Polisi wakimbizana na Wamachinga Dar

kilichotakiwa sio kuondoa machinga wote,ilitakiwa wale ambao hawakuwa na shida wabaki wale ambao ilikuwa kero ndo watolewe,imangine unawapa watu siku 30 waondoke wakati wamechukua mkopo hapo unaenda kuua vikoba na taasisi za kukopesha,tusifurahie tuu!
Nani anakopesha machinga?
 
Msipotoshe....hakuna Biashara isiyo na mpangilio. Kwanini hawataki kwenda maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya biashara ya kimachinga?!
Ukiambiwa uachie cheo ulichonacho ofisini uhamishiwe stoo kwa mlinzi na wafanya usafi utakubali? Kwa maana yote still uko ofisini? Utaweza?
 
Ukiona fremu inapangishwa elfu 50 kwa mwezi ujue eneo hilo mzunguko hamna kabisa! Fremu za barabarani kama hivyo hata mitaani tu ni 100-200K
Naam ndio hivyo, uhalisia wa maisha, life is not perfect wote tungetaka mzunguko mtamu huenda tungerundikana Kariakoo.., ila sababu wants are unlimited na sources are scarce, prices ni moja ya mchujo..., yaani tunajichuja wenyewe bila kulalamika, vinginevyo tungesema wanaopata fremu Kariakoo wanapendelewa (lakini uzito wa pochi yako unakufanya mwenyewe uende pengine)

Kwahio ndio hapo akili inachemka unatafuta ni nini cha kufanya sehemu ya fremu ya elfu 50 na upate wateja (labda uwe mganga wa kienyeji) wabongo ni watu wa imani sana.... natumai hautalala njaa...

Anyway kwa ufupi kwa maoni yangu kuhamishana wala kubaki sio suluhisho, suluhisho la kudumu ni kupunguza uzalishaji wa hawa wachuuzi..., vinginevyo miaka kadhaa kutoka sasa tutakuwa tunaongea haya haya..., zile sehemu ambazo leo utasema hazina wateja zitakuwa zimejaa na watu kulalamika ni wapi wawasogeze hawa wachuuzi...
 
Kitu kimoja ninachopingana na wamachinga ninwao kukosa ustaraabu.yaana wanaweka meza mbele ya duka la mwingine.popote pale wao wanaweka biashara.Yaani ni watu wabinafsi kupita hata waendesha daladala.Nakubaliana na utaratibu wa kuwapanga upya.wapishe wenye freme zao wanaolipa kodi za mapato na kodi za fremu.wewe kweli unakaanga mihogo katikati ya posta,kweli?
 
Mkuu wa mkoa ameshatoa siku 12....haya wanayatoa wapi ?!!!

Wasituharibie mipango yetu.....

Siempre CCM
 
Hawa mwendazake aliwaendekeza sana.. sasa hao polisi mabomu hawana??
 
Kitendo cha kujigawa wa makundi mawili, moja linalotetea wamachinga na kutaka wabakie katika maeneo wanayofanya biashara sasa, na kundi la pili la wengine kutaka wamachinga wahamishe ni ishara kwamba hata kuwagawa wa Tanzania kwa fikra za uchumi itakuiwa rahisi sana.
Tujiulize, hao wamachinga wanapilichafua jiji, taifa linapata hasara gani,m kisha tujiulize hao wamachinga wakipelekwa wasipo pataka na taifa litapata faida gani ?
Je wafanya biashara walipoingiliwa na wamachinga , walipata hasara, tuseme kweli walipata hasara, je nani sasa wa kuja kuleta maridhiano kati ya wafanya biashara wenye maduka na wamachinga ?
 
Huyu jamaa sijui veepe anaogopa bomu la chinga wakati polisi wanaozui chadema wapo wengi kuliko wanaozui machinga
 
Mbona RC ameongeza muda kwa siku 12 mbele , mashambulizi ya Polisi na wamachinga Msimbazi ni ya nini , kwanini zisisubiriwe hizo siku 12 ?
Katika hili nakubali kutokubaliana na wewe! Hapo si unaona wamewashambulia viongozi wao wakati wanawapanga? Sasa tunataka polisi wafanye nini zaidi ya kutembeza kichapo? Hao jamaa ni wakorofi, watoke kwenye njia za waende kwa miguu bwana!
 
Back
Top Bottom