Polisi Waunda Tume ya kuchunguza kifo cha Daudi Mwangosi

Polisi Waunda Tume ya kuchunguza kifo cha Daudi Mwangosi

Hivi waziri Nchimbi anasubiri nini kujiuzuru? au anasubiri jamaa arudi msibani Ethiopia?

Mkuu Hana uzalendo huo Mkuu na sio viongozi wa tz hii mpaka alazimishwe siuliona maige mpaka akalia kujitetea cheo chake??
 
Hakuna haja ya kuunda tume polisi waliofanya kitendo cha mauaji wanaonekana kwenye picha kamata wafunguliwe mashtaka ya mauaji, halafu kamata wale wote walioradhimisha kufanya mkutano kwa nguvu nao peleka mahakamani fungulia mashtaka ya uvunjaji wa amani.

Point
Pointless
 
hili jeshi la ajabu sana. Iron boys hawa according to Aristotle
 
[TABLE="class: wsite-multicol-table"]
[TR="class: wsite-multicol-tr"]
[TD="class: wsite-multicol-col"]
1346667662.jpg
Daud Mwangosi
​

[/TD]
[TD="class: wsite-multicol-col"]
1346667711.jpg
Paul Chagonja
​

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Francis Dande, HabariMseto blog -- JESHI la Polisi nchini limeunda tume itakayochunguza kifo cha Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Channel TEN, Marehemu Daud Mwangosi kilichotokea mjini Iringa wakati Jeshi la Polisi likipambana na wafuasi wa Chadema waliokuwa katika ufunguzi wa tawi la chama hicho katika Kijiji cha Nyololo mjini Iringa.

Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Paul Chagonjauchunguzi huo utavishirikisha vyombo vya usalama kutoka Jeshi la Polisi pamoja na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) 'kuwa Jeshi la Polisi limeunda tume itakayowahusisha Maofisa kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ pamoja Mkurugenzi wa Makosi ya Jinai Robert Manumba, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema ili kubaini ukweli kuhusu kiliochosababisha kifo cha mwandishi huyo basi tusubiri matokeo ya uchunguzi huo' alisema Chagonja.

Marehemu Mwangosi amefariki dunia jana wakati baada ya kulipukiwa na kitu kinachachodaiwa kuwa ni bomu wakati chama cha Demokrasia na Maendelo (Chadema) kikifungua tawi la chama vchake katika Kijiji cha Nyololo mjini Iringa.

966099517.JPG


Source: Jeshi la Polisi launda Tume ya kuchunguza kifo cha Daudi Mwangosi - wavuti

Haya ni matumizi mabaya ya rasilimali kila siku mnaunda tume kujustify posho then wanacook report.kwenye hili kila kitu kipo open...i wonder chagonja kasha anza ngonjera ooh!marehemu alipigwa na kitu kizito...Mara senza anadai wamekata watu 32.haya maigizo kwenye issues ambazo watu wapo serious zinatia kichefu chefu.
 
Mwaka jana Mwenyekiti wa CCM Rungwe aliuwawa na "mahasimu " wake wa kisiasa.
Baadaye kidogo Prof Mwandosya akaugua.
Hatukukaa sawa Dr Mwakyembe akaugua lwa sumu isiyoeleweka.
Sakata la Dr Ulimboka bado hatujalisahsu.

Sasa Mwanfishi wa habari CH 10 Ndg Mwangosi ameuwawa.

Wandugu pamoja na UCCM wangu sasa nakosa amani
 
Mwaka jana Mwenyekiti wa CCM Rungwe aliuwawa na "mahasimu " wake wa kisiasa.
Baadaye kidogo Prof Mwandosya akaugua.
Hatukukaa sawa Dr Mwakyembe akaugua lwa sumu isiyoeleweka.
Sakata la Dr Ulimboka bado hatujalisahsu.

Sasa Mwanfishi wa habari CH 10 Ndg Mwangosi ameuwawa.

Wandugu pamoja na UCCM wangu sasa nakosa amani

EEh kweli BWANA haya yote majembe!. ....hivi haya mambo yamepangwa nini?. ....Ila tukubaliane magamba ni hatari!. Yote haya ni kujilinda ili maovu waliyoyafanya yasiwarudi!
 
Nakubaliana na wewe, wanasiasa wooote waliofanya mkutano kwa nguvu wapelekwe mahakamani, na hapa naamanisha wote including Dr Bilali aliyefanya mkutano mkubwa wa CCM huko Bububu jana 2nd Sept 2012.

hehe Mkuu umemmaliza kabisa Ritz na ukiendelea hivi lazima aseme ''PO''
 
Last edited by a moderator:
Asante bwana!!huu ndio ukomavu,penye ukweli tuondoe itikadi za kisiasa,kidini nk,vipi kuhusu uhusika wa chama chako kwenye scenario zote hizo?una wazo lolote,tunaomba maoni yako mkuu.
 
umesahau na morogoro mauaji nako chama chako kimetajwa,, !
 
Tume yoyote itakayokuwa na mjumbe kutoka jeshi la polisi haitaaminika hata kwa dawa.
Kinachotakiwa hapa ni iundwe tume huru kabisa, kwa mujibu wa sheria ya vifo vyenye utata ili iweze kutuletea matokeo ya ukweli. Hata kama serikali haitawawajibisha watakaobainika kumuua marehemu Mwangosi lakini wananchi watakuwa wameufahamu ukweli.
HIKI NACHO KINA UTATA?basi vichwa vyetu ndio vyenye utata.
 
Masopakyindi angaliu tu kukosa kwako imani usigeuke nyuma, utageuka nguzo ya chumvi!!!
 
Pole mdogo wangu masopakyindi ila uliyoyataja wazungu huyaita "just the tip of an iceberg". Nitakachokuomba ni kitu kimoja tu, zidi kufunguka macho uweze kuyaona yale ambayo wengine tunayaona na kuyashuhudia kila siku na kila saa...yanasikitisha, yanaudhi na yanakasirisha. Maswali utakayoamua kujiuliza hivi sasa kama tu ungethubutu kujiuliza awali hapo nyuma, labda mchango wako katika kurekebisha hali kama hiyo ingeweza kuleta tofauti. Kama ilivyokuwa kwa Farao wa Misri, ilibidi ampoteze mtoto wake mpendwa ndipo fahamu za kujiuliza maswali magumu zilipomjia. Ni kweli finally alisalimu amri but at what cost!

Sina hakika una umri gani lakini Marehemu Daud Mwangosi angeweza kuwa mwanao au mdogo wako...sasa shuhudia wauaji wake wanavyoendelea kutamba. Kwa nini wanatamba? Kwa sababu wengine tulipopaza sauti zetu, ndugu zetu mliziba masikio, tulipolalamika hamkutuunga mkono, tulipotoa tahadhari mlitucheka...Kiburi cha Kikwete, kiburi cha CCM, kiburi cha Said Mwema na kiburi cha Kamuhanda kinatokana na waliokaa kimya kama wewe. Kwa mauaji yaliyofanyika hadi leo na kwa shida na taabu zinazotukabili, wewe masopakyindi ni mshiriki na huwezi kukwepa lawama.
 
Last edited by a moderator:
Natoa rai kwa IGP na uongozi wa juu serikalini; kama kweli suala la Mwangosi lime wagusa nadhani kabla ya yote ili angalau kurudisha imani kwa wananchi muwekeni pembeni RPC huyu na kuwachukulia hatua za kisheria make sheria za jeshi zipo askari wote walio husika kumuua Mwangosi. Picha za video ni ushahidi tosha, masuala ya uchunguzi hayana maana make ushahidi upo. Labda tu kama mnataka kufanya uchunguzi kubaini kama askari wale akiwemo RPC wao wana akili timamu.
 
Labda tu kama mnataka kufanya uchunguzi kubaini kama askari wale akiwemo RPC wao wana akili timamu.

Hili nalo la msingi sana kufanyika kwa polisi wote waliopo kazini na wale wanaotaka kujiunga na jeshi la polisi
 
Polisi wa Tanzania, wakisikia tu neno Chadema wanapatwa na hofu kuu.
Moja kwa moja huingiliwa na wehu, huanza kuongea uongo, kuleta porojo, kutishia, kupiga kuua na kutesa.
Hivi hawa wenzetu wanatishwa nini haswa na CHADEMA, mwenye jibu anisaidie tafadhali.
 
Uko sahihi lakini hilo lingewezekana tungekuwa na serikali serious. Kwa hawa wasanii watatafuta kila namna kufunika na kulindana tena hata kupongezana kwa unyama wanaofanya
 
Labda utokee muujiza,hawezi kuwekwa kando ilhali ametekeleza alichotumwa na wakubwa wake!
 
Back
Top Bottom