Dogoli kinyamkela
JF-Expert Member
- Nov 21, 2024
- 2,144
- 3,459
POMBE NI KINGA YA UKWELI KATIKA ASILI.
Kuna maneno mazito sana katika ulimwengu wa kale: wakati babu zetu walipo tumia kinga ya ulevi kusema Ukweli. Walijua wazi kuwa
“Ukweli ni mchungu na huumiza, lakini Uongo ni mtamu lakini Huua.” karibu katika meza ya
Katika jamii nyingi za asili, watu walijua kwamba kusema ukweli mbele ya hadhira ni tendo la ujasiri, si la kawaida. Ukweli unaweza kuvunja heshima, kuumiza nafsi, au hata kuanzisha vita lakini bado ni lazima usemwe.
Sasa ili hkuusema, walihitaji kifaa cha kinga ya roho.
Mababu walibuni kinga rahisi lakini lenye maana kubwa sana tena sana kinga hii ilikuwa ni "Pombe"
Katika utamaduni wa Kiafrika, pombe ya kienyeji haikuwa kileo cha starehe bali ni kiapo cha uaminifu.
Mtu hakunywa ili kupoteza fahamu, bali ili kufungua mlango wa nafsi.
Alipotaka kuongea jambo zito "SIRI" au MALALAMIKO, au UKWELI wa muda mrefu aliokuwa ameuficha. Basi alikunywa kidogo ili moyo wake uwe mwepesi. Hii ni tofauti na mazingira ya sasa.
Kale Pombe ilikuwa dawa ya kusema ukweli bila woga.
Wenye hekima walijua sio pombe iliyokuwa ikizungumza, bali roho iliyokuwa imefunguliwa.
Hivyo basi, kama babu alikuwa na jambo alisema “Acha kwanza nikunywe kidogo kabla sijasema,” Hii ni Code ya Asili nakupa🤣 walimaanisha
“Acha nijiandae kusema ukweli niliouficha kwa muda mrefu.”.....
Kati ya Wakweli Wote Mlevi Hushika Namba Moja....
Kuna tabaka tatu za wakweli katika maisha:
Tabaka la kwanza ni Mtoto
Mtoto hasemi uongo kwa sababu hajajifunza hofu. Hata kama unatafutwa na wauwaji ukajificha na kumwambia mtoto nenda kawambie sipo. Mtoto atasema hivyo hivyo.
"Baba Amesema hayupo"😂😂
Tabaka la pili ni Mlevi
Mlevi hasemi hasemi uongo kwa sababu ameshinda hofu. Yani ni kwamba mlevi huwa haogopi hata kama Anaongea na bosi wake siku hiyo Atamchana ukweli mpaka Dunia ishangae...
Tabaka la tatu kwa siku ya leo ni Mzee mwenye busara
Wazee hawa kama Akina warioba hawasemi uongo kwa sababu anaijua thamani ya ukweli.
Watatu hawa ni walimu wa maisha.
Mtoto hukufundisha usafi wa moyo, mlevi hukufundisha ujasiri wa kusema, na mzee hukufundisha hekima ya wakati sahihi.
Ukijifunza kutoka kwao, unakuwa mtu wa ukweli katika kila hali mahala popote hata kama kutanzi kiko shingoni kwa sababu tu Umeishinda Hofu.....
Watu wengi wa leo huchanganya ulevi na upumbavu.
Lakini pombe si tatizo ila matumizi yake yasiyo na hekima ndiyo sumu.
Wababu zetu walikunywa kiasi; walikunywa ili kufikiri, si kusahau.
Walijua pombe nyingi huzima akili, lakini pombe kidogo hufungua milango ya kutafakari.
Kwao, pombe ilikuwa mbolea ya mazungumzo ya kweli.
Ilitumika kwenye baraza la wazee, tambiko, na hata mapatano ya amani.
Hapo ndipo ukweli ulizungumzwa bila hofu wala unafiki.
Walevi wa kweli waliheshimiwa kwa siri.
Mtu alipolewa na kuanza kuongea kwa sauti kubwa, watu hawakumcheka.
Walijua mlevi ni kinywa cha roho, anasema maneno ambayo akili za kawaida zimeziba.
Ndani ya maneno yake, kuna ujumbe wa kiroho, onyo, siri ya jamii, au funzo kwa vizazi.
Kwa hiyo wazee walisema:
“Mlevi akiongea, usimcheke. Tafuta maana ndani ya maneno yake.”
Kwa sababu mara nyingi, ukweli wa jamii hupatikana kwenye maneno ya walevi.
Leo hii, watu wengi wanakimbia ukweli kama ugonjwa.
Tunaogopa kusema, tunaogopa kusikia, na tunaogopa kukosolewa.
Lakini ukweli haubadiliki hata ukifunikwa kwa miaka, siku moja utatoka.
Na atakayeusema, huenda akaitwa mlevi, mwenda wazimu, au asiye na adabu. Haya ndio yamemkuta Capten Tesha
Lakini kumbuka:
Ujasiri wa kusema ukweli ni kipimo cha uhai wa nafsi.
Kama baba yangu alivyo wahi kuniambia kuwa :
“Kama mtoto wako ni mkimya kupita kiasi, mpe pombe kidogo. Asipoongea hata baada ya hapo, basi jua amezimika ndani.” yani nimsukule....
Maneno hayo ni fundisho kubwa.
Si lazima utoe pombe bali toa nafasi, toa ujasiri, toa uhuru.
Kwa sababu mtu ambaye hawezi kusema ukweli wake, amefungwa kiroho.
Siku moja, utakaa mbele ya watu na utamani kusema ukweli wako.
Utahisi hofu, mashaka, na aibu.
Ndipo utakapo kumbuka hekima hii ya kale:
Sio pombe yenyewe inayohitajika, bali kile pombe kilichowakilisha ujasiri wa nafsi.
Kwa hiyo ukihisi moyo unatetemeka kabla ya kusema ukweli,
mwambie nafsi yako:
“Leo sitalewa kwa pombe, nitalewa kwa ukweli.”
Kwa sababu ulevi wa kweli ni ule wa kusema bila woga, kusimama bila hofu, na kuishi bila unafiki.
Ndugu yangu kama umesoma mpaka mwisho na ukaelewa vizuri ninunulie bia 🍺 moja tu leo ninataka nilewe......
Kuna maneno mazito sana katika ulimwengu wa kale: wakati babu zetu walipo tumia kinga ya ulevi kusema Ukweli. Walijua wazi kuwa
“Ukweli ni mchungu na huumiza, lakini Uongo ni mtamu lakini Huua.” karibu katika meza ya
Mkushi Dr. DOGOLI KINYAMKELA ☠️💀 Tuangalie asiliKatika jamii nyingi za asili, watu walijua kwamba kusema ukweli mbele ya hadhira ni tendo la ujasiri, si la kawaida. Ukweli unaweza kuvunja heshima, kuumiza nafsi, au hata kuanzisha vita lakini bado ni lazima usemwe.