Wahamiaji haramu tisa wa Kenya wakamatwa Dodoma Tanzania

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Polisi mkoani Dodoma nchini Tanzania limewakamata wahamiaji haramu tisa ambao ni raia wa Kenya kwa kosa la kuingia nchini kinyume cha sheria katika matukio mawili tofauti.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumamosi Februari 15, 2000, Kamanda wa polisi mkoani Dodoma, Gilles Muroto amesema wahamiaji hao kati yao watatu ni raia wa Kenya wenye asili ya Somalia waliokamatwa katika Kijiji cha Mtera wilaya ya Mpwapwa, Dodoma.

Amewataja raia hao ni Abdirahman Mohamed (25) Luul Mohamed (30) na Hawa Gedow (18) wakitokea nchini Kenya kwenda nchini Zambia kupitia Mkoa wa Songwe Tanzania .

Muroto amesema raia hao walikuwa kwenye gari lenye namba za usajili T. 248 AWA aina ya Nissan Patrol rangi nyekundu likiendeshwa na Kelvin Mpoli mkazi wa Himo mkoani Kilimanjaro ambaye ni mwalimu wa shule ya sekondari Kifaru Wilaya ya Mwanga mkoani himo akiwa na Cathbert Kirita (58) mmiliki wa gari hilo.

Katika tukio lingine, wahamiaji haramu sita walikamatwa Februari 3, 2020 kata ya Haneti Wilaya ya Chamwino wakitokea mkoani Arusha kwenda Mbeya.

Amesema walikuwa wakitumia usafiri wa gari la abiria lenye namba T.858 DAP kampuni ya Capricon inayofanya safari zake kutoka Arusha kwenda Mbeya.

Amewataja majina yao kuwa ni; Abdifatah Mohames (12), Ikran Mohames (17), Abdullah Mohamed (11), Farhiya Fahar (33), Abdlaziz Mohamed (13) na Mohamed Mohamed (23) wote raia wa nchi ya Kenya ambao walikuwa na hati za kusafiria za Kenya, “zilitiliwa mashaka na kubainika kuwa waliiingia nchini kinyume cha sheria.”

Amesema wahamiaji hao watafikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika.
 
Kwanini tu wasiwaache waende zao maana hao ni wapitaji tu

Kwa sisi wazurulaji wa kwenye mataifa ya watu mbona huwa tunaachwa tu tukikamatwa tunatoa posho kidogo then tunasepa


Yanini Tanzania kukamata watu ambao ni wapitaji tu

Sent using

Nene mwenekele
 
Mkenya kupita kwenda zambia ni muhamiaji haramu? Huyo kamanda ajitathmini


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hawa wahamiaji wapo wengi sanaa nchi hiii leo nimekutana na mkongo kabisa kwa 100% akijaribu kujipatia kitambulisho cha mpiga kura wale wamama wasimamizi kama walimshtukia niliacha wakimuhoji na alikuwa anajiuma uma tu mashuleni (private schools) wapo wengi tu
 
Sidhani kama ni sahihi kutangaza umekamata wakenya kwa sababu za ujirani na kidiplomasia....
kila siku viongozi wetu wakenya na tz wanasema sisi ni ndugu...
wawakamate kimya kimya na kuwarudisha makwao kimya kimya
 
Kwanini tu wasiwaache waende zao maana hao ni wapitaji tu

Kwa sisi wazurulaji wa kwenye mataifa ya watu mbona huwa tunaachwa tu tukikamatwa tunatoa posho kidogo then tunasepa


Yanini Tanzania kukamata watu ambao ni wapitaji tu

Sent using

Nene mwenekele
Alafu tunawaita wahamiaji haramu utafikili walikuwa na makazi hapo Dodoma na hawakufuata utalatibu
 
Viongozi wetu wanapenda sana kamera kwani illikuwa lazima awatangaze wahamiaji haramu....tumewahi kutoka Tarakea tukaenda Hadi Kajiado lakini ilikuwa ni kutembea tu na kurudi Tanzania,....tungekamatwa tungeitwa wahamiaji haramu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Parliament must earmark more funding to shore up border security. Illegal aliens from Kenya and Somalia are a burgeoning threat to the safety and welfare our communities.
 
Msafiri kafiri,Mpaka wakiingia south cha moto watakuwa wamekiona.
 
Back
Top Bottom