Polisi wawanasa wahamiaji haramu 11 wakitoka Tabora kwenda Mbeya

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia wahamiaji haramu kumi na moja [11] raia wa nchini Rwanda na Burundi kwa kosa la kuingia nchini bila kuwa na kibali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei ameeleza kuwa wahamiaji hao walikamatwa mnamo Februari 7, 2022 majira ya saa 12:00 jioni katika kizuizi cha Polisi Chalangwa kilichopo Kata ya Chalangwa, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, wakiwa wanasafiri ndani ya gari lenye namba za usajili T.295 DBQ Basi mali ya Kampuni ya Prince Ahmed wakitokea Tabora kuelekea Mbeya.

Wahamiaji hao wakiwemo watoto wadogo sita [06] wafahamika kwa majina:-

1. AKULIMANA EMANUEL [40]
2. QUIZERA RACHEL [32]
3. AMANI HORESI [32],
4. TUYIZERE WELLORL [32]
5. MOSES RAPHAEL [20]
6. KWIZELA WILES, mwaka 1.5
7. BUMTUBWIMINO JEHOVANIS [14]
8. MIYOBYOSE JUSTIN [06]
9. ISHIMWE ALINE [15]
10. SHIMI ARENI [15]
11. WIZEMANA CRIMANTINE [15]

Watuhumiwa wanafanyiwa mahojiano na kisha watakabidhiwa idara ya uhamiaji kwa hatua zaidi za kisheria.
 
Hii ni misingi ya kikoloni!.
Yani ukifikiri kwa undani unakuja kujua binadamu kama sometimes ha-make sense hivi! Just unakuwa haramu kwenye mazingira ya dunia mahali ulipozaliwa..🤣

Okay wacheni tutii Sharia bila shuruti maana ndo dizaini ya maisha tuliyochagua.
 
Nchi hii ina matundu kila kona, hao wahamiaji kuna sehemu mpaka wanafanya vibarua kabisa licha ya kuingia na kutoka.
 
Hii ni misingi ya kikoloni!.
Yani ukifikiri kwa undani unakuja kujua binadamu kama sometimes ha-make sense hivi! Just unakuwa haramu kwenye mazingira ya dunia mahali ulipozaliwa..🤣

Okay wacheni tutii Sharia bila shuruti maana ndo dizaini ya maisha tuliyochagua.
Ubinafsi.
 
Hawana tu pesa mbona muda tu , tena wangetafutiwa na usafiri kabisa wakuwafikisha huko
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia wahamiaji haramu kumi na moja [11] raia wa nchini Rwanda na Burundi kwa kosa la kuingia nchini bila kuwa na kibali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei ameeleza kuwa wahamiaji hao walikamatwa mnamo Februari 7, 2022 majira ya saa 12:00 jioni katika kizuizi cha Polisi Chalangwa kilichopo Kata ya Chalangwa, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, wakiwa wanasafiri ndani ya gari lenye namba za usajili T.295 DBQ Basi mali ya Kampuni ya Prince Ahmed wakitokea Tabora kuelekea Mbeya.

Wahamiaji hao wakiwemo watoto wadogo sita [06] wafahamika kwa majina:-

1. AKULIMANA EMANUEL [40]
2. QUIZERA RACHEL [32]
3. AMANI HORESI [32],
4. TUYIZERE WELLORL [32]
5. MOSES RAPHAEL [20]
6. KWIZELA WILES, mwaka 1.5
7. BUMTUBWIMINO JEHOVANIS [14]
8. MIYOBYOSE JUSTIN [06]
9. ISHIMWE ALINE [15]
10. SHIMI ARENI [15]
11. WIZEMANA CRIMANTINE [15]

Watuhumiwa wanafanyiwa mahojiano na kisha watakabidhiwa idara ya uhamiaji kwa hatua zaidi za kisheria.
Nakumbuka kuna siku nilikuwa nataka dodoma naenda mbeya,kuna eneo karibia na mtera kuna kizuizi pale basi linasimama kisha kuna askari wa uhamiaji anaingia ndani na kuanza kuotea mmoja baada ya mwingine katika kumsalimia......Naona tanzania sasaivi tupo vizuri sana katika mitego ya kuwatambua raia ambao sio
 
Back
Top Bottom