Polisi wamwachie Lulu mara moja................ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wamwachie Lulu mara moja................

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Apr 8, 2012.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Apr 8, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 418,988
  Trophy Points: 280
  [​IMG][​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  Marehemu Steven Kanumba


  Polisi wetu wameonyesha ukilaza wao kumkamata Lulu ambaye alikwenda kuwaarifu ya kuwa mpenzi wake amedondoka na kufa mwenyewe. Polisi wenye mafunzo stahiki walipaswa kutoa PF, kurekodi kauli za wahusika na kuchukua contacts zao na kuwaruhusu waondoke wakisubiria taarifa ya ukaguzi wa mwili wa mwendazake................................

  Kitendo cha polisi kumkamata na kumhusisha na mauaji Lulu ni kumnyang'anya haki zake za asili na za kikatiba za kuwa hana kosa hadi pale atakaposhitakiwa na kosa..................polisi wamemkamata huku hawana ushahidi wowote kuwa kanumba aliuawa na kuwa hiyo ni kesi ya murder na kauli ya kamanda wa polisi aliedai kuwa Lulu atashitakiwa kwa mauaji inathibitisha jinsi jeshi la polisi lisivyojua wajibu wake ndani ya polisi jamii................

  katika mazingira ya namna hii nani atatoa taarifa kwa polisi wakati akijua ataanza kubughudhiwa..............na kushukiwa kuwa anahusika na mauaji wakati hakuna ushahidi wowote hadi sasa wa kufanya hivyo.........mtoto wa watu kakoseshwa kula Easter yake kwa sababu ya uzembe na umbumbu wa polisi wetu................kweli tunakazi ya kuwalisha hawa vilaza polisi na familia zao kwa kutubughudhi tu!

  Pili, hakuna maelezo kwa nini mdogo wake wa Kanumba - Seth - naye hakukamatwa pia kutokana na maelezo yake mwenyewe kuwa siku nzima alikuwa na kaka yake kabla ya Lulu kuja
  ...................mashaka kama yanaweza kutiliwa kwa Lulu kwa nini watu wote waliokuwapo wakati marehemu yupo hai wasichukuliwe kama ni watuhumiwa bali mdogo wake aonekane hana hatia kama siyo ubaguzi wa kijinsia? kauli ya polisi kuwa ni ugomvi wa kimapenzi ndiyo uliomwuuwa unazidi kulidhalilisha jeshi la polisi kwa kufikia hatma ya swala lenyewe hata kabla ya kusubiri maelekezo ya taarifa za kitabibu...............kutoka Muhimbili.......hii sasa ni aibu kwa jeshi la polisi....................na yaonyesha kuna watu wengi wamefungwa kutokana na huu uzembe wa kufikiri wa polisi wwetu........


  .............katika khali ya kawaida Lulu alitaka kuishia lakini ni mwendazake ambaye alikuwa anamzuia na yaonekana alikuwa ana nguvu zaidi ya kumzuia pale alipoweza kumrudisha chumbani na kufunga mlango wa chumba..........................watu hudondoka tu kwa viungo ndani ya miili ayo kushindwa kutekeleza majukumu yake..........viungo hivyo ni kama moyo, maini, figo, bandama n.k na hata ubongo waweza kushindwa kufanya kazi na mtu akadondoka chini na kupata majeraha ambayo mbumbumbu wetu wa polisi hawana zana za upembuzi yakinifu hata kusema hakuna kesi ya aina yoyote ile hadi pale watakapopata taarifa ya post-mortem kutoka kwa madaktari Muhimbili.................................

  polisi wamwachie binti akale sikuukuu au vinginevyo wajiandae kumfidia kwa usumbufu na udhalilishaji waliomsababishia...................
   
 2. StaffordKibona

  StaffordKibona JF-Expert Member

  #2
  Apr 8, 2012
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 671
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kama kuna ukweli ndani yake
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Apr 8, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 418,988
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  ni vyema wakamwacha binti wa watu akale sikukuu yake.....................mwuuaji huwezi kumjua kwenye mazingira haya bila ya afya ya kanumba kueleweka........hadi hivi sasa polisi hawana ushahidi wowote sasa kwa nini wahisi kuna mauaji?
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Apr 8, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Polisi gani? Hawa hawa wenye njaa na kiu ya mali?
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Apr 8, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 418,988
  Trophy Points: 280
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #6
  Apr 8, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  Kuna kila dalili ya Lulu kutopata fair trial.
   
 7. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #7
  Apr 8, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Hivi mkuu unaonge kwa kufuata sheria ama unaongea kwa matakwa yako binafsi?

  nadhani unaelewa kuwa Tanzania nzima inaelewa kuwa Lulu ndie aliyekuwa na marehemu hadi dakika za mwisho hilo halina ubishi,hata kama Lulu hausiki na kifo hicho ni lazima awekwe ndani hii ni kwa ajiri ya usalama wa Lulu mwenyewe

  kwani kanumba alikuwa na washabiki wengi na ana ndugu ambao wameondokewa na mpendwa wao,kwa hiyo kama itatokea polisi wakamwachia Lulu na akashambuliwa na kupoteza maisha yake watu wa kwanza wa kulaumiwa ni polisi,kwa hiyo polisi wanafanya kazi zao kwa kufuata sheria,taratibu na kanuni

  la sivyo wewe kama wewe uwe mlinzi wa Lulu CHOCHOTE kitakachotokea juu yake wewe ndie utakae husika

  kukamatwa kwa lulu ni kwa usalama wake,ingawaje mashitaka pia yatakuja baada ya uchunguzi
   
 8. r

  royna JF-Expert Member

  #8
  Apr 8, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 481
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Jamani wana JF naombeni mnisaidie kunitumia picha y Lulu
   
 9. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #9
  Apr 8, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,932
  Likes Received: 2,081
  Trophy Points: 280
  Pamoja na kuwa nakubaliana na wewe juu ya uwezo (duni) wa polisi wetu...lakini katika hili la wao 'kumshikilia' Lulu kuhusiana na kifo cha Sk sikubaliani na wewe. Kuna utata mkubwa bado juu ya chanzo cha kifo cha SK...amejiuwa, amekufa, ameuwawa! Kwa maelezo yaliyopo kwenye public mpaka sasa ni kuwa Lulu ndiye aliyekuwa na marehemu na kwa mujibu wa mashahidi (mdogo wa marehemu na majirani) kulisikika 'vishindo' chumba ambacho wapenzi hawa walikuwamo kabla ya SK kufariki. Sasa, katika hali kama hii Lulu ni shahidi muhimu (hasa kama itathibitika kuwa SK ameuwawa) sana katika uchunguzi wa kipolisi na pengine hata ule wa kitabibu. Kuwa wa kwanza kutoa taarifa polisi hakuondoi ukweli kuwa katika hili Lulu anabaki kuwa mshukiwa nambari moja. Baada ya uchunguzi wa awali bila ya shaka anaweza kuachiwa au wakaongezeka wengine.
   
 10. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #10
  Apr 8, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 710
  Trophy Points: 280
  Kama mtu hujui kanuni, taratibu na sheria usianzishe uzi kwa hisia zako binafsi au kijionyesha kuwa una kereketwa saaaana na maisha ya huyo Lulu, we kwa akili yako kwa tukio kama lililotokea ulitarajia Lulu asihusishe hata katika upelelezi kwa maana ya kuisaidia polisi? Kwa hali hiyo lazima awepo chini ya ulinzi kama mtuhumiwa na ikionekana hana hatia na anaona ameonewa basi ana haki ya kulifungulia jeshi mashtaka.
   
 11. Shakazulu

  Shakazulu JF-Expert Member

  #11
  Apr 8, 2012
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 940
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Ghafla kila mtu amekuwa mtaalamu wa sheria na mambo ya upelelezi. Haya ngoja tusubiri tuone hatma yake!!!
   
 12. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #12
  Apr 8, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Yes especially kwenye nchi inayoendesha maamuzi yake kwa kuangalia watu wanasema nini kwenye luninga. Hivi hatuna watu wenye uwezo wa kutumbukia chini ya kila jambo na kutafuta facts ili haki iwe inatendeka? Kila kitu ni magumashi magumashi tu.
   
 13. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #13
  Apr 8, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 418,988
  Trophy Points: 280
  crime scene is contaminated pale ambapo dakitari aliruhusu mwili uondolewe kabla ya polisi kufika na dakitari wala Seth hawakamatwi.....................waombelezaji akiwemo JK wameshiriki kwenda kuvuruga ushahidi kutokana na polisi kutolifunga eneo la crime scene ............sasa Lulu atatendewa haki kweli?
   
 14. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #14
  Apr 8, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  Halafu kuna kamanda wa polisi kanukuliwa akisema uchunguzi ukikamilika watamshitaki Lulu na kosa la mauaji!! SMH
   
 15. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #15
  Apr 8, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,547
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  umeongea point mkuu
   
 16. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #16
  Apr 8, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 418,988
  Trophy Points: 280
  Jeshi la polisi ni la kufuta tujipange upya................kama wao wanaona ana kesi ya kujibu hata kabla ya kupata post-mportem report na crime scene is such contaminated basi tumekwisha kabisa nchi hii. Sijui hata hiyo mishahara tunawalipia ya nini...........
   
 17. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #17
  Apr 8, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 418,988
  Trophy Points: 280
  watoke wapi na ajira zenyewe ni kujuana tu....................na mafunzo yao ni kule Moshi kunywa supu tu.................hakuna forensic science kule ya kuzama kwenye maeneo mazito kama hili.......mara nyingi huona polisi wakibeba mzoga wa mtu aliyekufa bila hata ya kuvaa gloves na wala hawaandamani na dakitari..............bila hata ya kuchukua ushahidi kwenye eneo la tukio au hata kulifunga kuzuia ushahidi usiharibike..........
   
 18. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #18
  Apr 8, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Nadhani kuwekwa ndani kwa lulu ni kwa usalama wake,hata kama ana hatia ama hana hatia.
   
 19. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #19
  Apr 8, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 418,988
  Trophy Points: 280
  Angalia CI nawe utajifunza hakuna cha ughalfa hapa.....................jifunze na utaelimika
   
 20. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #20
  Apr 8, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  jamani nyie hivi angekuwa kanumba ni mwanao ungependa kusikia prime suspect yupo free walah angekuwa mwanangu na lulu akaachiwa ingekuwa ama zangu ama zake,aliyekufa hapa ni mtoto wa m2,kwa kweli akae 2 ndani mpaka uchunguzi ukamilike,
   
Loading...