Polisi Waunda Tume ya kuchunguza kifo cha Daudi Mwangosi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi Waunda Tume ya kuchunguza kifo cha Daudi Mwangosi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiganyi, Sep 3, 2012.

 1. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: wsite-multicol-table"]
  [TR="class: wsite-multicol-tr"]
  [TD="class: wsite-multicol-col"]
  [​IMG] Daud Mwangosi

  [/TD]
  [TD="class: wsite-multicol-col"]
  [​IMG] Paul Chagonja

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Francis Dande, HabariMseto blog -- JESHI la Polisi nchini limeunda tume itakayochunguza kifo cha Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Channel TEN, Marehemu Daud Mwangosi kilichotokea mjini Iringa wakati Jeshi la Polisi likipambana na wafuasi wa Chadema waliokuwa katika ufunguzi wa tawi la chama hicho katika Kijiji cha Nyololo mjini Iringa.

  Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Paul Chagonjauchunguzi huo utavishirikisha vyombo vya usalama kutoka Jeshi la Polisi pamoja na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) 'kuwa Jeshi la Polisi limeunda tume itakayowahusisha Maofisa kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ pamoja Mkurugenzi wa Makosi ya Jinai Robert Manumba, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema ili kubaini ukweli kuhusu kiliochosababisha kifo cha mwandishi huyo basi tusubiri matokeo ya uchunguzi huo' alisema Chagonja.

  Marehemu Mwangosi amefariki dunia jana wakati baada ya kulipukiwa na kitu kinachachodaiwa kuwa ni bomu wakati chama cha Demokrasia na Maendelo (Chadema) kikifungua tawi la chama vchake katika Kijiji cha Nyololo mjini Iringa.

  [​IMG]


  Source: Jeshi la Polisi launda Tume ya kuchunguza kifo cha Daudi Mwangosi - wavuti
   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Tume ya nini wakati wanahabari wamemuonyesha muuaji ,picha zinajionyesha ,mahala walipomuulia panajulikana na aliyewatuma ni Jakaya Kikwete na shemeji yake IGP Saidi Mwema,mapepo na majini yao ni kwamba kable ya 2015 kwa kutumia polisi watakuwa wameua viongozi wote wa chadema na wananchi kama laki moja huo ndio ukweli manake dhamira yao inaonekana wazi sasa
   
 3. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Tume yoyote itakayokuwa na mjumbe kutoka jeshi la polisi haitaaminika hata kwa dawa.
  Kinachotakiwa hapa ni iundwe tume huru kabisa, kwa mujibu wa sheria ya vifo vyenye utata ili iweze kutuletea matokeo ya ukweli. Hata kama serikali haitawawajibisha watakaobainika kumuua marehemu Mwangosi lakini wananchi watakuwa wameufahamu ukweli.
   
 4. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Ha! Ha! Ha! Ha! Ha! Ha! Ha! Ha! Sina mbavu mie!
  Waunganishe tume hii na ile ya Dr. Ulimboka.
  Ha! Ha! Ha! Ha! Ha! Ha! Ha! Ha! Sina mbavu mie!
   
 5. papason

  papason JF-Expert Member

  #5
  Sep 3, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Hapo haki haiwezi kutendeka!
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  Sep 3, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hii taarifa ya polisi kuunda tume ya uchunguzi inaleta hasira sana. Extremely angry.
   
 7. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #7
  Sep 3, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Yaani unaua halafu unajiundia tume ujichunguze...hawa jamaa ni minduku kweli...
   
 8. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #8
  Sep 3, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Hakuna haja ya kuunda tume polisi waliofanya kitendo cha mauaji wanaonekana kwenye picha kamata wafunguliwe mashtaka ya mauaji, halafu kamata wale wote walioradhimisha kufanya mkutano kwa nguvu nao peleka mahakamani fungulia mashtaka ya uvunjaji wa amani.
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  Sep 3, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na wewe, wanasiasa wooote waliofanya mkutano kwa nguvu wapelekwe mahakamani, na hapa naamanisha wote including Dr Bilali aliyefanya mkutano mkubwa wa CCM huko Bububu jana 2nd Sept 2012.
   
 10. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #10
  Sep 3, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  ndo maana mimi nayaita haya ma ccm na liserikali lao ni MAONGO/MAJAMBAZI/MAFISADI/WAUAJI. wamejimilikisha hii nchi wakati walipigiwa kura na watu wasiozidi hata asilimia kumi. wanatoa wapi ujasiri wa kutunyanyasa sisi wengine ambao hata hatukuwachagua?? sisi hatuja mbugudhi mtu, tunafanya maandamano na mikutano yetu kwa mujibu wa sheria mama ya nchi i.e. katiba ya jamuhuri ya muungano. wao ccm majambazi wanajifanya wana haki miliki ya maisha yetu. ngoja siku ifike, hakyanani tutawachijia kwenye nyumba zao na watoto wao. HIVI WAO NI KINA NANI??? KURA ZENYEWE ZA KUCHAKACHUA HALAFU WAPO MSTARI WA MBELE KUUA WATU. HII NCHI NI YETU SOTE??? MBONA WENGINE WANAKESHA KWENYE FIESTA HUKU SENSA INAENDELEA, CHADEMA TUMEKOSEA NINI??? KAMA WANAZIJUA SHERIA KWA NINI WALIZIKIUKA WAKAIBA KURA??? KAMA WANAZIJUA SHERIA KWA NINI POLISI WENGI TU WANA VYETI VYA KUGHUSHI??? KAMA WANAZIJUA SHERIA MBONA WAMEFICHA MABILIONI USWIS NA WOTE WANAJIFANYA MABUBU??? HII NCHI NI YA WOTE NA LAZIMA KILA MTU APATE HAKI YAKE YA KUISHI BILA KUHOFIA CCM MAJAMBAZI/WAUAJI.
   
 11. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #11
  Sep 3, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Tumeona picha dhahiri polisi wanampiga tume ya nini sasa?....
   
 12. F

  Froida JF-Expert Member

  #12
  Sep 3, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Wasiwe wanasiasa wa Nyololo tuu wawepo pia wa bububu,Mwanza,Tanga,Temeke manake panga likate kote
   
 13. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #13
  Sep 3, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,936
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Tume ya nini wakati picha imekwishafanya kazi ya tume? Hiyo picha hakimu anaikubali kabisa kama evidence!! IGP unasubiri nini kujiuzulu?! Halafu ukute hao wote hapo 'vichwa vya ng'o**e' ni members wa tume!!!
   
 14. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #14
  Sep 3, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160

  Majibu tayari yapo hapo, kuwa kalipukiwa na kitu kinachodaiwa ni bomu sasa tume ya nini? picha zinaonesha Polisi wanamuua, polisi wanaunda tume, bomu lilitoka ghala la polisi, bunduki ilorusha bomu hilo ni ya polisi, waliokataza maandamano ni polisi, polisi walishamema atakayeamndamana atakiona ( whatever it means), polisi wanachunguza tukio hilo.

  Kesi ya nyani, hakimu ngedere, mwendesha mashtaka tumbiri unategemea nini???????


  Wanatufanya mazoba eti
   
 15. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #15
  Sep 3, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Majibu ya hiyo TUME tumeshaweza kuyabashiri, hayatatofautiana na yale ya Morogoro. Hatuchelewi kusikia, marehemu alijilipua mwenyewe ili kutafuta umaarufu. "Napendekeza huu mtindo wa kukimbilia kuundwa tume wakati vitu vipo wazi na vinajieleza ufe, sasa unaliathiri Taifa kwa kiwango kisichosadikika kama hivi"
   
 16. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #16
  Sep 3, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Hiyo tume ina ripoti kwa nani na inamchunguza nani? . Hiyo tume ipuuzwe kwani haina credibility ya kuchunguza hilo tukio huo ni usanii tupu. Lakini ifike mahali waTZ tuwazomee hawa jamaa tena wasije wakawapotezea watu mda wao kwa kuchunguza kitu chenye ushahidi wa picha. Kamata walioko kwenye picha wanafahamika including Kamuhanda
   
 17. unknown animal

  unknown animal JF-Expert Member

  #17
  Sep 3, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  yaani fisi anapewa mfupa alinde,kweli vitengo vyote ni makamasi matupu
   
 18. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #18
  Sep 3, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,317
  Likes Received: 2,601
  Trophy Points: 280
  Hahaha hii kali ina maana watajichunguza wao wenyewe...wao ni suspect namba moja
   
 19. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #19
  Sep 3, 2012
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,372
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  bora iundwe tume ya kuchunguza waliounda hiyo tume!
   
 20. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #20
  Sep 3, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,317
  Likes Received: 2,601
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Hii picha ina majibu mengi sana;
  Polisi wanaweza kutumia kila mbinu kujitetea lakini kwa hili wamecheza faulo mbaya...Jaribu kuiangalia kwa makini hii picha na kusoma kitendo cha kila askari. Utagundua kuwa wapo waliokuwa wanawazuia wenzao kuendeleza kipigo kwa mwandishi huyo(angalia movement za askari kanzu mwenye fulana ya bluu, pia kuna askari mwenye kofia nyekundu asiye na kikinga risasi, pia kuna askari upande wa pili mwenye kofia nyeusi)....
  Hivyo huyo mwandishi alipigwa tena kipigo kibaya na ndio maana yupo chini akiwa hajiwezi.
  Angalia pia mkono wa kulia wa huyo mwandishi, katika kiganja chake ameshika kamera, kwa hilo tu polisi walitakiwa watoe ulinzi maana kitendo cha kuwa na kifaa kama kamera ni ishara kuwa jamaa alikuwa ni mwanahabari naalikuwa katika harakati za kazi.
  Halafu pia ukijaribu kuivuta picha kwa karibu utaona kuna kitu kama moshi kinafuka karibu kabisa na mwili wa marehemu na moshi huo unaelekea moja kwa moja katika mtutu ulioelekezwa kwake, moshi huo bilashaka ni matokeo ya bomu lililopigwa na huyo askari wa kushoto kabisa aliyeelekeza mtutu wake kwa marehemu.
   
Loading...