Polisi wamsaka mbunge CHADEMA kwa kufunga ofisi

Polisi wamsaka mbunge CHADEMA kwa kufunga ofisi

Arusha.Polisi Mkoa wa Manyara inamsaka Mbunge wa Viti wa Mkoa wa Manyara (CHADEMA),Rose Kamili pamoja na watu wengine wanne kwa tuhuma za kufunga ofisi ya kijiji cha Basotu kwa zaidi ya wiki moja sasa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Akili Mpwapwa alisema jana kuwa wanamsaka mbunge huyo,pamoja na wenzake ili watowe maelezo kuhusiana na tukio hilo kabla ya kufikishwa mahakamana.

Mbunge Kamili alipoulizwa jana kuhusiana na kusakwa huko, alikiri kupata taarifa lakini akasema,kama polisi wanamuhitaji wamfuate nyumbani kwani wanapajua.

Hata hivyo, alisema uamuzi wa kufungwa ofisi hiyo, yalitolewa kwenye mkutano wa mkuu wa kijiji,kutokana na kupinga unyanyasaji wa viongozi wa kijiji, kutosoma mapato na matumizi tangu mwaka 2007 na pia kuwataka wafike Basotu viongozi wa wilaya.

Wananchi 365 walioshiriki mkutano mkuu huo wa kijiji, licha ya kufunga ofisi hiyo pia walichagua vijana waliopitia mafunzo ya mgambo kulinda ofisi hizo hadi muafaka utakapopatikana.

CHADEMA tumieni busara msije chafua amani ya nchi!

CCM acheni kutumia vibaya madaraka na rasilimali za nchi msije chafua amani ya nchi.
 
Waje wamchukue tu kama kweli wana la kuongea zisije kuwa wamepata habari za kiintelegensia kutoka policcm.
 
Wanamtafuta kwa lipi kama kweli ni mkutano mkuu wa kijiji ndio uliotoa maamuzi ya kufunga hizo ofisi na sababu ya kufanya hivyo iko wazi ni kwamba mapato na matumizi hayajasomwa tangu 2007 hadi sasa 2013 more than six years, balaa tupu.

Hapa utaona jinsi gani CCM inavyokumbatia uovu, kwao watenda maovu kwao ndio watu wema. Haingii akilini kusadikishwa kwamba mtu mmoja eti Rose Kamili mbuge wa viti maalumu anaweza kufunga ofisi ya kijiji, hapa utaona ni jinsi gani kodi za wananchi zinatumiwa ovyo, maana badala ya polisi kufanya majukumu mengine wanaambiwa wakamwinde na kumkamata Mh mbunge na kuandaa mashitaka dhidi yake, upuuzi mtupu na ni wastage of time.

Sifa za kijinga zitaimaliza hii nchi
 

CHADEMA tumieni busara msije chafua amani ya nchi!
Tumeona busara za CCM juu ya; Meremeta, Richmond,mabilioni yaliyoko uswiss, kwa Dr Ulimboka,kwa Kubanda,kusafirisha maliasili zetu kwenda nje ya nchi, gharama kubwa za ujenzi wa mbomba la kusafirishia mafuta Mtwara mpaka dar......hivyo hatuuhitaji tena huo upumbavu wenu...
 
Kuna siku walisema wanamtafuta Mbowe kwa siku mbili, wakati mbowe simu zake zote zinapatikana, hawajafika kwenye ofisi ya mkoa ambapo kama yuko Arusha ndiyo ofisi anakopatikana, hawakuenda kwenye hotel aliyokuwa amefikia sasa nikajiuliza wanatumia jia gani kumtafuta, hivi mtu kama mbowe akiwa hapa Arusha una weza kutumia saa ngapi kumpata au ni kuchafuana tu...
Ecoutez moi ça;5869951 said:
Hawa jamaa siwangewasiliana nae akaenda mwenyewe!!!
 
Ni masikitiko makubwa polisi mkoani manyara kwa kuwasaka wachangiaji wa hoja katika mikutano yao mikuu ya kijiji baada ya kuwashinda watendaji wa vijiji kwa hoja.na ni jambo la kushangaza kwa polisi kuwasaka na kuwakamta wananchi wanaodai haki yako ya kimsingi na kuwawajibisha watendaji wasiowaadilifu na wezi katika mkutano mkuu maalumu wa kijiji cha bassotu wilaya ya hanang wananchi walikuwa wandai mambo yafuatayo 1.taarifa ya mapato na matumizi tangu mwaka 2007.2.kutokushirikishwa katika matumizi bora ya ardhi na rasilimali yao .watu kukamatwa ovyo na kunyanganywa mali zao.3.kuvunjiwa ngalawa na mtendaji polisi na mkt.mkurugenzi kutishia wjumbe wa mkutano mkuu na mkuu wa wilaya kutishia na kuleta polisi na silaha je huo ni uungwana mbona ni utawala wa kimabavu.wananchi walichoka na kuazimia kufunga ofisi yao ya kijiji.tangu serikali kuchaguliwa hakuna maendeleo yeyote wala hakuna ujezi wa shule.wanafunzi wanabanana hakuna vyumba wala nyumba za waalimu.hakuna madawati.wananchi wanadai hela za minara ya simu na shamba la kijiji mapato ya ziwa yote hiyo zimeliwa na mtendaji wa kijiji na mkt wake.wananchiwalidai taarifa ya ukaguzi hawakupata tangu mwaka 2005.na mkurugenzi amepuuzia wala hataki kusaidia wananchi wanapata vitisho toka jeshi la poilisi na mkuu wa wilaya .watanzania sasa tuwakomboe wenzetu ili watumie haki yao ya kikatiba.napenda kuwaambia polisi wazingatie haki ya kikatiba ya kila mwananchi ibara ya 18 na ibara ya 8 na ibara 24.kama hawasomi wapewe semina aidha wajue majukumu na madaraka ya mikutano mikuu na wajibu wa mwananchi ktk kuwawajibisha viongozi wao.acheni uonevu mtu wa kukamatwa ni watuhumiwa mtendaji wa kijiji na mkt na mkurugenzi mtendaji .msipofanya hivyo hamjui utawala bora na demokrasia
 
mkurugenzi kudai hawezi kuhudhuria mkutano wa kijiji kwakushinikiza ofisi kufunguliwa .je huo ndio utawala bora na kudai ofisi ni yake je amejenga yeye na wakati huo ni michango yetu na kodi zetu.mwamie asome katiba kuwa yeye anatakiwa awajibike kwa wananchi kwakuwa ndio mwajiri wake na analipwa kwakodi ya wananchi hao hanang siyo shamba la bibi madiwani acheni kulala chapa kazi tunawapima majibu mwaka 2015

 
Tunashukuru kwa Taarifa maana tulikuwa hatujui nguvu ya umma inavyofanya kazi katika kijiji hicho.
 
ofisi ya kijiji hiwezi kufungwa mtu mmoja tuache upumbavu huo ni uamuzi ya wengi mtu mmoja hawezi kuamrisha umati zaidi ya watu 600 huo ni uwazimu acheni kuwa na mambo yakipuuzi fanyeni uchunguzi bila upendeleo wa upande wowote zingatieni uaminifu na sheria na usawa.washughulikieni hao wahalifu wanaokula mali za wananchi
 
Hapo hao mapolisi wanapaswa kwanza kupitia sheria za serikali za mitaa kabla hawajaumbuka kwa kuumbuka.
 
napenda kueleza ukweli kuwa watu wanaotafutwa ni mwenyekiti wa muda aliyechaguliwa katka kikao hicho baada ya mwenyekiti kuutelekeza mkutano wa kijiji ambao ulikuwa endelefu na kumhitaji mkurugenzi baada ya mkt kushindwa kujibu hoja za wananchi wajumbe baada ya kuhojiwa nani au mkutano upi uliruhusu kuchukua mashamba ya wanakijiji na kudai hajui na mambo mengine mengi baada ya viongozi hao kuutelekeza kikao hicho zaidi ya masaa matatu3 wananchi wakamchagua mkt ramadhani ghamunga kuwa mkt wa kikao hicho na elihuruma kuwa katibu wa kikao hicho,la kushangazwa viongozi hao walikamatwa na kupelekwa kituo cha polisi katesh na kuachiliwa kwa mdhamana.je huo ni utawala bora au uonevu tu je nini maana ya mkutano mkuu na wajibu wa mwananchi na madaraka ya mikutano mikuu mkurugezi anafanya kazi akiwa ofisini hawatembelei wananchi wenye madai halali na wenye kudai haki zao.wananchi wengine ni wenyeviti wa vitongoji ya bassotu a na laja ambao nao walikamatwa na kupelekwa polisi katesh na wapo nje kwa dhamana.na wengine ni wenye hoja nzito katika vikao kama wajumbe halali ndg.onesmo na antemi nao walikamatwa na wako nje kwa dhamana je huo ndio utawala bora na wa sheri watanzania wasaidieni wananchi na kuwapa elimu na watu haki za bainadamu haki ardhi waje kwa haraka kijiji cha bassotu hukuwafuasi wa ccm wanaweka shinikizo na mhe nagu anavitumia vyombo vya dola tusaidie wakazi hao hapo kuna chuki kubwa sana polisi nao wamekuwa wanasiasa hapa wilaya ya hanang na mkoa wa manyara
 
Badala ya kusaka wahalifu...wanambwelambwela na mambo ya siasa..nyambafu zenu policcm
 
mkutano mkuu ndio wenye uwezo wa kuwondoa madarakani viongozi wa kijiji na mkt wao.na ndio kikao cha juusana katika kijiiji.na ni kama bunge na kwenye ktiba wananchi ndio wanaowaweka madarakani na viongozi huwajibika kwa wananchi,kama wanauwezo wa kuwaweka basi wanauwezo wa kuwaondoa asante
soma katiba .na kitabu cha utawala bora ukitaka kwa undani tutawawelimisha juu ya sheria pia kuna haki za binadanuu
 
polisi acheni uonevu waacheni wananchi waendelee na vikao vyao
 
Zinasemaje???

Mkuu pitia moja wapo ni kwamba afisa mtendaji anapaswa kubandika mapato na matumizi ubaoni kila mwezi akishindwa kufanya hivyo kwa miezi 3 mfululizo wananchi wanayo haki ya kuitisha mkutano mkuu na kupata saini 60+ za wananchi na kuung'oa uongozi
 
MAFILILI kwa nini hamtaki kusoma taarifa ya matumizi na mapato??

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom