vamda
JF-Expert Member
- Aug 1, 2012
- 865
- 535
Salamu wana jamvi. Bila ya kupepesa macho, naenda moja kwa moja kwenye mada.
Leo tarehe 5- 10- 2020 watanzania tumeshuhudia ajali mbaya ya daladala na lori la mizigo. Abiria wa daladala takriban wanne wamefariki papo hapo na wengine lukuki kujeruhiwa vibaya (mahututi).
Kwanza naomba kuuliza jeshi la polisi, ni sheria ipi inayoruhusu abiria kusimama kwa kurundikana na kusongamana kwenye mabasi ya abiria maarufu kama daladala?
Naamini endapo abiria wa daladala iliyopata ajali, wangeketi kwenye viti bila ya kusimama huenda vifo visingetokea au madhara yasingekua makubwa kama ilivyotangazwa.
Waliotengeneza magari wameweka kiwango cha mwisho cha idadi ya abiria wanaotakiwa kuwemo ndani ya magari hayo. Askari wa usalama barabarani hamuwezi kukwepa lawama hii kutokana na uzembe wa kushindwa kusimamia sheria za usalama wa abiria. Au mnataka tuamini kwamba mna maslahi bibafsi kwenye biashara hiyo maana hata nauli zilizopangwa na sumatra (LATRA) zinazingatia abiria kuketi bila ya kusimama.
Ajali nyingi hutokana na askari wa barabarani kutochukua hatua stahiki za kisheria. Tunashuhudia, mbali na mabasi kurundika na kusimamisha abiria lukuki pia malori mengine hujaza mizigo zaidi ya uwezo wake. Vilevile magari mengi barabarani ni mabovu hususani daladala. Juzi nilipanda daladala viti vibovu, shokapu (shock absorber) hazifanyi kazi, dashboard haioneshi alama zozote, taa iliyowaka ilikuwa moja tu n. K. Nilishangaa daladala hilo lilikuwa na stika ya nenda kwa usalama (yaani limekaguliwa na polisi na kuruhusiwa kuendelea kubeba abiria).
Watanzania nani aliyetuloga? Nchi jirani zinatucheka kwa kutokuwa makini katika utendaji. Kwa vifo na majeruhi vilivyotokana na ajali hii ya daladala TEMEKE, polisi kitengo cha usalama barabarani watoe maelezo kwa nini wanaruhusu wafanyakazi wa kwenye madaladala kuwarundika abiria kwa kuwasimamisha. Polisi wawajibike kwa ajali hii. Naamini mtanishukuru kwa kuwaambia ukweli.