Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,174
Marehemu Steven Kanumba
Polisi wetu wameonyesha ukilaza wao kumkamata Lulu ambaye alikwenda kuwaarifu ya kuwa mpenzi wake amedondoka na kufa mwenyewe. Polisi wenye mafunzo stahiki walipaswa kutoa PF, kurekodi kauli za wahusika na kuchukua contacts zao na kuwaruhusu waondoke wakisubiria taarifa ya ukaguzi wa mwili wa mwendazake................................
Kitendo cha polisi kumkamata na kumhusisha na mauaji Lulu ni kumnyang'anya haki zake za asili na za kikatiba za kuwa hana kosa hadi pale atakaposhitakiwa na kosa..................polisi wamemkamata huku hawana ushahidi wowote kuwa kanumba aliuawa na kuwa hiyo ni kesi ya murder na kauli ya kamanda wa polisi aliedai kuwa Lulu atashitakiwa kwa mauaji inathibitisha jinsi jeshi la polisi lisivyojua wajibu wake ndani ya polisi jamii................
katika mazingira ya namna hii nani atatoa taarifa kwa polisi wakati akijua ataanza kubughudhiwa..............na kushukiwa kuwa anahusika na mauaji wakati hakuna ushahidi wowote hadi sasa wa kufanya hivyo.........mtoto wa watu kakoseshwa kula Easter yake kwa sababu ya uzembe na umbumbu wa polisi wetu................kweli tunakazi ya kuwalisha hawa vilaza polisi na familia zao kwa kutubughudhi tu!
Pili, hakuna maelezo kwa nini mdogo wake wa Kanumba - Seth - naye hakukamatwa pia kutokana na maelezo yake mwenyewe kuwa siku nzima alikuwa na kaka yake kabla ya Lulu kuja...................mashaka kama yanaweza kutiliwa kwa Lulu kwa nini watu wote waliokuwapo wakati marehemu yupo hai wasichukuliwe kama ni watuhumiwa bali mdogo wake aonekane hana hatia kama siyo ubaguzi wa kijinsia? kauli ya polisi kuwa ni ugomvi wa kimapenzi ndiyo uliomwuuwa unazidi kulidhalilisha jeshi la polisi kwa kufikia hatma ya swala lenyewe hata kabla ya kusubiri maelekezo ya taarifa za kitabibu...............kutoka Muhimbili.......hii sasa ni aibu kwa jeshi la polisi....................na yaonyesha kuna watu wengi wamefungwa kutokana na huu uzembe wa kufikiri wa polisi wwetu........
.............katika khali ya kawaida Lulu alitaka kuishia lakini ni mwendazake ambaye alikuwa anamzuia na yaonekana alikuwa ana nguvu zaidi ya kumzuia pale alipoweza kumrudisha chumbani na kufunga mlango wa chumba..........................watu hudondoka tu kwa viungo ndani ya miili ayo kushindwa kutekeleza majukumu yake..........viungo hivyo ni kama moyo, maini, figo, bandama n.k na hata ubongo waweza kushindwa kufanya kazi na mtu akadondoka chini na kupata majeraha ambayo mbumbumbu wetu wa polisi hawana zana za upembuzi yakinifu hata kusema hakuna kesi ya aina yoyote ile hadi pale watakapopata taarifa ya post-mortem kutoka kwa madaktari Muhimbili.................................
polisi wamwachie binti akale sikuukuu au vinginevyo wajiandae kumfidia kwa usumbufu na udhalilishaji waliomsababishia...................