Polisi wazingira mgodi wa Bulyanhulu

Polisi wazingira mgodi wa Bulyanhulu

Ah!!!!
Thursday, May 25, 2017
Polisi wazingira mgodi wa Bulyanhulu


pic+mgodi+wa+bulynkulu.jpg



Kwa ufupi
  • Jeshi hilo limefanya hivyo baada ya Tellack kuagiza kuimarisha ulinzi katika eneo lote la mgodi huo kuhakikisha hakuna mtu anayetoka wala kuingia.
By Peter Saramba, Mwananchi
Kahama. Jeshi la Polisi limeuzingira mgodi wa Bulyanhulu baada ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Tellaack kuzuiwa kuingia katika mgodi huo alikokwenda kukagua iwapo uzalishaji unaendelea bila kuwepo kwa Maofisa wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini nchini (TMAA).

Jeshi hilo limefanya hivyo baada ya Tellack kuagiza kuimarisha ulinzi katika eneo lote la mgodi huo kuhakikisha hakuna mtu anyetoka wala kuingia.

Mapema leo, Mkuu huyo wa mkoa alitembelea mgodi mwingine wa Buzwagi ambao pia unamilikiwa na kampuni ya Acacia kama ulivyo ule wa Bulyanhulu.

Katika mgodi wa Buzwagi, Tellack na msafara wake waliruhusiwa kuingia na kishuhudia shughuli za uchimbaji ukiwa umeshitishwa kwa kukosekana maofisa wa TMAA walioondoka mara baada ya Rais Magufuli kutangaza kuvunja bodi na kutengua uteuzi wa watendaji wakuu wa wakala hiyo.
Kumbe maofisa huwa wanakuwepo uzalishaji unapofanyika!!!!!!! Duh!!! Tumeliwa sana.
 
Inahitajika busara kubwa sana kuihandle hii ishu, bila shaka wanasheria wa ACACIA wapo chimbo wanajipanga, natamani na wa kwetu wawe maeneo wakiandaa nondo za kutetea kilicho chetu........vinginevyo tutakuja kutupiana Mpira hapa, kila MTU akikana msimamo wake na mwisho ikawa aibu kwa TAIFA.
Acheni uoga ******* nyie. Haya madini yapo nchi ya nani. Hawataki wasepe. Mbona uarabuni mafuta yao hawazinguliwi hivo. Nyie ndo mnaotuletea kauzibe
 
Acheni uoga ******* nyie. Haya madini yapo nchi ya nani. Hawataki wasepe. Mbona uarabuni mafuta yao hawazinguliwi hivo. Nyie ndo mnaotuletea kauzibe
Mkuu punguza maneno makali,ila hao uliyowataja kuwa ni was-- na wametuingiza ktk
Dimbwi hilo wapo na wana tesa tu

Ova
 
Wakati mwingine viongozi wanafanya kazi nzuri,wakati mwingine wanafanya makosa kwa kujiona wao ndio mwisho wa mambo yote,inamaana mkuu wa mkoa hakujua kuwa anatakiwa aongozane na TMAA katika kufanikisha kazi hiyo?.
..r you serious, aandamane na watu ambao wanatuhumiwa kwa kusababisha upotevu wa mapato ya nchi??
 
Inahitajika busara kubwa sana kuihandle hii ishu, bila shaka wanasheria wa ACACIA wapo chimbo wanajipanga, natamani na wa kwetu wawe maeneo wakiandaa nondo za kutetea kilicho chetu........vinginevyo tutakuja kutupiana Mpira hapa, kila MTU akikana msimamo wake na mwisho ikawa aibu kwa TAIFA.
Inabidi tujipange kupambana nao kisheria zaidi isije ikala kwetu.
Tunarudi 67......aliko feli Nyerere mpaka akaachia kwa hiari
Leteni ushamba tu,mtaaibika mda sio mrefu.msinihusishe
Hii ndio Kampeni inayofanywa na siri-kali ya Dr. Pombe ya kuwavutia wawekezaji.

Yule waziri amesema wakija na vyerahani 4 , tayari ni kiwanda. Tutegemee wawekezaji kufungua viwanda 42 elfu. Ukichanganya na vile 52elfu ambavyo tayari vipo, nchi hii itakuwa ya uchumi wa viwanda kweri kweri.
Serikali itatugawia na tutagawana umasikini kweri kweri na kila mdanganyika atatosheka.

Link Tanzania nchi yenye viwanda vingi Afrika Mashariki

Link2. Waziri Mwijage: Kwa sasa Tanzania ina zaidi ya viwanda 52, 000

Warioba aliamua kuisaidia CCM "yake" kwa kuwaletea Rasimu ambayo ingewaokoa lakini waliamua kumfanyia upasuaji bila sindano ya ganzi. Leo wanaleta "maigizo" matakatifu kama ya "samaki wa Magufuli".

Wacha tu serikali iendelee kutugawia umasikini kwa kutushirikisha kihamasa naa kihisia kwenye maigizo yao.

Miswada ya sheria watunge wao.
Semina za kupitisha miswada ya sheria kwa wabunge wa CCM na kuwaweka sawa wabunge wa CCM wazifanye wao.
Sheria za kusamehe kodi wawekezaji wanazitengeneza wao
Mikataba "mibovu" waingie wao.
Na Pia "Uzalendo" wajivishe wao?

Eee, Mungu tumekosea wapi sisi wadanganyika?
 
Wale vigogo wa mgodi waliokaidi amri ya mkuu wa mkoa watiwe ndani for 48 hours ili washike adabu, ila hawa wengine 'manamba' waachiwe waenende zao kwa 'Amani ya Bwana'. Wao sio decision maker kwa hiyo hawakuwa na maamuzi ya nani aingine na nani asiingie mgodini... Pole mkuu wa mkoa kwa kudharauliwa ndani ya himaya yako!
Hawa vigogo wa machimboni wametibia saaaaaaana. Nadhani yamebaki mashimo tu.
 
acacia wafungashe kila kilicho chao waondoke tuone nani ataye umia na kuomba pooo!
 
huu ni uvamizi wa mali ya muwekezaji..Kwa kuwa Tanzania ina watu wana akili kama nxi wa chooni watashangilia sana laiki madhara ya hiki kinachofanyika ni makubwa sana sana kupata kutokea katika historia ya nchi hii..Jikumbusheni zimbabwe walifanywa nini kwa ajili ya mambo ya hovyo hovyo kama haya..Serikali imepewa mgodi wa Tulawaka na ACACIA wakaachiwa kila kitu mpaka toilet paper mwaka haujafika wameshindwa kuendesha mgodi umefungwa ..sasa endeleeni kushangilia tu kama maainzi ya chooni yameona kinyesi mtakuja kujuta
 
Acheni uoga ******* nyie. Haya madini yapo nchi ya nani. Hawataki wasepe. Mbona uarabuni mafuta yao hawazinguliwi hivo. Nyie ndo mnaotuletea kauzibe
Uarabuni what?
wewe sio kukojoa, kanye kabisa ndio ulale .
Unajua sanctions zilivyoumiza biashara ya mafuta Iran ?
Unadhani Iraq iko Africa?
Na Syria je?
Na Afghanistan?
Umeiona Libya?

Kaa kimya uwafichie wazazi wako aibu
 
Kula kwetu ni lazima tu Mkuu, tumekosa umakini wa kukaa chini kama Watanzania kutafakari kwa kina ili kujinasua katika hii mikataba iliyojaa ufisadi. Kwa mara nyingine tena WAMEKURUPUKA!

inachoniuma zaidi ni hii hali ya mtu mmoja kujiona ana akili saana na uwezo mkubwa wa kufikiri kuliko sisi soote mpaka kufikia kufanya maamuzi kwa utashi wake ambapo itakapotokea madhara tutaathirika sote....
haya mambo yalitakiwa yatengenezewe mjadala wa kitaifa kisha na wao kuchukua maoni yetu ili hata kama likitokea baya mbeleni tujialaumu woote...

ila ninachokiona hizi phds zitatuachia matatizo makubwa saaana mpaka hawa wote waondoke sijui itakuaje yaaani naona giza kila nikitafakari kwa kina
 
  • Thanks
Reactions: BAK
..r you serious, aandamane na watu ambao wanatuhumiwa kwa kusababisha upotevu wa mapato ya nchi??
Kwani hujasoma kuwa hata katika mgodi alioruhusiwa kuingia aliondoka kwa kuwa hakukuwa na watu wa TMAA?.
 
I am result oriented person... Yes, it sounds good and I like it lakini muhimu kwangu score board itasoma nini baada ya dakika 90!!

Tanzania ni zaidi ya uijuavyo!! Unaweza kuta tunashangalia vyenga, makanzu, matobo na kila mbwembwe za soka! Tunashambulia lango la adui kama nyuki!

In no time, inapigwa bonge la counterattack na sekunde 10 baadae, tunaokota mpira kwenye nyavu zetu wenyewe!!!

Haidhuru, wapo watakaokuja na kusema... sio kwa Stars hii ya Samatta!
ishu za msingi unaleta upuuzi wako,kama una nyege za mpira nenda uwanjani
 
Kwani hujasoma kuwa hata katika mgodi alioruhusiwa kuingia aliondoka kwa kuwa hakukuwa na watu wa TMAA?.
Hakwenda pale ili awakute watu wa TMAA..anafahamu hawapaswi kuwepo baada ya bodi yao kuvunjwa, alikwenda ili aone kinachoendelea pale mgodini na kuwaambia wasiendelee na baadhi ya kazi pasipokuwepo watu wa serikali..sasa wewe unasema tena angefuatana nao TMAA, wa nini???
 
Pole sana Majangili wala siyo wazungu ni Watanzania wenzetu tuliowapa Dhamana akina Che Mkapa na JK.Usiwalaumu wazungu wakati kuna Watanzania wanaakili za kujaza choo tu.Wanafikiria matumbo yao ndiyo sababu sitompongeza wala kumpigia makofi Magufuli maana alikuwepo kwenye kufunga sheria zenye ukakasi,wakawatukana Wapinzani tena kwa mbwembwe za kuwaita kila majina mabaya leo ati tuwaite wazalendo kwa lipi.

Mafuta Majanga hula na wakwao
Iko sahihi huwezi kutengeneza tatizo ili ukijaribu kukitatua eti unataka upigiwe makofi.
 
Acheni uoga ******* nyie. Haya madini yapo nchi ya nani. Hawataki wasepe. Mbona uarabuni mafuta yao hawazinguliwi hivo. Nyie ndo mnaotuletea kauzibe
Kweli bangi na viroba ni hatari kwa vijana
 
simlaumu Acacia sitakajua kumlaumu hata siku moja ,ujinga na ngiriba za ccm zimetufikisha hapa kumbukeni hata sauti ya ukali alioitumia mkapa kuwatetea wawekezaji walioitwmakaburu akatwambie tukome mwisho wasiku ccm ikaridhia kupisha huu unyapala wa ubinafsishaji kwenye mikutano ya chama hakusema magufuli wala nani mule ndani,eti leo tunajishebedua kuwa tumeibiwa sana hadi mnataka kulia bado hatua zinazo chukuliwa ni zilezile za kuingiza taifa kwenye mess
 
Back
Top Bottom