Polisi wanapomlinda mwenye danguro anayedhalilisha wasichana wadogo kingono Mwananyamala

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,899
Danguro%20Mwananyamala.jpg

Nyumba inayoonekana ni ghorofa inayodaiwa kutumiwa kama
danguro iliyopo Mwananyamala Magengeni jijini Dar es Salaam

Yatima abakwa kwenye danguro Dar miaka 10
  • Alawitiwa na kuambukizwa virusi vya ukimwi
  • Polisi naye adaiwa kumbaka akiwa kituoni
Msichana yatima, mkazi wa mkoani Manyara, amefungiwa kwenye danguro kwa zaidi ya miaka 10 akinyanyaswa kingono, kuteswa na kuambukizwa Virusi Vya Ukimwi (VVU).Msichana huyo aliyeondolewa nyumbani kwao Oysterbay mjini Babat,i alilaghaiwa na mwanamke aliyejifanya kuwa msamaria mwema, akitangaza nia ya kumsaidia kielimu na kimaisha, kufuatia kifo cha mama yake mzazi.

Msichana aliyefikwa na masahibu hayo ni Sara Tarimo (27) ambaye aliangukia mikononi mwa mwanamke mwenye danguro hilo, Abia Lucas (44) anayeishi Mwananyamala Magengeni.Ilikuwa ni baada ya kifo cha mama yake Magreth Kitinati, aliyekuwa akiishi naye Oysterbay huko Manyara.Sara anasema mwanamke huyo alimtoa kijijini kwao hadi jijini Dar es Salaam, na kumshinikiza kwenye `utumwa wa ngono' kwa kipindi cha miaka 10 akiwa amefungiwa ndani.Akiwa mwanafunzi wa shule ya msingi, mama yake mzazi alifariki, hivyo ujio wa msamaria huyo ulikuwa faraja na tumaini jipya kwa maisha yake. Haikuwa hivyo.

Sara alisema alipoteza bikra yake baada ya kumlazimisha kufanya ngono na mwanamume mtu mzima, aliyembaka na ukawa mwanzo wa kutumiwa kingoni na wanaume wa kila aina.
Sara alisema alifanywa unyanyasaji huo akiwa na miaka 13 na kwamba hilo lilikuwa tukio lake la kwanza kukutana na mwanaume.Baada ya kufanikiwa kutoroka na kuwataarifu polisi nyendo za mama huyo ambaye sasa anashikiliwa kwa mahojiano, Sara anasimulia kumbukumbu za kusikitisha za miaka aliyoipoteza katika himaya ya danguro la ‘msamaria.'

HISTORIA YAKE
Sara ni mmoja wa watoto watatu katika familia yao. Kaka yake Emmanuel Tarimo (31) na dada yake Neema Tarimo.Wakati akipochukuliwa na ‘msamaria' alimuacha kaka yake huko Babati akijitafutia riziki kwa kubeba mizigo na dada yake akiendelea na masomo ya shule ya msingi.Anasikitika kuwa katika maisha yake hakubahatika kumfahamu baba yake, lakini aliwahi kuelezwa na mama yake kuwa ni mwenyeji wa Kilimanjaro.Mama yake ndiye aliyekuwa anatunza familia yao licha ya kwamba hakuwa na ajira rasmi, wala biashara za kudumu.Mazingira hayo, yalimlazimisha kukatisha masomo akiwa darasa la tatu katika shule ya Msingi Idangunyii.Anasema alikuwa na ndoto ya kupata elimu zaidi, lakini kifo cha mama yake kilisababisha ajione kuwa hana bahati.

MAISHA KWENYE DANGURO
Alisimulia kuwa, baada ya ‘msamaria ' kujitokeza na kumwahidi kuwa atamtafutia shule na kugharamia elimu alimsikiliza na kumfuata hadi jijini Dar es Salaam.Sara alieleza kuwa mwanamke huyo alipofika nyumbani kwao Babat, alieleza kuwa anatafuta wasichana 10 kwa ajili ya kufanya kazi za ndani kwa familia za Dar es Salaam."Aliiambia familia yangu kuwa, hata kama wasichana watakaopatikana watakuwa wanasoma wataendelezwa mara baada ya kufika mjini wakati wakiendelea na kazi ,'' anasema na kuongeza:"Nakumbuka ilikuwa siku ya Ijumaa mwaka 2003, tuliondoka kwa usafiri wa basi tukiwa 10 ingawa sikuwatambua wenzangu kwa sababu alituchukua kutoka katika vijiji tofauti."

Alisimulia kuwa walifika nyumbani kwa mwanamke huyo Mwananyamala Magengeni kwenye ghorofa mbili, ambayo juu linaonyesha ujenzi unaendelea.Alisema wakiwa nyumbani kwa mama huyo, walibadilishwa mavazi kutoka yale waliyotoka nayo kijijini na kupewa nguo nyingine- sketi fupi, kaptula na blauzi maarufu kama ‘vitop'.Alikumbuka kuwa baada ya kupewa nguo hizo, walitakiwa kila mmoja akajipumzishe kwenye chumba chake vilivyokuwa ghorofa ya kwanza.

KUBAKWA MARA YA KWANZA
Alieleza kuwa siku hiyo akiwa chumbani kwake mlango uligongwa na alipouliza ni nani, alijibiwa na sauti ya kiume kuwa ni mlinzi.Alipofungua, mwanaume mtu mzima alimwambia wakati huo sio wa kulala bali ni wa kazi na kumtaka avue nguo huku akimtisha na bisibisi.Vitisho vilitawala akilazimishwa kufanya ngono kwa nguvu na mwanaume huyo aliyetumia bisibisi kumchoma mdomoni na mkononi karibu na kiwiko."Nilipiga kelele za kuomba msaada lakini hakuna aliyekuja kunisaidia hadi yule mzee alipomaliza haja yake na kuniacha nikiwa kwenye maumivu makali."

Anasema hakuamini kilichotokea na kulalamika kwa mwenyeji wake…."Nilimfuata yule mama kumweleza yaliyonitokea cha ajabu aliniambia hiyo ndiyo kazi niliyofuata mjini."Anasema "baada ya kupewa maneno hayo makali nilipelekwa kwa daktari wa hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi zaidi."Anasema aliendelea kuwa mtumwa wa ngono kwa sababu baada ya matibabu akawa anaendelea na kazi hiyo.

Sara anasema katika hospitali hiyo ndiko walikokuwa wanatibiwa na mwanamke huyo alimweleza kuwa huyo ni daktari wao.Anasema aliwahi kudhalilishwa kingono na wanaume zaidi ya 10 kwa siku moja, wakiwa wa rika, tabia na maumbile tofauti."Nakumbuka siku moja alikuja mteja aliyekuwa amelewa, akaniambia amelipa fedha nyingi kwa mama na anachotaka ni kunitumia kinyume cha maumbile.""Sijawahi kufanya hivyo, nilipokataa alitoa kisu na kunitishia…alinilazimisha nivue nguo na kulala kitandani kabla hajanijeruhi." Anasema."Nikiwa kitandani alidondosha kisu tumboni mwangu, akakilalia na kunijeruhi, nikakimbizwa Mwananyamala na kutibiwa na yule daktari wa mwanzo niliyeambiwa ni tabibu wetu ambaye alinishona sehemu nilizojeruhiwa na alikuja nyumbani kunitoa nyuzi," anasema
MALIPO

Sara anasema hakuwahi kulipwa japo wakati wakiendelea na kazi hiyo, mwanamke huyo aliwaeleza kuwa malipo yao ni Sh. 30,000 kwa mwezi na kwamba wangelipwa baada ya kukamilisha alichokitaka.Akielezea faida waliyomtengenezea mama huyo alisema alikuwa akitoza kati ya Sh. 10,000 hadi 15,000 kwa wateja waliofanya ngono kwa njia ya kawaida na wale waliokuwa wakiwaingilia kinyume cha maumbile ilikuwa aliwalipisha kati ya Sh. 30,000 na 50,000.Anaeleza kuwa walikuwa wakipatiwa matibabu, chakula na kununuliwa mavazi lakini hawakuruhusiwa kutoka nje ya nyumba hiyo."Niliwahi kumhoji mama kwa nini alitudanganya unatuleta mjini kwa ajili ya kufanya kazi za ndani na kutusomesha?"" Nilimuomba anirudishe nyumbani, lakini alikataa na kuniambia kazi yake itakapokwisha nitarudi sikuyaelewa majibu haya," anasema.

ALIVYOTOROKA
Alisema baada ya kutumikishwa kwa muongo mmoja, Februari 4, 2013, siku aliyofanikiwa kutoroka baada ya mwanaume aliyefanya naye mapenzi siku ya kwanza kufika kwenye danguro hilo akihitaji huduma yake."Alilipia na kuja chumbani kwangu na kunieleza kuwa lile embe lililokula kipindi kile lilikuwa bichi, hivyo amekuja kwa mara nyingine likiwa limeiva na baada ya kumaliza haja zake." "Aliniambia anataka kunipa zawadi hivyo niliporuhusiwa na mama tuliondoka naye, tukipita maeneo tofauti akinielekeza majina ya mitaa na mwishowe tuliingia sokoni Kariakoo," anasimulia.

Waliondoka na gari aina ya Volkswagen hadi Kariakoo na wakati huo alihisi njaa na kumuomba kabla ya kumnunulia zawadi, wanunue kwanza chakula.Mteja huyo katika mazungumzo yake alimfahamisha kuwa ni mwanasheria anayefanya kazi manispaa japo hakutaja jina. "Tukiwa njiani alikokuwa amekusudia kunipeleka nilikuwa nikitembea nyuma yake, hapo ndipo nilipotoroka nikikimbia bila kujua ninaelekea wapi, nilizunguka na hatimaye giza liliingia na watu walipungua kwenye eneo nililokuwapo.""Sijui ilikuwa saa ngapi, lakini niliona gari la polisi niliamua kuwafuata nikamueleza askari wa kike mkasa mzima," alisema.Anasema walikwenda kituo kikuu cha polisi na kuchukuliwa maelezo lakini pia alimpatia nguo nyingine kwa vile alikuwa amevaa mavazi yasiyo na staha. "Siku iliyofuata niliambiwa kuna dawati la kushughulikia masuala ya wanawake, lakini kwa wakati huo wahusika hawakupo. Ilipofika Alhamisi nilikabidhiwa kwa askari mwingine anaitwa Happy." Aliongeza: "tuliondoka naye hadi Oysterbay polisi, huko walitoka askari kadhaa kwenda Mwananyamala nyumbani kwa mama huyo."

Sara alisema walifanya upekuzi kwenye vyumba walivyokuwa wakilala bila mafanikio, walishuka chini na kumuamuru afungue moja ya vyumba vilivyokuwa vimefungwa lakini mwanamke huyo alikataa na polisi walimuagiza aende kituoni kuandika maelezo dhidi ya tuhuma hizo.Alieleza kuwa wakati mtuhumiwa huyo akiwa mahabusu watoto wake anaoishi nao mmoja mwanaume mwenye miaka 27 na mwingine wa kike walimsihi afute kesi hiyo, lakini alikataa na kuongeza kwa alifungua jalada la uchunguzi lenye kumbukumbu RB/2468/2013 la Februari 7.

VYOMBO VYA HABARI
Alisema amefikisha suala hili kwenye vyombo vya habari akiomba msaada wa nauli ili aweze kurudi kwao pamoja na chakula."Kabla sijafika NIPASHE nilitoa taarifa kwenye Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ambacho kimeahidi kulifanyia kazi suala langu," anasema.

AFYA YAKE
Sara analalamikia kuwa na vivimbe mbavuni na sehemu za siri na anahofu kuwa huenda ameambukizwa magonjwa ya ngono na Ukimwi.Anasema ana wasiwasi kwa vile aliwahi kupata vipele vingi mwilini japo daktari wao alimueleza kuwa vilisababishwa na joto lakini sasa vimekuwa uvimbe mkubwa.Anasema wakiwa kwenye danguro hilo daktari wao alikuwa anawapa dawa mara kwa mara ambazo hawafahamu zilikusudiwa kutibu nini na zilipomalizika aliendelea kuzileta japo hakuwahi kutumia tiba hiyo.

KONDOMU
Anasema baadhi ya wanaume wenye ndoa walitumia kondomu wakati wa kufanya ngono lakini asilimia kubwa ya wateja wa danguro hilo walikuwa hawatumii mipira hiyo ya kiume."Walikuwa wananiambia nina mke ninampenda hivyo natumia kondomu lakini wengine walikuwa hawatumii, chumbani tulikuwa tunawekewa kondomu lakini ukiwaambia wazitumie wanakataa."

KUGUNDULIKA NA VVU
Sara anasema Jumatatu Februari 11, akiwa polisi Oysterbay, aliamriwa kuondoka eneo hilo kwani si sehemu ya kuishi nail kufungua mashtaka."Nilikwenda kituo cha mabasi ya mikoani Ubungo lakini usiku nilizidiwa ilipofika asubuhi nilikwenda zahanati ya Mwenge nilikotibiwa na kuelezwa kuwa nimeambukizwa Virusi Vya Ukimwi (VVU) na kutakiwa kuanza kutumia dawa."

KULAWITIWA NA POLISI
Wakati uchunguzi wa tuhuma dhidi ya Abia ukiendelea, inadaiwa kuwa usiku wa Jumatano polisi wa kituo cha Oysterbay alimlawiti Sara eneo lenye migomba kituoni hapo.Akizungumza na NIPASHE kwenye kituo cha trafiki kilichopo kituo cha mabasi ya mikoani Ubungo, alisema alifanyiwa unyama huo baada ya polisi kumfuata akiwa amelala kwenye maegesho ya magari.Anasema alikwenda Ubungo kuchukua nguo alizozificha hapo na akiwa huko alikutana na askari huyo ambaye alimueleza matatizo yake, ndipo akamtaka wakale chakula."Baada ya chakula wakati tunarudi kituoni, aliniambia nimlipe kwa kumruhusu kunifanyia tendo hilo lakini nilikataa na askari huyo alinishika kwa nguvu na kunilawiti." Anaongeza kuwa kutokana na kitendo hicho aliondoka kituoni hapo saa 12:00 asubuhi na kufikisha taarifa ITV kwa vile aliona polisi hawakuwa na msaada kwake.

Baada ya kutoa malalamiko yake na kusaidiwa na wafanyakazi wa ITV alijitokeza polisi mwanamke na kumchukua kwa matibabu kwenye zahanati ambayo Sara alisema haifahamu na baadaye kupelekwa kituo cha mabasi Ubungo ili kurudishwa nyumbani kwao Manyara.Alimweleza Mwandishi Wetu kuwa aliomba simu kutoka mtu aliyekuwa kituoni hapo ili awasiliane naye kabla hajasafirishwa na polisi hao.Baada ya mwandishi kufika Ubungo na kufanya mahojiano na Sara gari la polisi lenye namba PT 2083 lilifika na kumpeleka polisi Oysterbay na kuandikisha maelezo.

MAELEZO YA POLISI
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, John Mtalimbo, alipofuatwa alisema taarifa zipo kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya Kinondoni (OCD).Aidha, alisema kwa mujibu wa OCD msichana huyo amekuwa akitangatanga maeneo ya Buguruni na sehemu nyingine ambazo hakuzitaja."Naona lengo lake ni kutuchafua, kwa nini asubuhi alikuja ITV na sio kutoa taarifa kwetu kama amelawitiwa na askari wetu, anatuchafua," alisisitiza Kamanda Mtalimbo. Alikiri kuwa siku mbili zilizopita polisi ilimtafutia tiketi ili kumrudisha kwao lakini haikufanikiwa.Kamanda alipoulizwa sababu za kumsafirisha Sara wakati amefungua kesi ya kuuzwa kimwili kwenye danguro alisema ni kutokana na kukosa makazi.

Awali, Mwandishi Wetu alinasa mawasiliano ya simu ya Kamanda Mtalimbo na mtu aliyeelezwa kuwa ni OCD akimwelekeza jinsi yakuandika maelezo dhidi ya binti huyo.
Alisikika akisema:"Inabidi tujipange, hapa watakuja waandishi wa habari, (bila kujua kama mwandishi wetu alikuwepo eneo hilo), watataka kujua kinachoendelea na kumshauri andike kuwa walikubaliana kufanya ngono." Licha ya kusikia kilichozungumzwa juu ya mlalamikaji huyo alipoingia ofisi kwake na kujitambulisha na kuuliza habari za Sara Mtalimbo alimweleza kuwa hana taarifa hizo na kwamba anasubiri zitoke kwa OCD.

Akisoma maelezo ya OCD wa Kinondoni, Mtalimbo alisema Februari 2, mwaka huu Sara aliripoti kituo hapo kuwa alikuwa akiishi Mwananyamala alikokuwa akifanyishwa kazi za kuuza mwili na mtuhumiwa aliyemtaja kwa jina la Abia.Alisema baada ya polisi kupokea malalamiko hayo walikwenda Mwananyamala kuonyeshwa danguro hilo na polisi walipomkamata Abia mlalamikaji alishindwa kumtambua na kuongeza kuwa walifungua jalada la uchunguzi na kwa sasa mtuhumiwa yuko nje kwa dhamana na Sara aliendelea kubaki kituoni hapo hadi alipoonekana ITV jana asubuhi.

Kamanda alielezwa kuwa katika mahojiano ya Sara na OCD alimfahamisha kuwa Jumatano wiki hii akiwa Ubungo alitongozwa na askari aliyemuahidi kumpatia Sh. 10,000 baada ya kumlawiti."Walikwenda kwa makubaliano migombani na baada ya kufanya kitendo hicho, askari alimpa Sh. 20,000 ," alisema na kuhoji sababu za msichana huyo kutofikisha tukio hilo kituoni badala yake alikimbilia ITV.Hata hivyo alipoulizwa iwapo mlalamikaji amemtambua askari huyo kupitia gwaride la utambuzi na iwapo alichukuliwa hatua alisema bado na kuongeza:"Maelezo niliyokupa ndiyo mambo mengine yatafuata baadaye."

NYUMBANI KWA ABIA
Gazeti hili likafika nyumbani kwa Abia na kukutana na binti alijitambulisha kuwa anafanyakazi za ndani na kueleza kuwa mwenye nyumba hakuwepo na hajui alikokwenda. Alipoulizwa kuhusu danguro binti huyo mwenye miaka kati ya 13 na 20 alisema hafahamu kinachoendelea kwani mwajiri wake anamkataza kutoka nje kukutana na majirani lakini akadokeza kuwa Jumatatu wiki hii walikuja polisi wakamkamata mama huyo ambaye siku iliyofuata alirudi nyumbani.

KUWEPO MADANGURO
Majirani wa mtuhumiwa walikataa kutoa ushirikiano kwa kuhofia wanazungumza na polisi lakini Mwenyekiti Serikali ya Mtaa Kata ya Makumbusho, Said Muhunzi, alisema uchunguzi uliofanyika umebaini kuwepo kwa danguro hilo. "Nimebaini wapo wasichana wenye umri mdogo ambao wanaonekana na majirani wakiingizwa hapo kila mara na baadhi ya watu, majirani wamethibitisha hili," alisema.

Aliongeza kuwa, Jumatano iliyopita kikundi chake cha ulinzi shirikishi, kilifika kwenye nyumba hiyo saa 7:00 usiku na kumkuta mtuhumiwa Abia na watu wengine wakiwa nje na kuwataka waingie ndani kwa kwani haukuwa muda wa kukaa nje. "Ijumaa iliyopita niliwaambia walinzi waende tena saa 8:00 usiku kuangalia kama watawakuta nje, waliona watu watano wakinywa pombe nje," alisema na kuongeza: Aliongeza kuwa watu hao ni Abia, Salome, mtoto wa marehemu mumewe na wanaume watatu na kuongeza kuwa kijana mmoja anayeitwa Juma alifahamika baada ya wenzake kumtaja kutokana na kuwatishia walinzi hao kwa bastola.

Muhunzi alisema Salome anatumiwa na Abia kutafuta mabinti kwa ajili ya danguro hilo na kwamba kufuatia tukio hilo la walinzi kutishiwa walifungua kesi tatu katika kituo cha polisi Minazini alizozitaja kuwa ni kukutwa nje wakinywa pombe usiku,kutishia kuua na kuzuia ulinzi usifanyikeAlisema walifungua jalada lenye kumbukumbua RB/118/2013 na kesi hiyo ilifikishwa kituo cha polisi Oysterbay na kukuabidhiwa kwa mpelelezi aliyemtaja kwa jina moja la Mwesiga
Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo, alisema eneo lake moja ya changamoto zilizopo ni kuibuka kwa madanguro na baadhi ya wasichana wenye umri mdogo kujiuza kwenye baa nyakati za usiku.

Alitaja baadhi ya baa (majina tunayo ) kuwa zinaongoza kwa kuwa na wasichana wengi wanaojiuza na kwamba wanatoa elimu kupitia kamati ya Ukimwi na kufanya msako lakini tatizo ni kubwa.Alitaja danguro maarufu liitwalo ‘kwa wahaya' lililopo Minazini na kusema kuwa ofisi yake inawajua watuhumiwa kwa majina.Habari zilizozifikia gazeti hili jana asubuhi, Sara alikuwa amewekwa mahabusu kituoni hapo.

Source: NIPASHE
Mandishi:
ROMANA MALLYA

Habari hii nimeihariri mpangilio ili kutochosha msomaji kutokana na kuwa habari ndefu kidogo, lakini inaleta picha nzuri kazi kubwa iliyofanywa na huyu mwandishi katika suala hili. Licha ya makosa madogo madogo lakini imekizi kiwango, nampongeza sana Mwandishi Romana Mallya.

 
Shukrani kubwa zimwendee ROMANA MALLYA Mwandishi wa Nipashe kwa kazi kubwa na nzuri aliyoifanya. Kiwango hiki cha utafiti na uandishi ndicho kinachotakiwa katika kujienga jamii yetu. Waandishi wanatakiwa kupenya huko kupata habari za udhalilishaji kama huu.

Polisi badala ya kumshaidia mwadhirika wakati serikali inayo wizara maaluma kwa shughuli hizo, halafu wanafanya mbinu za kumridisha mwadhirika mkoani wakati ameshafungua faili la mashtaka kituoni. Maana yake yule mama aliwapo hongo au?
 
Hii dunia haina huruma tena, jamani watu maskini wananyanyasika sana.....
 
duu hii inasikitisha sana ila cha msingi tuu ni kwamba haki na sheria za nchi hapa zifuatwe kwasababu kumekuwa na tabia ya watu kuadhibiwa bila makosa na pia kumekuwa na tabia ya polisi kushirikiana na baadhi ya watu ili kutunga kesi za uongo hasa pale inapokuwa inahusu malalamiko ya mtu kuwa kabakwa.ushauri wangu kila kitu kwa maana ya taaluma inapaswa izingatiwe hasa kwa hawa polisi inabidi wawe makini sana katika taaluma yao ni si kufanya kazi kwa hisia na ikibainika basi waliohusika wachukuliwe hatua zinazo staili bila kujari wazifa wa mtu.kwa sasa ni hayo tu.
 
Hii dunia haina huruma tena, jamani watu maskini wananyanyasika sana.....

Kinachonishangaza vyombo vya dola vilipofika kwenye jengo hili na kutaka mhusika mmiliki wa madanguro hayo afungue milango akawakatalia, inawezekana hili polisi wakubali mbona sehemu nyingine huwa wanapiga mateke milango ya watu? Labda danguro hilo hutumiwa na baadhi ya polisi pia.
 
duu hii inasikitisha sana ila cha msingi tuu ni kwamba haki na sheria za nchi hapa zifuatwe kwasababu kumekuwa na tabia ya watu kuadhibiwa bila makosa na pia kumekuwa na tabia ya polisi kushirikiana na baadhi ya watu ili kutunga kesi za uongo hasa pale inapokuwa inahusu malalamiko ya mtu kuwa kabakwa.ushauri wangu kila kitu kwa maana ya taaluma inapaswa izingatiwe hasa kwa hawa polisi inabidi wawe makini sana katika taaluma yao ni si kufanya kazi kwa hisia na ikibainika basi waliohusika wachukuliwe hatua zinazo staili bila kujari wazifa wa mtu.kwa sasa ni hayo tu.
Ndugu yangu nchi hii hakuna anayejali haki na sheria za nchi. Wanaotakiwa kulinda sheria ndio wavunjifu wakubwa wa sheria.
Nchi hii imekuwa kama pori la mbwamwitu!
 
Kuna watu wana roho ya kinyama sana, lakini pia hii inatakiwa iwakumbushe wanaume wanapokuwa maeneo wakiburudika, wajue kwa kiasi kikubwa wanashiriki uovu mwingine asioujua
 
Hii taarifa inalazimu tuulize mambo mawili muhimu:

1. Jeshi la Polisi limeanzisha dawati kwa ajili ya kushughulikia mambo yanayohusu jinsia-hasa wanawake. Kuna hela za wafadhili zimetumika kutoa mafunzo na siku chache zilizopita, Naibu katibu mkuu- wizara ya Mambo ya ndani ya nchi alikuwa anafunga mafunzo ya haya haya mambo ya polisi na jinsia.

Lakini kwa taarifa hii inashangaza kuona polisi wanambaka 'victim' na mbaya zaidi, hata askari wa kike wanakuwa kikwazo kwa huyu victim! Kuna umuhimu gani wa kuwa na hilo dawati?

2. Tuna wizara (kamili) inahusika na mambo ya jinsia na watoto na waziri wake ni Mh Sophia Simba. Siyo ni waziri, pia Mama Simba ndiye mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa CCM. Siku zote nimekuwa nahoji kazi za hii wizara, na namna inavyomsaidia mwanamke wa Tanzania. Kuna taarifa za kushtusha sana zimekuwa zinatolewa na vyombo vya habari lakini Wizara ni kama haiguswi kabisa.

Hivi kwanini wawanake wa Tanzania wanalipa kodi ili iendeshe wizara ikiwemo hii anayoongoza Sophia Simba? Wanapata nini in-return? Huyu binti aliyegeuzwa sex-slave kwa miaka 10 amepata msaada gani toka kwenye Wizara hii?
 
Hii taarifa inalazimu tuulize mambo mawili muhimu:

1. Jeshi la Polisi limeanzisha dawati kwa ajili ya kushughulikia mambo yanayohusu jinsia-hasa wanawake. Kuna hela za wafadhili zimetumika kutoa mafunzo na siku chache zilizopita, Naibu katibu mkuu- wizara ya Mambo ya ndani ya nchi alikuwa anafunga mafunzo ya haya haya mambo ya polisi na jinsia.

Lakini kwa taarifa hii inashangaza kuona polisi wanambaka 'victim' na mbaya zaidi, hata askari wa kike wanakuwa kikwazo kwa huyu victim! Kuna umuhimu gani wa kuwa na hilo dawati?

2. Tuna wizara (kamili) inahusika na mambo ya jinsia na watoto na waziri wake ni Mh Sophia Simba. Siyo ni waziri, pia Mama Simba ndiye mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa CCM. Siku zote nimekuwa nahoji kazi za hii wizara, na namna inavyomsaidia mwanamke wa Tanzania. Kuna taarifa za kushtusha sana zimekuwa zinatolewa na vyombo vya habari lakini Wizara ni kama haiguswi kabisa.

Hivi kwanini wawanake wa Tanzania wanalipa kodi ili iendeshe wizara ikiwemo hii anayoongoza Sophia Simba? Wanapata nini in-return? Huyu binti aliyegeuzwa sex-slave kwa miaka 10 amepata msaada gani toka kwenye Wizara hii?

Hayo ni mambo muhimu ya kujiuliza, mada hii imenitia uchungu sana
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Sidhani kama Baba Mtu anaweza kuja kwenye Wanawake wa hadhi ya chini kiasi hicho.

Ila waweza kukuta kwamba, huyo Mama Dangulo ni mtu wao wa karibu sana ndani ya CCM na hawa watu wanalindana sana. Huwezi kumgusa labda hawa watu wa Haki za Akina mama walivalie njuga hili swala na kumuumbua ndipo watakapomtosa na kujifanya hawafahamiani kabisa maana kwenye Siasa si hakuna Urafiki/Uadui wa Milele?
Labda baba mwanasha alikuwemo ndani au shemeji yake said alikuwa anabanjuaka humo..
 
Kwa maovu haya kuna siku Mungu ataagiza kile kimondo ambacho kiko karibu na dunia ambacho kina uwezo wa kuteketeza kilomita za mraba 562,500 kiangukie Tanzania na sijui nani atabaki, Ninawaomaba jamani tendeni haki hili tuweze kuepuka hasira ya Mungu.
 
Hata mi nampongeza sana Romana kwa kazi nzuri. Ingawa wahariri wake hawana shukurani. Kazi tu kula mishiko kupitia kinachoitwa jukwaa la wahariri- TEF!!
 
Back
Top Bottom