Mtoto wa Mkulima
JF-Expert Member
- Apr 12, 2007
- 681
- 126
Polisi waua majambazi 3,wakamata bunduki AK47
Magesa Magesa na Hemed Kivuyo Arusha
JESHI la Polisi mkoani hapa limeua majambazi watatu, kujeruhi mmoja na kukamata bunduki aina ya AK 47.
Akithibitisha jana kukamatwa kwa majambazi hao, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Bw. Wenceslaus Magoha, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa saba mchana katika kijiji cha Ngoile, Ngorongoro.
Kamanda aliwataja majambazi waliouawa kuwa ni Moseko Piring'o (25), Lekioni Lalepa (28) na Kisese Sanof (25) wote wakazi wa kijiji cha Harash na alimtaja aliyejeruhiwa kuwa ni Lengotonye Tilipe (25), ambaye alipigwa risasi katika mkono wa kushoto.
Kabla ya kukamatwa kwa watu hao ilidaiwa kuwa walishafanya uhalifu katika maeneo kadhaa ya Ngorongoro na baada ya hapo walikuja kufanya uhalifu mwingine na kupata upinzani mkubwa kutoka kwa askari wa hifadhi ya wanyama.
Kamanda alisema majambazi hao walijibizana na polisi kwa risasi na kuvunja kioo cha mbele cha gari la hifadhi ya wanyama na kuharibu gari la Polisi katika ubavu wa kulia na kumjeruhi raia, Bw. Kereto Lambala (18), kwenye mguu wa kulia.
Kabla ya kukamatwa kwa majambazi hao, Oktoba 24 walimvamia Bw. Sapia Kanyi (28) katika duka lake na kumjeru kwa risasi mguu wa kushoto na kumpora kiasi cha sh. 400,000.
Kamanda Magoha aliongeza kuwa uhalifu wa majambazi hao haukuishia hapo bali walimvamia Bw. Lazaro Saitoti na kumpora sh. milioni 1.5 na kilo 10 za sukari na kumalizia kwa Bw. Moses King (22) ambaye walimwibia sh. 100,000.
Ilidaiwa kuwa jambazi mmoja aliyekuwa na bunduki aina ya AK 47 alikuwa akiwapa polisi upinzani mkali, lakini baada ya risasi kumwishia alitupa silaha chini na kunyoosha mikono na polisi kumuua.
Miili ya majambazi hao imehifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospitali ya wilaya ya Karatu na mmoja wao ambaye ni majeruhi, anatibiwa katika hospitali hiyo chini ya ulinzi mkali wa Polisi.
Yamekuwapo matukio ya uporaji wa mara kwa mara katika hifadhi ya Ngorongoro na kutishia usalama wa raia wema na watalii wanaotembelea mbuga hizo.
http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=4324