Pongezi Dr. Kitila Mkumbo

Pongezi Dr. Kitila Mkumbo

Status
Not open for further replies.

Centrehalf

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2013
Posts
509
Reaction score
145
Wana Jf nimefurahishwa sana na tabia ya dr. Kitila Mkumbo,nimemfuatilia sana tangu zilipoibuliwa tuhuma dhidi yake pamoja na Zitto na Samson Mwigamba,amekuwa katika hali ya utulivu mkubwa kuliko watuhumiwa wenzie.

Maana baada ya kamati kuu kuwavua nyadhifa zao na kuwapa siku 14 dr amejitokeza mara mbili tu kwenye media kuzungumzia suala hilo.

Kutokana na sababu hiyo nimeanza kuamini kwamba maneno aliyosema kwenye kamati kuu kwamba aliingizwa tu kwenye mkenge na Zitto pamoja na Mwigamba ni ya kweli.

Nasema hivyo kwa sababu ukiangalia baada ya wote wa 3 kurudisha fomu zilizokuwa na mashtaka 11, dr. Mkumbo amekuwa kimya akisubiri hatma yake,tofauti na wenzie ambao wameendelea kuhangaika kwa kisngizio cha kupigania haki yao ndani ya chama hata kabla ya chama kutoa hitimisho.

Zitto Kabwe ndio huyo yuko Kigoma akiomba huruma ya wananchi,Mwigamba ndio huyo katia timu kwa msajili wa vyama.

Swali linakuja ni kwanini hawa wawili wanatafuta utetezi nje ya chama chao mapema?Na kwa nini dr. Mkumbo katulia akisubira maamuzi ya vikao vya chama?

Je ni kutofautiana kwa viwango vyao vya elimu ndio kulikowatofautisha?Hakika dr. Mkumbo umenikosha sana na ukimya wako hivyo kuthibitisha kwamba hakika ww ni msomi uliye elimika.

GUILTY ARE ALWAYS AFRAID.

Hongera sana dr. Mkumbo.

Nawasilisha.
 
yule ndo alikua anawapeleleza wenzie mwisho wa siku akawachoma kamati kuu. so alijua afanyacho. mimi nashukuru coz bila yeye tusingejua mm.
 
Wana Jf nimefurahishwa sana na tabia ya dr kitila mkumbo,nimemfuatilia sana tangu zilipoibuliwa tuhuma dhidi yake pamoja na zitto na samson mwigamba.dr amekuwa katika hali ya utulivu mkubwa kuliko watuhumiwa wenzie.maana baada ya kamati kuu kuwavua nyadhifa zao na kuwapa siku 14 dr amejitokeza mara mbili tu kwenye media kuzungumzia suala hilo.kutokana na sababu hiyo nimeanza kuamini kwamba maneno aliyosema kwenye kamati kuu kwamba aliingizwa tu kwenye mkenge na zitto pamoja na mwigamba ni ya kweli.nasema hivyo kwa sababu ukiangalia baada ya wote wa 3 kurudisha fomu zilizokuwa na mashtaka 11 dr mkumbo amekuwa kmya akisubiri hatma yake,tofauti na wenzie ambao wameendelea kuhangaika kwa kisngizio cha kupigania haki yao ndani ya chama hata kabla ya chama kutoa hitimisho.zitto kabwe ndio huyo yuko kigoma akiomba huruma ya wananchi,mwigamba ndio huyo katia timu kwa msajili wa vyama.swali linakuja ni kwanini hawa wawili wanatafuta utetezi nje ya chamachao mapema?na kwa nini yy dr mkumbo katulia akisubira maamuzi ya vikao vya chama? je ni kutofautiana kwa viwango vyao vya elimu ndio kulikowatfautisha? hakika dr mkumbo umenikosha sana na ukimya wako hivyo kuthibitisha kwamba hakika ww ni msomi uliye elimika.GUILTY ARE ALWAYS AFRAID.hongera sana dr mkumbo.nawasilisha.

kumbe umeona umhimu wa elimu? mbona kwenye waraka waliposema ""elimu ya mkuu wa taasisi si tu ni ndogo bali pia ni ya maghumashi"" mlikasirika? kumbe waraka ulikuwa sahihi!!
 
umeandika pumba, waraka wa Kitila unaishi, kama ule waraka wa chacha wangwe

Kitila alisema hata zitto alikuwa haujui, leo hii unasema kitila alisema alidanganywa na zitto, acha kushusha hadhi ya dr. kudanganywa na zitto

kuhusu ukimya, kitila siku zote yuko hivyo......................msilazimishe zitto awe kimya

myakoma mwaka huu na ujao

mlianza wenyewe na tuliwaonya mnaweweseka sasa

narudia kitila hawezi kudanganywa na zitto, wadanganye huko vijiweni

div. 5 noma sana
 
Hakuna awezaye kunena maneno makuu kuliko fikra zake, japokuwa ni kweli kwamba tuyanenayo ni sehemu tu ya yale tuyawazayo akilini mwetu.
 
CHADEMA bana wanafurahisha, ukikubaliana na upuuzi wa wakina Lema, Mbowe, Slaa na Josephine unaonekana shujaa, una hekima na msomi. Ukiwapinga kwa ubadhirifu wao na uhafidhina unaonekana msaliti! Zitto ndio main character hapa hao wengine walikuwa wancheza supporting roles tu! usiwafananishe! Zitto has a lot at stake!
 
Dr ni muajiriwa wa serikali,ni marufuku muajiliwa wa umma kujinadi kwenye majukwaa ya siasa,akichabikia chama chochote cha siasa,unataka wanawe wasiende chooni?
 
Naunga mkono hoja ya ukimya wa Dr. Kitilla ila pia
Kuna ukimya wa aina mbili, ule ukimya wa mtu hana la kusema na ule ukimya wa kuamua tuu kutosema!.

Kuna ukimya wa kusubiria hatima, ila ila kama tayari umeishaijua hatima, huna haja ya kuisubiria kimya!.

Dr. Kitilla anaisubiria hatima!, Zitto anaijua tayari!, wala hausubirii!.

Ila pia kuna kimya kingi chenye mshindo mkuu!.

Pia shishangai kama walivyo kuku, kuna kuku akishikwa kuchinjwa, anatulia tuu anachinjwa kama afanyavyo kondoo!, na kuna kuku akishikwa kuchinjwa, lazima akukuruke!.

Kwenye tuhuma zozote, ukimya ni admission of guilt, Dr. Kitilla alikubali tangu day one, kuwa yeye ndie initiator wa ule waraka na kumshirikisha Mngamba!, hivyo kunyamaza na kusubiria ni halali yake!.

Zitto anasingiziwa!, hatma yake iliishaamuliwa siku nyingi!, alikuwa anatafutiwa sababu tuu!, kwa nini anyamaze?!. Atulie tuu achinjwe kama yule kuku kondoo?!.
Pasco.
 
bado hajatulia huyo usimpe sifa na wasifu wa kijinga.

ukitaka kujua tembelea fb kwenye wall ya msando ndo utajua kuwa yupo hivyo unavyodai au la...

kimsingi hawa watu wanamatatizo haswa...
 
Nashukuru na ww kwa kuchangia pumba zako mkuu.maana ukitaka kujua akili ya mtu na kumpa nafasi ya kusema au kutenda.
 
Zito anapoteza tu muda majukwaani suala lao litamalizwa na vikao vya chama kwa mujibu wa katiba.
Haliwezi kuishia jukwaani kasulu wala kigoma mjini Dr Mkubo yupo sahihi kuwa na subira.
 
Naunga mkono hoja ya ukimya wa Dr. Kitilla ila pia
Kuna ukimya wa aina mbili, ule ukimya wa mtu hana la kusema na ule ukimya wa kuamua tuu kutosema!.

Kuna ukimya wa kusubiria hatima, ila ila kama tayari umeishaijua hatima, huna haja ya kuisubiria kimya!.

Dr. Kitilla anaisubiria hatima!, Zitto anaijua tayari!, wala hausubirii!.

Ila pia kuna kimya kingi chenye mshindo mkuu!.

Pia shishangai kama walivyo kuku, kuna kuku akishikwa kuchinjwa, anatulia tuu anachinjwa kama afanyavyo kondoo!, na kuna kuku akishikwa kuchinjwa, lazima akukuruke!.

Kwenye tuhuma zozote, ukimya ni admission of guilt, Dr. Kitilla alikubali tangu day one, kuwa yeye ndie initiator wa ule waraka na kumshirikisha Mngamba!, hivyo kunyamaza na kusubiria ni halali yake!.

Zitto anasingiziwa!, hatma yake iliishaamuliwa siku nyingi!, alikuwa anatafutiwa sababu tuu!, kwa nini anyamaze?!. Atulie tuu achinjwe kama yule kuku kondoo?!.
Pasco.

Kuku ukimchinja na kumuacha kabla hajakata roho lazima akukuruke iwe kwa hiari yake ama kwa kulazimishwa. Kwa kitila lazima atulie yupo kwenye uchunguzi na mwajiri wake. Kwa zitto lazima atuoneshe upande wa pili wa shilingi ili hata akifukuzwa tusianze kusema "amefukuzwa ndo maaana anasema hili na lile.....alikuwa wapi?". Hakika hii ngoma ni nzito kweli kweli.
 
Naunga mkono hoja ya ukimya wa Dr. Kitilla ila pia
Kuna ukimya wa aina mbili, ule ukimya wa mtu hana la kusema na ule ukimya wa kuamua tuu kutosema!.

Kuna ukimya wa kusubiria hatima, ila ila kama tayari umeishaijua hatima, huna haja ya kuisubiria kimya!.

Dr. Kitilla anaisubiria hatima!, Zitto anaijua tayari!, wala hausubirii!.

Ila pia kuna kimya kingi chenye mshindo mkuu!.

Pia shishangai kama walivyo kuku, kuna kuku akishikwa kuchinjwa, anatulia tuu anachinjwa kama afanyavyo kondoo!, na kuna kuku akishikwa kuchinjwa, lazima akukuruke!.

Kwenye tuhuma zozote, ukimya ni admission of guilt, Dr. Kitilla alikubali tangu day one, kuwa yeye ndie initiator wa ule waraka na kumshirikisha Mngamba!, hivyo kunyamaza na kusubiria ni halali yake!.

Zitto anasingiziwa!, hatma yake iliishaamuliwa siku nyingi!, alikuwa anatafutiwa sababu tuu!, kwa nini anyamaze?!. Atulie tuu achinjwe kama yule kuku kondoo?!.
Pasco.

Hali halisi hakuna sababu ya kuhangaika huku na kule wakati amepeleka hoja za kujenga utetezi kwenye uongozi wa juu chamani. Alichofanya Kitila Mkumbo ni sahihi, maana kwa sababu za msingi anachofanya Zitto na mwenzake Mwigamba hazina msingi wakati hatima yao bado hijafikiwa na wala kuitwa katika jopo la kujenga utetezi wao. Sasa povu lote analotoa huko Kigoma na kuvimbisha mishipa kwamba anazunguka nchi nzima kuna mantiki gani?

Nani anaratibu na kugharimia mikutano hiyo ya Zitto kama sio CCM ambayo imeacha suala zito la mawaziri kujiuzuru kwa kashfa ya kushindwa kazi wao wako busy na Chadama? Kinachoendelea CCM inafanya kila liwezekanalo Zitto asiondoke Chadema kwa vile ni chombo muhimu kwao ndio maana wako kwa hali na mali kuhangaikia hilo kuliko yanayowasibu.

Zitto anazidi kuonyesha uwezo wake wa kupima na kusoma nini kifanyike na nini kisifanyike kupwaya mno, na kwamba hekima na busara hana.
Hata ile kitu inaitwa common sense hana. Hata taratibu kama za mahakama huwa kesi ikiwa katika mwenendo basi huna budi kusitisha kuzungumzia hadi uamuzi utakapofikiwa, vinginevyo anachofanya sasa anaharibu mwenendo wa kesi yake.
 
Siwezi kusema kweli alidanganywa na zito ila anachofanya zito ni siasa za kijinga na inaonesha kweli alitumwa na ccm kuivuruga cdm. Kina lowasa walivyotukanwa mara zote na kutishiwa kufukuzwa waliamua kukaa kimya na sasa wanaonekana washindi. Zito anajifanya mjuaji mno
 
Binafsi nampongeza dr. Kitila kwa utulivu wake, tatizo la zitto haeleweki, mara aseme hivi na afanye vile, hakukuwa na haja mapema kwenda kulialia kwa wanakigoma! Kuwaingiza wanakigoma kwenye ugomvi wa zitto na chadema, ili ionekane ni ugomvi wa chadema na wanakigoma sio sawa! Zitto ilitakiwa apambanie uwanachama wake kwenye cc ya chadema na sio kwenda kulialia mwandiga!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom