Polisi wawajibike ajali ya daladala Temeke

Mwenyezi Mungu tunamsingizia mengi. Yeye anatuangalia na kutuhurumia maana hatujui tutendalo
 
Sijajua Hilo daladala lilikuaje Ila kwa muda uliosemwa mara nyingi ni zile daladala zinazokuwa gereji kwa matengenezo mafundi wanaziiba zinapiga kazi usiku kucha alfajiri zinarudishwa gereji, Ile kauli ya usinifundishe kazi huende ni kujitetea siajabu gari lilikuwa na mapungufu mengi tu.
 
Wewe ulieandka Uzi huu,inaonekana waz hujui inshu za usafir wa daladala dar,wew unakiusafir chako,hujui ambavyo watu huteseka
 
Kwa nini waseme dereva wa daladala ndo mwenye makosa bila kumwajibisha dereva wa lori kwa kushindwa kuendesha kwa kujihami kwenye junction. Inakuwaje huyo dereva wa lori ajiachie kisa taa nyekundu imemruhusu bila kuchukua tahadhari yoyote?
Wa lorry hapo anakosa gani na taa zimemruhusu? Au ulitaka asimame ghafla?
 
Ila hawa madereva wa daladala akili zao wanazijua wenyewe, kuna mmoja aliiba route Barabara ya huko haijui vizuri, kurudi anawahi asikutane na traffic abiria tukamwambia apunguze mwendo alitujibu "nimeshindwa kupunguza mwendo" kumbe kweli kashindwa, kilichofuata ni kutubwaga mtaroni, hii ndio ajali mbaya Kati ya ajali nilizozipata nilipoteza fahamu, Hindu Mandali walinikataa wakashuri nipelekwe Muhimbili, nikipanda daladala kwa kweli huwa nasali kabisa, maana sijui dereva atakuwaje.
 
Huyu anaandika huu uzi unakaa mkoa gani?, Kwa Dar hakuna daladala za kutosheleza watu kama zitabeba level siti, pia hii ajali imetokea saa 9.50 alfajiri, kwa muda huu traffic gani atakua barabarani muda huo?
Kipindi cha corona watu walikua wanakaa level seat na hawabaki vituoni na wanawahi kufika mapema, na kuhusu muda wa alfajiri, jeshi la polisi linafanya kazi kwa Massa yote 24 , tupo pamoja?
 
Hii ni Afrika mkuu...kero kama hizi huwezi zikosa afrika.ukikosa kwenye daldala utakuta hospital.makanisani.shulen.masokon kero kila kona sabab ya chumi zetu hazija tengamaa..cha muhimu ni wew abiria kuchanganya na zako sabab wew ndio mpandaj wa daaldala...ukiona limejaa shuka
Kumbe wapo sahihi wanaosema: NO HURRY IN AFRICA
 
Mimi ndiyo maana huwa napenda kumu observes dereva uendeshaji wake mwanzoni tu mwa Safari iwe fupi au ndefu!

Nikimuona anaonesha dalili za uvunjifu wa sheria naanza kumuonnya sisubiri askari wa usalama barabarani wala Sumatra, yarabi nafsi yangu!
Unapoona tatizo chukua hatua. Usisubiri kesho. Kama nilivyofanya mimi, nimechukua hatua ya kukemea uzembe wa jeshi la polisi kwa kufumbia macho makosa ya barabarani
 
Chanzo cha ajali kimeelezwa kuwa ni dereva wa basi kupita kwenye mataa zikiwa nyekundu!

Inasikitisha sana, kwanini amewaua wenzake?

Lakini ni wazi kuwa sababu nyingine ni kwenda mwendo kasi!

Abiria jitambueni jamani

Kwanini ukubali mhuni aangamize maisha yako?

Kwanini mhuni ahatarishe maisha yako?

Hapana aisee!
Tuungane pamoja kukemea uzembe wa kimakusudi
 
Huyu anaandika huu uzi unakaa mkoa gani?, Kwa Dar hakuna daladala za kutosheleza watu kama zitabeba level siti, pia hii ajali imetokea saa 9.50 alfajiri, kwa muda huu traffic gani atakua barabarani muda huo?
Mbona nchi jirani wameweza level seat. Sisi tuna mapungufu gani hadi tushindwe
 
Huyu anaandika huu uzi unakaa mkoa gani?, Kwa Dar hakuna daladala za kutosheleza watu kama zitabeba level siti, pia hii ajali imetokea saa 9.50 alfajiri, kwa muda huu traffic gani atakua barabarani muda huo?
Sio ajali zote za kizembe hutokea saa 9 alfajiri
 
Salamu wana jamvi. Bila ya kupepesa macho, naenda moja kwa moja kwenye mada.

Leo tarehe 5- 10- 2020 watanzania tumeshuhudia ajali mbaya ya daladala na lori la mizigo. Abiria wa daladala takriban wanne wamefariki papo hapo na wengine lukuki kujeruhiwa vibaya (mahututi).

Kwanza naomba kuuliza jeshi la polisi, ni sheria ipi inayoruhusu abiria kusimama kwa kurundikana na kusongamana kwenye mabasi ya abiria maarufu kama daladala?

Naamini endapo abiria wa daladala iliyopata ajali, wangeketi kwenye viti bila ya kusimama huenda vifo visingetokea au madhara yasingekua makubwa kama ilivyotangazwa.

Waliotengeneza magari wameweka kiwango cha mwisho cha idadi ya abiria wanaotakiwa kuwemo ndani ya magari hayo. Askari wa usalama barabarani hamuwezi kukwepa lawama hii kutokana na uzembe wa kushindwa kusimamia sheria za usalama wa abiria. Au mnataka tuamini kwamba mna maslahi bibafsi kwenye biashara hiyo maana hata nauli zilizopangwa na sumatra (LATRA) zinazingatia abiria kuketi bila ya kusimama.

Ajali nyingi hutokana na askari wa barabarani kutochukua hatua stahiki za kisheria. Tunashuhudia, mbali na mabasi kurundika na kusimamisha abiria lukuki pia malori mengine hujaza mizigo zaidi ya uwezo wake. Vilevile magari mengi barabarani ni mabovu hususani daladala. Juzi nilipanda daladala viti vibovu, shokapu (shock absorber) hazifanyi kazi, dashboard haioneshi alama zozote, taa iliyowaka ilikuwa moja tu n. K. Nilishangaa daladala hilo lilikuwa na stika ya nenda kwa usalama (yaani limekaguliwa na polisi na kuruhusiwa kuendelea kubeba abiria).

Watanzania nani aliyetuloga? Nchi jirani zinatucheka kwa kutokuwa makini katika utendaji. Kwa vifo na majeruhi vilivyotokana na ajali hii ya daladala TEMEKE, polisi kitengo cha usalama barabarani watoe maelezo kwa nini wanaruhusu wafanyakazi wa kwenye madaladala kuwarundika abiria kwa kuwasimamisha. Polisi wawajibike kwa ajali hii. Naamini mtanishukuru kwa kuwaambia ukweli.
 
Kurundukwa kama magunia kwenye mabasi ni ushenzi wa kiwango cha juu. Tutastaarabika lini. Tuache mazoea. Zamani watu walipiga mswaki kwa kutumia miti, je unapenda tuendelee na mazoea hayo ya zamani? Tuchukue hatua. Saa ya ukombozi ni sasa
Mwendokasi Ni kisasa zaidi lakini Ni maalumu kwa abiria kusimama kukaa Ni maalumu kwa wazee,walemavu na wajawazito siti kwenye haya mabasi Ni chache tu na nafasi iliyobaki Ni kubwa Sana kwaajili ya kusimamisha watu wengi zaidi na hii si kwa Tanzania au Afrika tu mpaka kwa wenzetu haya Mambo yapo
Hei
 
Huyu anaandika huu uzi unakaa mkoa gani?, Kwa Dar hakuna daladala za kutosheleza watu kama zitabeba level siti, pia hii ajali imetokea saa 9.50 alfajiri, kwa muda huu traffic gani atakua barabarani muda huo?
mbona Kenya na Zanzibar wameweza level seat ? Hata Dar inawezekana ,mbona mchana daladala watu hawasimami ?ni kujiendekeza tu
 
Nye watu mnaosema level seat haiwezekani kwa dar hamjielewi ,mbona wakati wa corona mliweza
 
Salamu wana jamvi. Bila ya kupepesa macho, naenda moja kwa moja kwenye mada.

Leo tarehe 5- 10- 2020 watanzania tumeshuhudia ajali mbaya ya daladala na lori la mizigo. Abiria wa daladala takriban wanne wamefariki papo hapo na wengine lukuki kujeruhiwa vibaya (mahututi).

Kwanza naomba kuuliza jeshi la polisi, ni sheria ipi inayoruhusu abiria kusimama kwa kurundikana na kusongamana kwenye mabasi ya abiria maarufu kama daladala?

Naamini endapo abiria wa daladala iliyopata ajali, wangeketi kwenye viti bila ya kusimama huenda vifo visingetokea au madhara yasingekua makubwa kama ilivyotangazwa.

Waliotengeneza magari wameweka kiwango cha mwisho cha idadi ya abiria wanaotakiwa kuwemo ndani ya magari hayo. Askari wa usalama barabarani hamuwezi kukwepa lawama hii kutokana na uzembe wa kushindwa kusimamia sheria za usalama wa abiria. Au mnataka tuamini kwamba mna maslahi bibafsi kwenye biashara hiyo maana hata nauli zilizopangwa na sumatra (LATRA) zinazingatia abiria kuketi bila ya kusimama.

Ajali nyingi hutokana na askari wa barabarani kutochukua hatua stahiki za kisheria. Tunashuhudia, mbali na mabasi kurundika na kusimamisha abiria lukuki pia malori mengine hujaza mizigo zaidi ya uwezo wake. Vilevile magari mengi barabarani ni mabovu hususani daladala. Juzi nilipanda daladala viti vibovu, shokapu (shock absorber) hazifanyi kazi, dashboard haioneshi alama zozote, taa iliyowaka ilikuwa moja tu n. K. Nilishangaa daladala hilo lilikuwa na stika ya nenda kwa usalama (yaani limekaguliwa na polisi na kuruhusiwa kuendelea kubeba abiria).

Watanzania nani aliyetuloga? Nchi jirani zinatucheka kwa kutokuwa makini katika utendaji. Kwa vifo na majeruhi vilivyotokana na ajali hii ya daladala TEMEKE, polisi kitengo cha usalama barabarani watoe maelezo kwa nini wanaruhusu wafanyakazi wa kwenye madaladala kuwarundika abiria kwa kuwasimamisha. Polisi wawajibike kwa ajali hii. Naamini mtanishukuru kwa kuwaambia ukweli.
Issue ya abiria kusimama hiyo sisi wenyewe tunaiendekeza,utakuta Gari limejaa abiria bado wanataka kujazana na yote hiyo kila mtu anataka kuwahi na ufinyu wa magari

Ova
 
Back
Top Bottom