Polisi wawaita kituoni wananchi walioibiwa masufuria ya 'ubwabwa'

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Wananchi mkoani Njombe wameshauriwa kufika na kutambua mali zilizokamatwa wakati wa doria kutokana na kuibwa nyakati za usiku yakiwemo magodoro, pikipiki, sufuria zinazotumiwa na mama lishe migahawani, mitungi ya gesi, jiko na vingine vingi.

Mali hizo nyingi zimekuwa zikiibwa wakati wa usiku, zimekusanywa na zipo kituoni kwa ajili ya kusubiri kutambuliwa lakini wananchi wamekuwa hawajitokezi. Vingine ni laptop, TV na redio.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamis Issah amesema kuna watu ambao huwa wanakata tamaa mapema kufuatilia mali walizopoteza wakisharipoti matukio Polisi, hivyo waende kwa kuwa kuna masufuria ambayo bado yana masalia ya chakula.

"Kuna watu wakisharipoti hawaji kituoni kufuatilia, kuna magodoro matano hapa, kuna mitungi ya gesi, kuna majiko, kuna masufuria tena mengina bado yana chakula hayajasafishika, kina mama mnaoibiwa mje mtambue masufuria yenu.

"Tunaomba wananchi wa Njombe mje mtambue vitu vyenu, kuna majiko hapa lakini wezi wameyaharibu," amesema Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamis Issah.

 
Mali hizo nyingi zimekuwa zikiibwa wakati wa usiku, zimekusanywa na zipo kituoni kwa ajili ya kusubiri kutambuliwa lakini wananchi wamekuwa hawajitokezi. Vingine ni laptop, TV na redio
Hao wanaokamatwa huwa hawana fedha mifukoni mwao? Nazo zingewekwa kwenye orodha
 
Duh aiseeemtu anaona bora asamehe kuliko kwenda kuchukua maki yake baada ya kuhojiwa kwa masaa tele
 
hata hivyo , wamelalamika kuwa ,kuwa upande wa chakula cha wali, umebaki ukoko
 
Walioibiwa hela mbona hamuweki hela?
Eti masufuria yenye wali khaaa
Yangekuwa magodoro mapya wangejigawia
 
Back
Top Bottom