Polisi wawajibike ajali ya daladala Temeke

Polisi wawajibike ajali ya daladala Temeke

Kwanza naomba kuuliza jeshi la polisi, ni sheria ipi inayoruhusu abiria kusimama kwa kurundikana na kusongamana kwenye mabasi ya abiria maarufu kama daladala?
Sheria kawaulize LATRA kwani wao ndio wanaotunga sheria kuhusiana na usafiri wa nchi kavu, polisi wao ni wasimamizi wa hizo sheria kuhakikisha kuwa zinafuatwa tu.

Naamini endapo abiria wa daladala iliyopata ajali, wangeketi kwenye viti bila ya kusimama huenda vifo visingetokea au madhara yasingekua makubwa kama ilivyotangazwa.
Hivi nani aliekwambia kuwa abiria kuketi kwenye gari (level seat) ndio hakupelekei ajali au ajali ikitokea ndio watu hawafariki kwa vile wameketi nani? Hujakutana na ajali, ambapo abiria wameketi lakini wote wamefariki? Hebu kaa chini ufikirie upya sio unaandika kama ubongo wako umefanyiwa factory reset.

Askari wa usalama barabarani hamuwezi kukwepa lawama hii kutokana na uzembe wa kushindwa kusimamia sheria za usalama wa abiria.
Muda mwingine fichaga upumbavu mkuu, kwa ajali kama ile utawalaumu vipi askari wa usalama barabarani wakati kwa muda huo hawakuwepo eneo hilo kwa vile barabara zilizo katika maungano zinaendeshwa na traffic light?
Usiwe mwepesi wa kuongea. Nyie ndio wepesi wa kuongea negativity pale askari wa usalama barabarani anapolikamata gari na kuwaona kuwa wanawaonea madereva.
Dereva akipigwa faini kutokana na mapungufu ama kosa mnawaponda sana hao askari na kuwaita kwa majina mnayoyajua nyie na kuwaona kama wako pale kazi yao ni kucheza singeli.

Polisi wawajibike kwa ajali hii. Naamini mtanishukuru kwa kuwaambia ukweli.
Hakuna kipengele wala kifungu kinachowawajibisha polisi. Kama huelewi majukumu yao ni bora ungeuliza,
Kazi zao ni kukagua magari na kuona pale kwenye upungufu ama kasoro huwataka madereva wazirekebishe. Lakini wewe ulieandika hii mada sijui unaishi mkoa gari maana kwenye mada yako umeandika uharo mtupu.
Kwa wanaoijua route hiyo, haina abiria wengi sana, hasa kwa muda wa usiku na pia chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa dereva wa daladala na kutaka kukatisha kwenye mataa, sasa ninachokushangaa badala ya kuwataka madereva wa daladala kufuata sheria za usalama barabarani, pamoja na matumizi ya alama kwa usahihi wewe umekuja na kuanza kuwalaumu askari wa usalama barabarani, kitu ambacho kwa jinsi eneo ajali ilipotokea na kwa muda huo pia sio sahihi. Kosoa pale kosa husika lilipo na pia unatakiwa uelewe magari mengi katika mji wa Dar es salaam wakati wa usiku huingizwa barabarani yakitokea gereji.
 
Ok, kumbe ulimaanisha 2000 ya kubrash viatu? Trafiki gani anapokea 2000? Huyo ni popoma.
Wanapokea efu 2000 wewe ebu zidisha efu 2000 mara 40 kwa siku afu uje tena uzidishe mara 30 uone utapata ngapi kwa mwezi....
Wale majamaa wanaishi vizuri mjini hapa usione wanapigwa jua

Sent from my TA-1004 using JamiiForums mobile app
 
Wanawapa kwa kupenda, laiti kama wangetimiza wajibu sidhani kama wangekuwa wanatoa hizo elf 2 mbili zao.
 
Wanaowapa wanawapa kwa kupenda, laiti kama wangetimiza wajibu sidhani kama wangekuwa wanatoa hizo elf 2 mbili zao.
Ndio wanatoa kwa sababu nyingi kubwa hesabu isiharibike mana akiandika pale balaa cha ajabu mambo yanfanyika waziwazi kila mtu anaona utasema imepitishwa vile..

Dereva anasema kabisa konda nigee 2000 kila mtu anasikia ha ha ha

Sent from my TA-1004 using JamiiForums mobile app
 
Ndio wanatoa kwa sababu nyingi kubwa hesabu isiharibike mana akiandika pale balaa cha ajabu mambo yanfanyika waziwazi kila mtu anaona utasema imepitishwa vile..

Dereva anasema kabisa konda nigee 2000 kila mtu anasikia ha ha ha

Sent from my TA-1004 using JamiiForums mobile app
Kiufupi ni kwamba hao madereva wa magari kwanza kabisa magari yao yana kasoro nyingi ili kuficha hizo kasoro ndio inawabidi kutoa hizo 2000.
Pili hata ninyi mnaokuwemo kwenye gari mnakuwa na makosa, kwanini mnaona rushwa inafanyika wazi wazi kisha mnaangalia tu? Then gari hilo hilo likitembea na kupata ajali mtamlaumu askari trafiki aliyechukua 2000 au dereva aliyetoa 2000?
 
Watu hawaezi sema sababu 90% sisi wote sio waaminifu sehemu zetu za kazi ndio mana unaona mambo yanaendelea tu kwann umchome traffick wakati na wewe kazini kwako kuna yako unafanya yasiyo halali nafsi lazma ikusute

Sent from my TA-1004 using JamiiForums mobile app
 
Ndio wanatoa kwa sababu nyingi kubwa hesabu isiharibike mana akiandika pale balaa cha ajabu mambo yanfanyika waziwazi kila mtu anaona utasema imepitishwa vile..

Dereva anasema kabisa konda nigee 2000 kila mtu anasikia ha ha ha

Sent from my TA-1004 using JamiiForums mobile app
Duuh. Hiyo ni noma. Wa kulaumiwa ni viongozi waliopewa dhamana
 
Back
Top Bottom