Kalunguine
JF-Expert Member
- Jul 27, 2010
- 2,543
- 134
now nimejua kwa nini wanafunzi walicharuka, shule ipo umbali wa mita100 kutoka highway, wanafunzi walianza andamana kuelekea barabarani kushinikiza yajengwe matuta baada ya mwenzao kugongwa vibaya na bus la alsaedy jumamosi. wakiwa nanaelekea barabarani kuna mwanafunzi alikuwa mstari wa mbele huku akipiga ngoma ya band ya shule, polisi walivyofika wakaanza kumnyang'anya ngoma, katika purukushani mmoja akatoa bastola na kumpiga begani. hivyo ikaamsha hasira kwa wanafunzi wote hata wakaanza piga mawe magari yasiyowahusu.dereva alimgonga huyo mwanafunzi baada ya kupanua barabara. older post;nimepita maeneo ya mbezi kwa yusuph muda sio mrefu, polisi wapo wakitawanya wanafunzi wa mbezi high school kwa risasi baada ya wanafunzi hao kufunga barabara kwa muda kadhaa. inasemekana kuna mwanafunzi aligongwa hapo, sasa wanahitaji barabara iwekewe matuta kurahisisha wanafunzi kuvuka barabara. wanafunzi nao wapo kwa makundi wakirushia mawe na chupa magari yanayopita eneo hili huku wengine wakikimbia baada ya kuumia.note, nimelazimika update habari baada ya kupata info zaidi.