Polisi Waunda Tume ya kuchunguza kifo cha Daudi Mwangosi

Tume ya nini wakati polisi wenyewe wanaonekana wanampiga virungu marehemu hapo?
 
966099517.JPG

Hii picha ina majibu mengi sana;
Polisi wanaweza kutumia kila mbinu kujitetea lakini kwa hili wamecheza faulo mbaya...Jaribu kuiangalia kwa makini hii picha na kusoma kitendo cha kila askari. Utagundua kuwa wapo waliokuwa wanawazuia wenzao kuendeleza kipigo kwa mwandishi huyo(angalia movement za askari kanzu mwenye fulana ya bluu, pia kuna askari mwenye kofia nyekundu asiye na kikinga risasi, pia kuna askari upande wa pili mwenye kofia nyeusi)....
Hivyo huyo mwandishi alipigwa tena kipigo kibaya na ndio maana yupo chini akiwa hajiwezi.
Angalia pia mkono wa kulia wa huyo mwandishi, katika kiganja chake ameshika kamera, kwa hilo tu polisi walitakiwa watoe ulinzi maana kitendo cha kuwa na kifaa kama kamera ni ishara kuwa jamaa alikuwa ni mwanahabari naalikuwa katika harakati za kazi.
Halafu pia ukijaribu kuivuta picha kwa karibu utaona kuna kitu kama moshi kinafuka karibu kabisa na mwili wa marehemu na moshi huo unaelekea moja kwa moja katika mtutu ulioelekezwa kwake, moshi huo bilashaka ni matokeo ya bomu lililopigwa na huyo askari wa kushoto kabisa aliyeelekeza mtutu wake kwa marehemu.

nje ya topic. Jina Kamuhanda ni moja ya majina ya Wahaya. Huyu jamaa ni mhaya mwenzangu kweli? Anayemfahamu vizuri amezaliwa wapi na historia ya wazazi wake naomba amwage hapa. Pengine kuna yaliyojificha nyuma ya huyu ndugu yetu kuongoza mauaji ya kutisha ndani ya muda mfupi huko Songea na jana Iringa.
 
Unaweza vipi kuua binadamu mwenzako halafu usiku ukapata usingizi? Jeshi la kishetani hili
 
Unaweza vipi kuua binadamu mwenzako halafu usiku ukapata usingizi? Jeshi la kishetani hili

wao wanaupata tena vizuri kabisa maana wameacha majukumu yao ya msingi, sasa wananyanyasa raia wasio na hatia
 
Wanamkabidhi tena ngedere kesi ya nyani? Pia ktk picha iliyoonyeshwa hapo juu haihitaji kwenda shule wala utimamu wa akili kumjua muuwaji waache kutuhadaa kwani haya mambo yana mwisho na Tz haijakuwepo kwa ajili ya kuongozwa na ccm milele
 
Sasa ushahidi wa picha na video upo sasa tume ni ya kufanya nini kama sio wanataka tu kuwapumbaza wananchi na kujitengenezea ulaji?Kwa mwendo huu Tanzania tutaendelea kweli?,nchi ya ajabu sana hii
 
Jamani mbona sioni hata membber mmoja wa chadema? au mwandishi wa habari ndo chadema?
 
"Mungu naomba nisaidie maana naona naweza kukosa mbingu bure kwa sababu ya kuwachukia
hawa polisi wa Tz wasiotumia akili,wakiagizwa waue wanaua ndugu zao bila kuwaza mara ya pili
kuwa wanafanya hivyo kwa maslahi ya wakubwa wao wanaotetea matumbo yao,na maslahi ya
bwana zao wanasiasa wa serikali dhaifu,isiyojali watu wake"
 
Kama polisi hawakukusudia kummwua Daudi Mwangosi (RIP) wanaonekana kwenye picha wachukuliwe hatua.

Hapo kama IGP ana akili timamu alitakiwa huyo RPC mpaka saizi awe ananyea debe na kutaja vijana wake wengine hao walio mzunguka
 
Yani hii ni Kali ya karne badala chama cha waandishi wa habari waunde tume polisi ndio wanajiundia tume? Nani kawaambia tunaziamini hizo tume? Kila kitu tume tume tume Hata vyenye ushahidi tume au watu hawajui maana ya tume? Au Sababu tumesha lishwa limbwata la tume na mahakama ili tusiendelee kuhoji? Nchii hii tukifika 2015 tutakuwa tumekufa wengi ila hawata tumaliza kwani wanazaliwa Wana mapinduzi kila Siku ila ingekuwa amri yangu tungeandamana kwa Siku 14 kulaani mauaji yote ya polisi kwa Raia na pia kuwarehemu wote waliopoteza maisha kwa ajili ya uzembe au siasa za policeccm
 
Hapo kama IGP ana akili timamu alitakiwa huyo RPC mpaka saizi awe ananyea debe na kutaja vijana wake wengine hao walio mzunguka

Huwezi Kuua mti kwa kukata majani au matawi Bali unaweza Kuua mti kwa kukata shina na mizizi yeye IGP angejiweka mwenyewe lockup Kama mshitakiwa namba moja na wengine wafuate
 
Mtuhumiwa mkuu anaunda tume kujichunguza mwenyewe!!! Kichekesho kingine hiki. Labda ingeundwa tume huru kama ile ya Jaji Kipenka iliyochunguza mauaji ya wale wafanyabiashara wa madini wa Ulanga yaliyofanywa na kina Zombe.
 
Tume ya nini wakati wanahabari wamemuonyesha muuaji ,picha zinajionyesha ,mahala walipomuulia panajulikana na aliyewatuma ni Jakaya Kikwete na shemeji yake IGP Saidi Mwema,mapepo na majini yao ni kwamba kable ya 2015 kwa kutumia polisi watakuwa wameua viongozi wote wa chadema na wananchi kama laki moja huo ndio ukweli manake dhamira yao inaonekana wazi sasa
Mafreemasons wanatoa watu kafara
 
A bunch of Jokers!!:angry:.....Seriously!! They must be on some dose of cheap drugs that affect their thinking!
 
Huwezi Kuua mti kwa kukata majani au matawi Bali unaweza Kuua mti kwa kukata shina na mizizi yeye IGP angejiweka mwenyewe lockup Kama mshitakiwa namba moja na wengine wafuate

Hivi waziri Nchimbi anasubiri nini kujiuzuru? au anasubiri jamaa arudi msibani Ethiopia?
 
uchunguzi huo utavishirikisha vyombo vya usalama kutoka Jeshi la Polisi pamoja na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) 'kuwa Jeshi la Polisi limeunda tume itakayowahusisha Maofisa kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ pamoja Mkurugenzi wa Makosi ya Jinai Robert Manumba, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema ili kubaini ukweli kuhusu kiliochosababisha kifo cha mwandishi huyo basi tusubiri matokeo ya uchunguzi huo' alisema Chagonja.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom