Polisi wanafanya kazi katika misingi ya kimaadili?

prumpeti

JF-Expert Member
Feb 28, 2022
1,021
2,279
Habari! natumaini ni wazima wa afya.

Kumekuwa na vitendo vinavyo leta maswali katika jamii ya watu walioelimika ukiachana na hawa wafata mkumbo ambao ndio wengi katika Taifa hili.

Je, polisi wanatekeleza majukumu yao katika misingi ya kimaadili?

Nimefuatilia kwa uchache tukio la ukamataji wa watu wanao shukiwa na majambazi huko serengeti kwa maelezo ya police mwenye mamlaka ya kuzungumzia tukio hilo anasema kwamba baada ya kuwakamatwa washukiwa watatu waliwataka kuwapeleka eneo ambalo wanaficha silaha wanazo tumia katika kutekeleza matukio ya kihalifu.

Wakati wakiwa njiani kuelekea huko washukiwa hao walileta vurumai za kutaka kutoroka ndipo police wakajihami na silaha ambapo ikapelekea kuwashambulia mpka kupelekea vifo vyao. Hapa kuna mambo kidogo yanaleta maswali.

Ukishatekeleza kitendo cha kumkamata mshukiwa lazima umfunge pingu ili kupunguza hatari za kutoroka au kukudhuru au hata kujidhuru mwenyewe.

Swali ni:

1. Washukiwa hao waliwezaje kutoroka au kujaribu kutoroka wakiwa wamefugwa?

2. Ni silaha gani ambazo washukiwa hao walikuwa nazo ambazo zilifanya police kuchukua tahadhari kiasi cha kufyetua risasi?

Haya ni baadhi ya maswali kulingana na matukio ya washukiwa kufia mikononi mwa police maswali ni mengi.

Ni wakati sasa kuwepo na chombo cha kusimamia na kukagua utekelezwaji wa majukumu ya askari hawa vinginevyo tunarudi tulipotoka.
 
Back
Top Bottom