Polisi wawajibike ajali ya daladala Temeke

Polisi wawajibike ajali ya daladala Temeke

Kupata leseni ni kula kiapo kwa hiyo dereva ndiyo mwenye wajibu wa kwanza kwa abiria, watembea kwa miguu na watumiaji wengine wa barabara.
 
Mbona nchi jirani wameweza level seat. Sisi tuna mapungufu gani hadi tushindwe
Tatizo wenye hayo magari ndio maboss wenyewe wakifuata sheria wanaona watapata hasa
 
Habari mkuu.
Mimi napingana na wewe kwenye kipengele kimoja tu,nacho ni cha abiria kusumama ndani ya daladala...hii sio sababu ya ajali ingawa ajali inapotokea madhara huwa ni makubwa...lakini hata katika nchi za ulimwengu wa kwanza ikiwemo japan yanapotengenezwa kwa wingi abiria husimama kwenye commuter bus service zao,kikubwa nionacho mm ni kutungwa na kutekelezwa kwa sheria kali za usalama barabarani hasa kwa madereva wanaobeba abiria...

M/mungu aziweke roho za marehemu sehemu zinapostahili...tunawatakia pia majeruhi nafuu ya mapema...
 
Kwaio dereva amevuka wakati hajaruhusiwa wakulaumiwa ni Askari na kuruhusiwa watu kusimama? Mnakuwa mnatumia bongo lakini kufikiria mambo?

Suala la abiria kusimama, ni matakwa ya mtu mwenyewe tu, ata kama haijaruhusiwa, lakini abiria ataingia na kusimama. Zanzibar sheria inataka level seat, lakini utakuta watu wanasimama kwenye gari. Askari akitaka kukushtaki, unaanza kulalamika na kutaka kuyamaliza chini ya meza. Kwanza jilaumi wewe unaefanya kosa na kutaka yaishe chini ya meza kabla ya askari.
 
Mwendokasi Ni kisasa zaidi lakini Ni maalumu kwa abiria kusimama kukaa Ni maalumu kwa wazee,walemavu na wajawazito siti kwenye haya mabasi Ni chache tu na nafasi iliyobaki Ni kubwa Sana kwaajili ya kusimamisha watu wengi zaidi na hii si kwa Tanzania au Afrika tu mpaka kwa wenzetu haya Mambo yapo
Hei
Mabasi ya mwendokasi yana idadi maalum ya abiria kusimamia. Ndio maana kuna vishikio vya mikono ambavyo vina idadi maalum. Pia mabasi hayo yana njia yake maalum
 
Habari mkuu.
Mimi napingana na wewe kwenye kipengele kimoja tu,nacho ni cha abiria kusumama ndani ya daladala...hii sio sababu ya ajali ingawa ajali inapotokea madhara huwa ni makubwa...lakini hata katika nchi za ulimwengu wa kwanza ikiwemo japan yanapotengenezwa kwa wingi abiria husimama kwenye commuter bus service zao,kikubwa nionacho mm ni kutungwa na kutekelezwa kwa sheria kali za usalama barabarani hasa kwa madereva wanaobeba abiria...

M/mungu aziweke roho za marehemu sehemu zinapostahili...tunawatakia pia majeruhi nafuu ya mapema...
Huko Japan ulikotolea mfano kama ni kweli je wanasimama kwa kurundikana na kubanana kama magunia ya viazi? Tuambie ni eneo gani la Japan umeona hayo
 
Huyu anaandika huu uzi unakaa mkoa gani?, Kwa Dar hakuna daladala za kutosheleza watu kama zitabeba level siti, pia hii ajali imetokea saa 9.50 alfajiri, kwa muda huu traffic gani atakua barabarani muda huo?
Hapo lazma SUMATRA na TARURA wabaduri sheria zao juu ya urefu wa gari ili ziruhusu articulated bus kuingizwa nchini kwaajir ya kupunguza hio adha kwa maeneo yenye abiria wengi
 
vamda tokea Wazazi wako Wawili wakulete hapa 'Shidani' Ulimwenguni, katika Kumbukumbu zako kuna Siku Polisi wamekubali Makosa yao Kwetu?
 
Mabasi ya mwendokasi yana idadi maalum ya abiria kusimamia. Ndio maana kuna vishikio vya mikono ambavyo vina idadi maalum. Pia mabasi hayo yana njia yake maalum
So huwa Wanahesabu abiria wakienea kwenye vishikio Basi au sio?
Hei
Kutumia barabara peke yao sio sababu na mwendokasi sometime huwa zinajaza hata pakuhemea shida daladala pia Ni salama sana ajali ya juzi Ni ajali tu Kama nyingine zote ni chombo Cha Moto kimepata ajali uzembe tu wa dereva Haina uhusiano na wingi wa abiria
 
Foleni zinasaidia sana kuepusha ajali maeneo ya mijini.

Yani barabara zikiimarishwa na foleni kuondolewa Basi itabidi kuwepo na mbadala wa kudhibiti mwendokasi wa madereva nchini!

Madereva wa bongo wanaendesha magari vibaya sana!

Wengi hawafuati sheria za usalama barabarani na Ndiyo maana huwa askari usalama barabarani kama ni wasumbufu.

Tatizo linaanzia kwenye kujifunza kuendesha gari, Mwalimu anaemfundisha mtu gari ndiye anaeweza kumtengeneza dereva mzuri au mbaya.

Serikali inapaswa kuchukua jukumu la kufundisha madereva wapya ili kuwepo na muongozo wa kufafana na msisitizo wa utii wa sheria bila shuruti.
 
Salamu wana jamvi. Bila ya kupepesa macho, naenda moja kwa moja kwenye mada.

Mnamo tarehe 5- 10- 2020, siku ya jumatatu, watanzania tumeshuhudia ajali mbaya ya daladala na lori la mizigo. Abiria wa daladala takriban wanne wamefariki papo hapo na wengine lukuki kujeruhiwa vibaya (mahututi).

Kwanza naomba kuuliza jeshi la polisi, ni sheria ipi inayoruhusu abiria kusimama kwa kurundikana na kusongamana kwenye mabasi ya abiria maarufu kama daladala?

Naamini endapo abiria wa daladala iliyopata ajali, wangeketi kwenye viti bila ya kusimama huenda vifo visingetokea au madhara yasingekua makubwa kama ilivyotangazwa.

Waliotengeneza magari wameweka kiwango cha mwisho cha idadi ya abiria wanaotakiwa kuwemo ndani ya magari hayo. Askari wa usalama barabarani hamuwezi kukwepa lawama hii kutokana na uzembe wa kushindwa kusimamia sheria za usalama wa abiria. Au mnataka tuamini kwamba mna maslahi bibafsi kwenye biashara hiyo maana hata nauli zilizopangwa na sumatra (LATRA) zinazingatia abiria kuketi bila ya kusimama.

Ajali nyingi hutokana na askari wa barabarani kutochukua hatua stahiki za kisheria. Tunashuhudia, mbali na mabasi kurundika na kusimamisha abiria lukuki pia malori mengine hujaza mizigo zaidi ya uwezo wake. Vilevile magari mengi barabarani ni mabovu hususani daladala. Juzi nilipanda daladala viti vibovu, shokapu (shock absorber) hazifanyi kazi, dashboard haioneshi alama zozote, taa iliyowaka ilikuwa moja tu n. K. Nilishangaa daladala hilo lilikuwa na stika ya nenda kwa usalama (yaani limekaguliwa na polisi na kuruhusiwa kuendelea kubeba abiria).

Watanzania nani aliyetuloga? Nchi jirani zinatucheka kwa kutokuwa makini katika utendaji. Kwa vifo na majeruhi vilivyotokana na ajali hii ya daladala TEMEKE, polisi kitengo cha usalama barabarani watoe maelezo kwa nini wanaruhusu wafanyakazi wa kwenye madaladala kuwarundika abiria kwa kuwasimamisha. Polisi wawajibike kwa ajali hii. Naamini mtanishukuru kwa kuwaambia ukweli.
 
Hadi ulaya wanasimama,na usichokkijua kuwa gari ina tani kadhaa ya kubeba,mnaweza kusimama lkn bado msifikie ile tani
 
huu uzi wako na kilichotokea wala haviendani, ulitakiwa uanzishe uzi unaohusiana na hicho unacholalamikia lakini sio kuunga kwenye ajali ya temeke. Kwenye ile ajali hakuna kosa la polisi, kosa ni la dereva kupita kwenye taa nyekundu na hata alipoonywa na abiria hakusikia, hivyo aliwaua kwa makusudi kabisa. Na hiyo daladala kwa muda huo wala haikuwa imejaza, wala abiria hawakusimama na kama kuna waliosimama basi hawakuzidi hata 5 na ni muda ambao hata askari wa barabarani hawakuwepo na hata wangekuwepo sio kazi yao kukufatilia usimame kwenye taa nyekundu ni kitu ambacho ni wajibu wako wewe dereva
 
Hata huko mbelez wanasimama kwenye usafiri wa umma, sio bongo tu!!
 
Huyu anaandika huu uzi unakaa mkoa gani?, Kwa Dar hakuna daladala za kutosheleza watu kama zitabeba level siti, pia hii ajali imetokea saa 9.50 alfajiri, kwa muda huu traffic gani atakua barabarani muda huo?
Asante mkuu

Pia nampa ukweli ile daladala ina bebe qatu zaidi ya 28...lakini wakati inapata ajali haikua hata na watu wanao fika 15..

Aliye kwambia ilijaza na kupitiliza sijui ni nani
 
Kipindi cha corona watu walikua wanakaa level seat na hawabaki vituoni na wanawahi kufika mapema, na kuhusu muda wa alfajiri, jeshi la polisi linafanya kazi kwa Massa yote 24 , tupo pamoja?
Kama linafanya kazi mida wote mbona hao Police traffic huwa hawaonekani barabarani usiku wa manane?
 
Kama sheria ipo hivyo waambie waanze na mabasi ya mwendokasi kwanza.
 
Back
Top Bottom