Polisi wamnasa muuza dawa za kulevya wa kimataifa aitwaye Leila... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi wamnasa muuza dawa za kulevya wa kimataifa aitwaye Leila...

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by nngu007, Jun 7, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Monday, 06 June 2011 21:03

  Fidelis Butahe
  JESHI la polisi nchini limewakamata watu wanane wakiwa na dawa za kulevya aina ya cocaine huku mmoja wa watuhumiwa hao, Mwanaidi Mfundo anayejulikana pia kwa jina la Naima Mohammed Nyakiniwa au Mama Leila aliyetajwa pia na Rais Barack Obama wa Marekani kama mtu hatari kwa biashara hiyo.

  Kwa mujibu wa polisi, Leila ambaye ni raia wa Kenya amekatwa nyumbani kwake Mbezi Beach, Dar es Salaam akiwa na wenzake saba. Alikutwa na hati sita za kusafiria zikiwa na sura tofauti tofauti.Wiki iliyopita Rais Obama alitangaza watuhumiwa saba wa biashara ya dawa za kulevya waosakwa zaidi ambao wamezuiliwa kuingia Marekani.

  Kwa mujibu wa gazeti dada la Mwananchi, Daily Nation la Kenya, Mwanaidi ambaye ni mama wa mabinti watatu, waliokulia eneo la majengo lenye historia ya uhalifu na ufuska, ana makazi mengine katika eneo la matajiri la Kitisuru, jirani na makazi ya matajiri ya Westlands, Nairobi.
  Gazeti hilo lilieleza pia kwamba Nyakiniwa alitajwa kuwa miongoni mwa vigogo wa dawa za kulevya wa kimataifa na Rais Obama Jumatano iliyopita kwenye Baraza la Congress. Pia katika orodha hiyo walitajwa Mbunge wa Kilome, John Haroun Mwau, mwenye biashara za aina mbalimbali nchini Kenya.

  Kwa mujibu wa Wizara ya Fedha ya Marekani, Mama Leila anashughulika na biashara ya dawa za kulevya aina mbalimbali ikiwamo heroin ambayo huisafirisha Kusini Magharibi mwa Asia na cocaine anayoisafirisha kwenda Amerika ya Kusini.
  Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Godfrey Nzowa alisema watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani Juni 3, mwaka huu.

  Pia Jeshi hilo limetoa orodha ya kiasi cha dawa za kulevya aina ya heroine na cocaine zilizokamatwa tangu mwaka jana na idadi ya dawa hizo kwa mwaka huu inazidi idadi ya mwaka jana.Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Nzowa alisema watuhumiwa hao walikamatwa na kikosi kazi cha udhibiti wa dawa za kulevya, Juni mosi, mwaka huu saa nane usiku huko Mbezi Beach.

  "Walikamatwa wakiwa na kilo tano za cocaine na lita 3 za chloroform. Wote wamefikishwa mahakamani, walikuwa katika harakati za kusafirisha kwa kuwa walikuwa wameshazifunga dawa hizo katika mifuko ya kahawa," alisema Nzowa.Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Antony Arthur na Ben Machania kutoka Kenya pamoja na Sarah Munuo, Almas Said, Yahya Haroun, Rajabu Mzome na Aisha Kungwi ambao wote ni Watanzania.

  Nzowa alisema Mfundo, maarufu kwa jina la Naima Mohammed Nyakiniwa ni mfanyabiashara wa kimataifa wa dawa za kulevya na kwamba alikuwa akisakwa na nchi mbalimbali duniani."Inawezekana walikuwa na kilo nyingi za dawa za kulevya ambazo walikuwa wameshazisafirisha, hizi dawa tulizozikamata zinaweza kuwa na thamani ya Sh200 milioni," alisema Nzowa.Alisema kuwa Mfundo pia alikutwa na hati sita za kusafiria ambazo zilikuwa na jina moja lakini sura tofauti: "Sura zake sita tofauti ambazo zilikuwa katika hati hizo za kusafiria zilimfanya ashindwe kutambulika kirahisi katika nchi alizokuwa akienda," alisema Nzowa.

  Juni 3, watu watuhumiwa hao hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa shtaka la kuingiza nchini kilo tano za dawa za kulevya aina ya cocaine zenye thamani ya Sh225 milioni.

  Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Kisutu Mustapher Siyani, Wakili wa Serikali, Patrick Malogoi alidai kuwa Juni Mosi, mwaka huu maeneo ya Mbezi Beach washtakiwa hao kwa pamoja kinyume na kifungu cha 16 (1) b (i) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya sura ya 95 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2009, waliingiza nchini dawa hizo za kulevya.

  Baada ya kuwasomea shtaka hilo, Hakimu Siyani aliwataka washtakiwa hao kutojibu chochote kwa sababu Mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza shtaka linalowakabili hadi Mahakama Kuu ya Tanzania. Hakimu huyo aliiahirisha kesi hiyo hadi Juni 15, mwaka huu itakapotajwa tena.
  Kuhusu mapambano dhidi ya biashara ya dawa za kulevya tangu mwaka jana, polisi imesema wafanyabiashara wakubwa wa dawa za kulevya waliokamatwa tangu kipindi hicho wote ni raia wa kigeni.

  Nzowa alisema mwaka 2010, kilo 190 na gramu 780 za heroine zilikamatwa na washtakiwa walikuwa 496, wasafirishaji 10, watumiaji 480 na wafanyabisahara 12 huku watu sita wakikamatwa, wanne raia wa Iran na wawili wa Afrika Kusini.
  "Cocaine zilizokamatwa zilikuwa kilo 64 na gramu 966, washitakiwa walikuwa 528, wasafirishaji watatu, watumiaji 521. Waliokamatwa walikuwa watu wanne ambao ni raia wa Liberia, Guinea, Ghana na Msumbiji."

  Alisema bangi zilizokamatwa zilikuwa kilo 22,904 na gramu 905, watuhumiwa walikuwa 9,739, wasafirishaji 400, watumiaji 9,329 na wafanyabishara wakubwa 10 na kwamba ekari 296 za mashamba ya bangi yaliteketezwa huku watuhumiwa wanne wakikamatwa.
  Alisema mirungi iliyokamatwa ilikuwa kilo 10,317 na gramu 502 na watuhimiwa walikuwa 1,351, wasafirishaji 200, watumiaji 1,146 na wafanyabiashara wakubwa watano.

  Alisema mwaka 2011, dawa za kulevya aina ya heroin zilizokamatwa zilikuwa kilo 182 na gramu 402.39 na kwamba watuhumiwa walikuwa 1,080, wasafirishaji watatu, watumiaji 1,075 na wafanyabiashara wakubwa waliokamatwa walikuwa raia wawili wa Pakistani.
  Alisema Cocaine zilizokamatwa zilikuwa kilo 91 na gramu 906, watuhumiwa walikuwa 1,070, wasafirishaji 15, watumiaji 1,048.

  "Wafanyabiashara wakubwa waliokamatwa walikuwa saba, watatu Wakenya, wawili Wanigeria na wengine ni kutoka Pakistani na Afrika Kusini," alisema Nzowa na kuongeza:"Bangi zilizokamatwa ni kilo 17,257, watuhumiwa 1,000, wasafirishaji 20, watumiaji 970 na wafanyabiashara wakubwa 10. Mirungi iliyokamatwa ni kilo 15, watuhumiwa 40 na watumiaji 40."

  Awali, Nzowa alisema mwaka 2009, kilo 9 za dawa za kulevya aina ya heroine zilikamatwa na kwamba walioshtakiwa walikuwa watu 122, wasafirishaji watano na watumiaji 117."Cocaine zilikamatwa kilo nne, washtakiwa walikuwa 108, wasafirishaji wawili na watumiaji 106.
  Mirungi iliyokamatwa ilikuwa kilo 22,904, watuhumiwa waliokamatwa ni 365, wasafirishaji 20 na watumiaji 345. Bangi zilizokamatwa ni kilo 56,197, watuhumiwa 3382, wasafirishaji waliokamatwa walikuwa 200 ila watano ni raia wa Comoro na watumiaji walikuwa 3,182."
  Alisema kuwa ekari 79 ziliteketezwa na watuhumiwa wenye mashamba waliokamatwa walikuwa tisa.

  ** He identified the names used by the woman as Mwanaidi Ramadhan Mfumo, Nahima Nyakinywa and Mama Leila. According to Mr Nzowa, the woman was found in possession of six different permanent and temporary passports.

  The passports and her appearances have allegedly been protecting her from being noticed in various countries. She was nabbed on June 1, at around 2am with her accomplices, in possession of five kilogrammes of cocaine and three litres of Chloroform.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Sijui Viongozi wadini walimpa Leila hiyo Passpoti?
   
 3. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wakuu hivi hamchoki na lugha zenu chafu chafu kama hizi, why do we have to be talking of the same thing kila siku??????????
   
 4. H

  Haki JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2011
  Joined: Jan 14, 2009
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna mpango maalum wa US kuweka base ktk nchi za East Africa. Mpango huu ndiyo umeshaanza kwa njia ya kutumia kigezo cha madawa ya kulevya. JK katoa statement kuwaonya viongozi wa dini kwa sababu Obama na jeshi lake wakishaweka base yao hapa, hatoweza kuficha makucha ya wauza unga, kwa hiyo atawatosa vigogo wote kuanzia ktk dini mpaka CCM.
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kumbe unajua kuwa vigogo hao wamo ndani ya CCM?
   
 6. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #6
  Jun 7, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Amejivua ga.....!
   
 7. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #7
  Jun 7, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Ni kazi nzuri mmefanya jeshi la Polisi. Ongezeni kasi
   
 8. Nsiande

  Nsiande JF-Expert Member

  #8
  Jun 7, 2011
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 1,649
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kazi nzuri jeshi la polisi,

  Mheshimiwa JK list uliyopewa na A Chifupa na hiyo uliyo nayo unasubiri nini kuwatia nguvuni ? Funga wote hawa wanatuharibia taifa letu na lijalo usiogope mtu, this is ur last term, @least do sth credible!
   
 9. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #9
  Jun 7, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,159
  Trophy Points: 280
  kikwete si ana mimba, na hiyo ndiyo inayomfanya awe ,ropokaji
   
 10. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #10
  Jun 7, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ila huwa sisikii hukumu zake.....hasa kesi kubwa kama hiii ya mwanaidi
   
 11. serio

  serio JF-Expert Member

  #11
  Jun 7, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 5,925
  Likes Received: 1,133
  Trophy Points: 280
  aah, wapenda ujiko hao,.mpaka obama ataje?
   
 12. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #12
  Jun 7, 2011
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  HANA PICHA TUMJUE? aah ni maoni tu
   
 13. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #13
  Jun 7, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Mama Leila amekamatwa kwa zaidi ya wiki moja au mbili sasa. Me nashangaa sana media za Bongo. hazifuatiliii habari hadi RPC awaite awape kibahasha ndo wanaenda kuchukua habari. Hii habari nimeisoma magazeti ya Kenya wiki iliyopita nadhani kabla hata Obama hajamtangaza huyu mama.

  Polisi wa Bongo wanajikosha kutangaza sasa hivi baada ya Obama kumtangaza kuwa ni "Drug Kingpin". Mzee Nzowa mbona wengine huwa anawatangaza haraka haraka. Au alitaka kumuachia kwa kisingizio "tunaficha jina lake hadi hapo upelelezi utakapokamilika"? Vita ya madawa ya kulevya Tanzania ni utani wala serikali haiko makini. Inatupa wasiwasi isije ikawa vyama na wanasiasa wanakuwa sponsored na drug money. Hii itakuwa scandal kubwa ya karne Tanzania. Maana kama majina JK anayo,inakuaje hatuoni wakishughulikiwa? Au hatuna ushahidi? Kama hatuna ushahidi, kitengo cha upelelezi kivunjwe. Usalama wa Taifa unafanya kazi gani? Maana ni hatari kwa Taifa.

  Msumbiji kimetokea kioja mwaka jana. Rafiki wa karibu na mshirika mkubwa wa biashara wa Rais ndiyo kinara wa unga.
   
 14. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #14
  Jun 7, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Ile issue ya kupakiziwa mtoto wa mengi uwanja wa ndege iliishia wapi!Au tume haijamaliza kazi yake!
   
 15. Chakochangu

  Chakochangu JF-Expert Member

  #15
  Mar 13, 2016
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 2,197
  Likes Received: 1,268
  Trophy Points: 280
  Hivi huyu mama leila na hawa vijana wake aliokamatwa nao kesi yao iliishia wapi?
   
 16. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #16
  Mar 13, 2016
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  madawa ya kulevya
   
 17. savius

  savius JF-Expert Member

  #17
  Feb 8, 2017
  Joined: Oct 21, 2014
  Messages: 358
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 60
  makonda angechukua hata majina ya ma-don was ngada kwa huyu mama
   
Loading...