Pombe na bangi havina tofauti

Pombe na bangi havina tofauti

uvugizi

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
1,351
Reaction score
1,100
Lupulin ni formula ya pombe inayopatikana katika shayiri (hops) , ambayo inatumika katika pombe . kile kiuchungu unachokisikia katika beer zote au pombe lupulin ndiyo chanzo.

Ule uchungu wa lupulin ukichanganyika na ethyl alcohol unapata Narcotic ( dawa za kulevya zipo kundi hili). Madhara makubwa sana yanakuja katika ubongo.

Lupulin chemical formula yake ni C32H5007.

Cannabinol ambayo ndiyo inayotoa kitu kinaitwa Marijuana cigarettes au bangi kwa kiswahili chetu formula yake ni C21H3002.

Cannabinol + lupulin au kwa maana nyingine hizi zote zimetengenezwa na chemical element za aina moja .

Lupulin = beer kutoka mmea wa hops

Cannabinol = bangi kutoka mmea wa hemp plant .

Wanasayansi wamebaini ( botanical scientists) kuwa hemp na hops sawa na lupulin na cannabinol , Mimea hii imetoka kwa baba mmoja mama mmoja ( same family) .

Refer. America international Narcotics research foundation.

My concern kuandika andiko hili , nikumpa mtu taarifa yenye research ili hata ukisoma kuhusu pombe, ujue si Maandiko tu yamekataza Bali hata tafiti za kisayansi pia.

maana kanisa na watumishi wa Mungu wa Leo wanaangamizwa kwa kukosa maarifa ( Hosea 4:6).

Kanisa lisilo na research halitakuwa na information hivyo linaangamia. Kwa sababu shetani amejawa na information , yaani mchawi anaweza kukuchunguza we we mtakatifu rohoni ila wewe uliye mwana wa Mungu na ni roho huwezi. AIBU.

Waliofanya tafiti kwa nini watu wanakuwa walevi wa kupindukia ( steady alcoholic) walibaini sababu kubwa ni vitisho vya tangu utotoni , kuogopeshwa na kujawa na hofu , kwa maana nyingine walevi wengi ni watu waoga.

Dr . George W.crane katika tafika zake from Ohio state university alisema , pombe siyo stimulant ni depressant in some stages hata ikitumika kidogo au kwa wingi , hakuna kitu kama kunywa kwa kiasi linapokuja swala la narcotics ( dawa kama za kulevya kama pombe( moderation with safety).

Kujitenga ni swala la pekee kuhusiana na pombe .

Katika tafiti zake Dr George W. Crane alisema " smartest people don't drink". Watu makini hawalewi.

Kibiblia pombe haina nafasi kabisa, ingawa kuna watu wanataka kuihalalisha kupitia maandiko ya 1 Timothro 5:23 .

Nitaleta siku nyingine biblically , kibiblia pombe inatumika kama dawa mpaka Leo.

Wanasayansi wanabishana mpaka sasa hivi ulevi wa pombe ni ugonjwa au matokeo yake kama cirrhosis nk , na kama ukiitwa ni ugonjwa basi uwe ni self inflicted disease. Kwa mujibu wa taasisi ya American medical association , ugonjwa ni kile kitu ambacho mchango wako haukuwepo sana au hukusababisha consciously .ingawa padre Guido stuer M.afr katika kitabu chake anasema ulevi ni ugonjwa na unatakiwa kupona , ameelezea pombe inavyokunywa wewe badala ya wewe kuinywa.

Ameanisha mpaka stages za ukuaji wa kileo na hatua za kutoka subconsciously na spiritually .
 
Basi sawa ila ujue hapa TZ pombe inaingiza mapato mengi serikalini...Kwa hiyo POMBE IHESHIMIWE
 
MKUU ACHANA KABISA NA POMBE.ANAKUNYWA FUKARA HADI TAJIRI.ANAKUNYWA MCHUNGAJI/SHEHE HADI MUUMINI.
Pombe ina hadhi yake mkuu kama hujui kamwage pombe ya mlevi bar.
 
Mpe mlevi pombe asahau shida zake

Usiangaike na mwili mkuu angaika na roho

Muhudum leta glass [emoji445][emoji444]
 
Walevi wengi ni watu waoga??!are u seriously? Sayansi uchwara hizo!
 
Ngoja niongeze chupa nyingine alafu niusome uzi wako vizuri...
 
Hivi kwanini mnapenda kuuhusisha mmea pendwa na mambo ya ajabu ajabu,hebu niletee maandiko ya kitabu cha imani yoyote kilichokataza na kuitaja bangi kwa jina.
 
Mnajaribu kutufitinisha ili tuachane [emoji23][emoji23] mkimaliza tafiti zenu njooni hapa tugonge Heineken tujipongeze hakuna namna.
 
Mbona stimu zipo tafauti kama ni kitu moja?
Huwezi fananisha bangi na gongo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom