo sio maalum, zile taa nyeupe ni hatari sana sana barabarani, wakati narejea Dar jana toka Lushoto usiku nilipatwa tena na tatizo hilo mara mbili mtu anakuwashia hizo taa na kukufanya upoteze kabisa mawasiliano. Wakamatwe na zifunguliwe na kutupwa.
 
Back
Top Bottom