Polisi wamsaka mbunge CHADEMA kwa kufunga ofisi

Polisi wamsaka mbunge CHADEMA kwa kufunga ofisi

MAFILILI

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2011
Posts
2,377
Reaction score
1,200
Arusha.Polisi Mkoa wa Manyara inamsaka Mbunge wa Viti wa Mkoa wa Manyara (CHADEMA),Rose Kamili pamoja na watu wengine wanne kwa tuhuma za kufunga ofisi ya kijiji cha Basotu kwa zaidi ya wiki moja sasa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Akili Mpwapwa alisema jana kuwa wanamsaka mbunge huyo,pamoja na wenzake ili watowe maelezo kuhusiana na tukio hilo kabla ya kufikishwa mahakamana.

Mbunge Kamili alipoulizwa jana kuhusiana na kusakwa huko, alikiri kupata taarifa lakini akasema,kama polisi wanamuhitaji wamfuate nyumbani kwani wanapajua.

Hata hivyo, alisema uamuzi wa kufungwa ofisi hiyo, yalitolewa kwenye mkutano wa mkuu wa kijiji,kutokana na kupinga unyanyasaji wa viongozi wa kijiji, kutosoma mapato na matumizi tangu mwaka 2007 na pia kuwataka wafike Basotu viongozi wa wilaya.

Wananchi 365 walioshiriki mkutano mkuu huo wa kijiji, licha ya kufunga ofisi hiyo pia walichagua vijana waliopitia mafunzo ya mgambo kulinda ofisi hizo hadi muafaka utakapopatikana.

CHADEMA tumieni busara msije chafua amani ya nchi!
 
Nyie policcm acheni kufanya kazi kwa vimemo
 
Sasa polisi kwa nini huwa hawakamati madiwani na wabunge wa magamba wanaoondoka na ufunguo za ofisi zao kwa mwezi mzima.
 
Polisi wa Tz bwana?!!! Badala ya kufanya kazi kitaalamu ni publicity na siasa mingi. Yaani mtu kama mbunge anasakwaje? Amekuwa jambazi au muuaji ,?? Hamna simu yake? Jeshi la intelijensia. Hovyooooo!!!!!!!
 

Wananchi 365 walioshiriki mkutano mkuu huo wa kijiji, licha ya kufunga ofisi hiyo pia walichagua vijana waliopitia mafunzo ya mgambo kulinda ofisi hizo hadi muafaka utakapopatikana.

CHADEMA tumieni busara msije chafua amani ya nchi!

Sasa unaanza kupata akili kidogo kidogo... At least umetambua siku hizi wanavijiji wote ni CHADEMA...
 
Mary Nagu mambo vip? kiboko yako nao unataka kumtia BP/Ndani mbunge mtaraji wa hanang 2015........
 
Unajua hii wewe Power.jpeg
 
Chadema hakuna ubabaishaji,action hapo hapo.huyo mtendaji kafanya kijiji nyumba yake binafsi tangu 2007 hakuna taarifa, polisi wanamkumbatia
 
Kama wananchi kuwachukulia hatua viongozi wabadhilifu na wasio fuata sheria na taratibu za Nchi hii ni kuvuruga AMANI, yakubidi ukapimwe akili sio bure hata kidogo.
Hivi kwa akili yako fupi ianyozidi kudhoofishwa na unazi kwa chama chako bila haya, anayestahili kutafutwa na kutiwa lupango ni nani hapo?
HEBU JARIBU KUWA MZALENDO KIDOGO.
 
Wanatafuta kumukamata mlalamikaji na muathirika badala ya kumkamata mtuhumiwa anae zorotesha maendeleo ya kijiji.tutafika kweli kama mlalamikaji anatafutwa ili apelekwe mahakamani baadala ya kusikilizwa na kupewa msaada hata kama amekosea njia ya kufikisha malalamiko yake si asikilizwe na kuelekezwa njia sahihi ya kuwakirisha malalamiko yake badala ya kuanza kumutishia kumpeleka mahakamani.
 
Back
Top Bottom