Polisi waua majambazi 3,wakamata bunduki AK47

Mtoto wa Mkulima

JF-Expert Member
Apr 12, 2007
681
126
Polisi waua majambazi 3,wakamata bunduki AK47Magesa Magesa na Hemed Kivuyo Arusha

JESHI la Polisi mkoani hapa limeua majambazi watatu, kujeruhi mmoja na kukamata bunduki aina ya AK 47.

Akithibitisha jana kukamatwa kwa majambazi hao, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Bw. Wenceslaus Magoha, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa saba mchana katika kijiji cha Ngoile, Ngorongoro.

Kamanda aliwataja majambazi waliouawa kuwa ni Moseko Piring'o (25), Lekioni Lalepa (28) na Kisese Sanof (25) wote wakazi wa kijiji cha Harash na alimtaja aliyejeruhiwa kuwa ni Lengotonye Tilipe (25), ambaye alipigwa risasi katika mkono wa kushoto.

Kabla ya kukamatwa kwa watu hao ilidaiwa kuwa walishafanya uhalifu katika maeneo kadhaa ya Ngorongoro na baada ya hapo walikuja kufanya uhalifu mwingine na kupata upinzani mkubwa kutoka kwa askari wa hifadhi ya wanyama.

Kamanda alisema majambazi hao walijibizana na polisi kwa risasi na kuvunja kioo cha mbele cha gari la hifadhi ya wanyama na kuharibu gari la Polisi katika ubavu wa kulia na kumjeruhi raia, Bw. Kereto Lambala (18), kwenye mguu wa kulia.

Kabla ya kukamatwa kwa majambazi hao, Oktoba 24 walimvamia Bw. Sapia Kanyi (28) katika duka lake na kumjeru kwa risasi mguu wa kushoto na kumpora kiasi cha sh. 400,000.

Kamanda Magoha aliongeza kuwa uhalifu wa majambazi hao haukuishia hapo bali walimvamia Bw. Lazaro Saitoti na kumpora sh. milioni 1.5 na kilo 10 za sukari na kumalizia kwa Bw. Moses King (22) ambaye walimwibia sh. 100,000.

Ilidaiwa kuwa jambazi mmoja aliyekuwa na bunduki aina ya AK 47 alikuwa akiwapa polisi upinzani mkali, lakini baada ya risasi kumwishia alitupa silaha chini na kunyoosha mikono na polisi kumuua.

Miili ya majambazi hao imehifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospitali ya wilaya ya Karatu na mmoja wao ambaye ni majeruhi, anatibiwa katika hospitali hiyo chini ya ulinzi mkali wa Polisi.

Yamekuwapo matukio ya uporaji wa mara kwa mara katika hifadhi ya Ngorongoro na kutishia usalama wa raia wema na watalii wanaotembelea mbuga hizo.

http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=4324
 
Hapa napo vipi? au napo ilibidi polisi auwawe walau polisi mmoja ndio wawe ni majambazi. Na hapo kama jamaa alitupa silaha chini na kunyoosha mikono kwanini polisi walimua?
 
walimuua kwa sababu wana uwezo huo na hakuna mtu anayetakiwa kuhoji kazi nzuri ya Polisi!! WAmetuondolea majambazi!!
 
hii kama kweli, ni kinyume na sheria ya jeshi lapolisi inahitaji kuthibitishwa na sheria kufuata mkondo.

lkn jee ni kweli au spinning za mwandishi?
 
Walipouwawa Jamaa wakutoka Kenya watu hapa walipiga kelele wakajipatia na makala ya kuandika kwenye Magazeti sasa hapa mbona wako kimya?
 
mtoto wa mkulima kuna faida gani ya kuandika kuhusu hili wakati ilishatolewa leseni kuwa Polisi wanaweza kuua mtu yeyote as long as wanamuita jambazi, it is useless! waacha wawaue hadi Watanzania watakapoona haja ya kulifunga jeshi lao kamba kwa utawala wa sheria. Nilipoandika kutaka uchunguzi nenda kaangalie watu walisema nini, kwanini leo kuuliwa Watanzania "majambazi" iwe issue kubwa? Tunavuna walichopanda!!
 
A
Polisi waua majambazi 3,wakamata bunduki AK47Magesa Magesa na Hemed Kivuyo Arusha

JESHI la Polisi mkoani hapa limeua majambazi watatu, kujeruhi mmoja na kukamata bunduki aina ya AK 47.

Akithibitisha jana kukamatwa kwa majambazi hao, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Bw. Wenceslaus Magoha, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa saba mchana katika kijiji cha Ngoile, Ngorongoro.

Kamanda aliwataja majambazi waliouawa kuwa ni Moseko Piring'o (25), Lekioni Lalepa (28) na Kisese Sanof (25) wote wakazi wa kijiji cha Harash na alimtaja aliyejeruhiwa kuwa ni Lengotonye Tilipe (25), ambaye alipigwa risasi katika mkono wa kushoto.

Kabla ya kukamatwa kwa watu hao ilidaiwa kuwa walishafanya uhalifu katika maeneo kadhaa ya Ngorongoro na baada ya hapo walikuja kufanya uhalifu mwingine na kupata upinzani mkubwa kutoka kwa askari wa hifadhi ya wanyama.

Kamanda alisema majambazi hao walijibizana na polisi kwa risasi na kuvunja kioo cha mbele cha gari la hifadhi ya wanyama na kuharibu gari la Polisi katika ubavu wa kulia na kumjeruhi raia, Bw. Kereto Lambala (18), kwenye mguu wa kulia.

Kabla ya kukamatwa kwa majambazi hao, Oktoba 24 walimvamia Bw. Sapia Kanyi (28) katika duka lake na kumjeru kwa risasi mguu wa kushoto na kumpora kiasi cha sh. 400,000.

Kamanda Magoha aliongeza kuwa uhalifu wa majambazi hao haukuishia hapo bali walimvamia Bw. Lazaro Saitoti na kumpora sh. milioni 1.5 na kilo 10 za sukari na kumalizia kwa Bw. Moses King (22) ambaye walimwibia sh. 100,000.

Ilidaiwa kuwa jambazi mmoja aliyekuwa na bunduki aina ya AK 47 alikuwa akiwapa polisi upinzani mkali, lakini baada ya risasi kumwishia alitupa silaha chini na kunyoosha mikono na polisi kumuua.

Miili ya majambazi hao imehifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospitali ya wilaya ya Karatu na mmoja wao ambaye ni majeruhi, anatibiwa katika hospitali hiyo chini ya ulinzi mkali wa Polisi.

Yamekuwapo matukio ya uporaji wa mara kwa mara katika hifadhi ya Ngorongoro na kutishia usalama wa raia wema na watalii wanaotembelea mbuga hizo.

http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=4324

"AKANYOOSHA MIKONO NA POLISI WAKAMUUA!"
 
Back
Top Bottom