VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Katika hali isiyo ya kawaida, Askari wa Polisi wa Doria wa Wilaya ya Kibaha walivamia, kukamata, kupiga na kupora watu pesa zao.Tukio hilo limetokea katika Mtaa wa Visiga-Madafu Kibaha, Pwani majira ya saa tatu usiku karibu na Baa moja iliyopo sehemu hiyo.Watu wakiwa wanaendelea na harakati zao za kimaisha, ghafla liliingia gari la Polisi na kushusha askari sita. Askari hao,bila kuchelewa waliaanza kukamata watu ovyo kuwapiga na kuwasweka garini mwao.
Waliokamatwa walipigwa vibao na ngumi garini huku wakisachiwa pesa na kuchukuliwa zote walizokuwa nazo.Gari lilitembea kidogo kuelekea Mailimoja kisha kuwashusha watu hao wakiwa na maumiu ya mwili na ya kiuchumi. Askari hao waliahidi kurudi tena siku nyingine.Je,hii ni halali?
Chanzo: Mimi nilikuwepo hapo. Nilikamatwa lakini Askari wakanywea baada ya kuwaonesha kitambulisho wakaniachia haraka.