Polisi wakimbizana na Wamachinga Dar

Hawa wajasiriamali sio wastaarabu mtu mwenye akili zake timamu hawezi shabikia,Mtu anayepanga biashara kwenye njia ya watembea kwa miguu walivyo wa ajabu maganda ya miwa na machungwa wanatupa kwenye mitaro ya maji matokeo ikinyesha mvua maji yanaingia mitaani kati ya kumi ya chinga nina imani wawili tu ndio wenye vitambulisho vya ujasiria
 
Zile siku kumi 12 za nyongeza kumbe ilikuwa ni geresha? Naiomba serikali imalizane kiungwana na hawa mabwana..
Sasa kuongezewa siku 12 , ndio wengine walioishatoka wameanza kurudishia mabanda yao sehemu walizokuwa wameshaanza kutoka!!usipo kuwa mungwana nani atakuonyesha ungwana huo?
 
kwenye simu unaweka tozo za kufa mtu
mtaani unawafukuza vijana wasipate riziki

Hivi hii serikali inafikiria mara mbilimbili maamuzi yake?
Wapate lakini kwa utaratibu mzuri, bila kuwa kero kwa wengine!!huwezi kufanya biashara bila kulipa kodi, anayelipa kodi anashindwa kufanya biashara kutoka na vurugu zako!!
 
Sheria zifuatwe,haiwezekani kujiamulia tu.. Uhuru wako unao mipaka...
 
Wapinzani ni wanafiki mno
Nchi lazima iwe na mipango, haiwezekani kila sehemu watu waweke bidhaa
Kwahiyo wapinzani ndio waliwaambiwa wamachinga wafanye biashara kokote,huu upuuzi umeanza 2016 baada wa jpm kusema wasisumbuliwe
 
Hata huko unapoona nchi zilizoendelea za ulaya hao wanaofanya biashara mitaani wapo hila wanapangwa wasibughudhi wengine sio kisingizio cha ajira mpk mzibe njia za watembea kwa miguu mtu inabidi apite barabarani kupishana na magari njia ya kutembelea imejengwa mabanda
Kuziba njia ni tatizo lililoletwa na marehemu
 
Service road siyo maeneo ya biashara
Walianza lini kukaa kwenye service road? Kwanini Machinga Complex ilibaki tupu? Kwanini hawaendi Mawasiliano, wanarudi pembezoni mwa Tanesco Power station? Karume lilifutiliwa mbali hata kuchomwa moto, ni lini lilianza soko la Karume, lini lilipaswa kuhama, na je tayari limeshahamia pale Complex ambapo ni pua na mdomo?
 
Machinga wasipate taabu wasambae kwenye miji mingine tanzania wakaichangamshe na kuikuza kibiashara waachane na hilo jiji linalowanyanyasa
 
Back
Top Bottom