Polisi Waunda Tume ya kuchunguza kifo cha Daudi Mwangosi

Jamani sisi wengine ni majirani na hapo Nyololo ambapo limetokea tukio la kusikitisha - kuua mtanzania - mlipakodi wa nchi hii - hakuna kambiya jeshi pale kwamba kuna bomu labda liliangushwa au kupotea - hakuna vita vya ndani kana kwamba kuna mabomu ya kutegwa yaliwekwa.

Polisi ndio walikuja na mabomu - jibu liko wazi. Tume ya nini jibu liko wazi - waliokuja na mabomu ni polisi na Marehemu Mwangosi ameaua na kitu kinachosadikiwa ni bomu.

Hasira inanipanda zaidi inaposikia haoa hao tena wameunda tume - sasa ya kumchunguza nani??. Aliyewaleta polisi pale au......???
 
Mambo mengine Tanzania yanatia kinyaa kweli kweli. Hivi kwa nini wananchi tusijilinde wenyewe dhidi ya Polisi? Polisi hawalindi wananchi bali wanaua wananchi.
 
Hili Jeshi letu la polisi utafikiri la KUKODIWA - kumbe ni jeshi ambalo linatokana na familia zetu sisi wenyewe
 
Kuna kibwagizo kimoja chanchi inayopenda tume.
Raisi aliulizwa, "mheshimiwa inasemekana serikali yako inapenda sana kuunda tume hata kwa mambo yasiyo na sababu".
Raisi: "Nani amekwambia habari hizi? Tutaunda tume kuchunguza kama zina ukweli"

Ninavyoona Tanzania tunatumia vibaya uwepo wa uundaji wa tume. Kila kitu tume! Kha!
 
Hakuna haja ya kuunda tume polisi waliofanya kitendo cha mauaji wanaonekana kwenye picha kamata wafunguliwe mashtaka ya mauaji, halafu kamata wale wote walioradhimisha kufanya mkutano kwa nguvu nao peleka mahakamani fungulia mashtaka ya uvunjaji wa amani.

Leo umetumia akili yako kuchangia, hongera bro polepole utaujua ukweli.
 
Hakuna sababu ya kuwa na tume ya uchunguzi inayoundwa na majeshi pekee. Kama ni hivyo nawaomba waandishi wa habari kuunda tume ya uchunguzi hata kwa kuomba msaada wa ulinzi toka nje ya nchi. Ni vigumu kupata ukweli kutoka kwa tume hiyo ya polisi iwapo jeshi la polisi lilitangaza uongo kuhusu chanzo cha mauaji ya mwana habari huyo. Waandishi wa habari kwa taaluma yenu na ushahidi wa picha ambao nyinyi mnao bila polisi kuwa nazo nina imani mtaleta taarifa bora kuliko tume hiyo iliyoundwa na polisi. Polisi wa tanzania acheni kuuwa kwani nanyi lazima siku moja mtakufa.Alikuwepo gaddafi, idd amini, bokassa,moutu, hitler na wengine sembuse nyinyi?
 
Naipenda hii nchi.

Naomba aje rais dicteta atakaye wapiga risasi watu kama hawa
 
Ha! Ha! Ha! Ha! Ha! Ha! Ha! Ha! Sina mbavu mie!
Waunganishe tume hii na ile ya Dr. Ulimboka.
Ha! Ha! Ha! Ha! Ha! Ha! Ha! Ha! Sina mbavu mie!
mi mwenyewe nimeishia kucheka tu mpaka nikahisi nipo kwenye jukwaa la utani
 
Hii ndio Hasara ya kuwa na polisi walionunua Vyeti na pia Wavuta Bange!!
 
Inasikitisha sana,Daudi kama alikuwa baba sasa hivi watoto wake ni yatima tayari,huyu alietoa uhai wa daudi afanyejwe?tume zinaundwa kila kukicha na matokeo yake ni ya kiubabaishaji.familia yake na wote waliokuwa wanamtegemea leo waende kwa nani kupata msaada?tume haitasaidia chochote.
 
966099517.JPG

Hii picha ina majibu mengi sana;
Polisi wanaweza kutumia kila mbinu kujitetea lakini kwa hili wamecheza faulo mbaya...Jaribu kuiangalia kwa makini hii picha na kusoma kitendo cha kila askari. Utagundua kuwa wapo waliokuwa wanawazuia wenzao kuendeleza kipigo kwa mwandishi huyo(angalia movement za askari kanzu mwenye fulana ya bluu, pia kuna askari mwenye kofia nyekundu asiye na kikinga risasi, pia kuna askari upande wa pili mwenye kofia nyeusi)....
Hivyo huyo mwandishi alipigwa tena kipigo kibaya na ndio maana yupo chini akiwa hajiwezi.
Angalia pia mkono wa kulia wa huyo mwandishi, katika kiganja chake ameshika kamera, kwa hilo tu polisi walitakiwa watoe ulinzi maana kitendo cha kuwa na kifaa kama kamera ni ishara kuwa jamaa alikuwa ni mwanahabari naalikuwa katika harakati za kazi.
Halafu pia ukijaribu kuivuta picha kwa karibu utaona kuna kitu kama moshi kinafuka karibu kabisa na mwili wa marehemu na moshi huo unaelekea moja kwa moja katika mtutu ulioelekezwa kwake, moshi huo bilashaka ni matokeo ya bomu lililopigwa na huyo askari wa kushoto kabisa aliyeelekeza mtutu wake kwa marehemu.
huyo ndiyo rpc kamuhanda kwenye tukio
 
Hivi ni nani aliloga viongozi wa tanzania? mbona kama dhaifu saaana akilini mwao wanawaza mambo ya ajabu tu
 
Mimi nikitarajia kumsikia IGP akilitangazia Taifa kwamba RPC wa Iringa amesimamishwa kazi na Polisi waliohusika wamekamatwa kusubiri uchunguzi wa tukio la jana! Sina hakika kama tutamaliza salama kipindi kilichosalia ktk utawala huu.
 
Tume yoyote itakayokuwa na mjumbe kutoka jeshi la polisi haitaaminika hata kwa dawa.
Kinachotakiwa hapa ni iundwe tume huru kabisa, kwa mujibu wa sheria ya vifo vyenye utata ili iweze kutuletea matokeo ya ukweli. Hata kama serikali haitawawajibisha watakaobainika kumuua marehemu Mwangosi lakini wananchi watakuwa wameufahamu ukweli.

Uundaji wa tume ya kipolisi ni kinyume na Kanuni za Kisheria, Msemo wa kiLatini "Nemo iudex in causa sua" (Hakuna anayestahili kufanya uamuzi juu ya kosa alilolitenda mwenyewe). Rules of justice have to observed.
 
Mimi sio mtaalam wa mabomu ila najua mabomu ya machozi huwa hayalipuki, hata likitua mbele yako!

Sasa hiyo live bomu nani alikuwa amebeba?
 
Hakuna haja ya kuunda tume polisi waliofanya kitendo cha mauaji wanaonekana kwenye picha kamata wafunguliwe mashtaka ya mauaji, halafu kamata wale wote walioradhimisha kufanya mkutano kwa nguvu nao peleka mahakamani fungulia mashtaka ya uvunjaji wa amani.

Pamoja na mtazamo wako, sahihisho, hapakuwa na mkutano bali ufunguzi wa tawi. Ni kitu kidogo sana kulinganisha na kampen za uchaguzi
 
Watanzania hatuna imani na polisi magamba katika lolote lile. Ushahidi wa nani waliohusika na mauaji uko wazi kabisa hivyo hakuna sababu yoyote ya kupoteza muda na tume nyingine ya polisi magamba.
 
Back
Top Bottom