Bufa
JF-Expert Member
- Mar 31, 2012
- 10,656
- 21,083
Yaani nanunua dhahabu Nyarugusu ili nikauze Huko Swiss alafu nimwambie yule mchimbaji aniuzie sawa na soko la Dunia ? Hapo takuwa nafanya Biashara au ninafanya kubalidilisha Pesa, na nikishaipata hio dhahabu mimi nakwenda kuwauzia wale duniani kwa bei gani ?
Ipo hivi:
Nunua dhahabu Nyarugusu kwa wachimbaji wadogo walalie aidha kwa njaa zao au ujinga wao.
Au nunua dhahabu Nyarugusu ongeza purity ndo peleka nje ili upate faida.
Au chimba mwenyewe bana matumizi kwenye uchimbaji ili bdae ukiuza upate faida
Au nunua dhahabu, kama una leseni, kisha itunze hadi bei ya dhahabu ikipanda ndo iuze ili upate faida. Bei ya dhahabu inabadilika kila siku kama hisa.
Nje ya hapo bei ya dhahabu yenye purity sawa haipishani sana toka eneo moja hadi lingine duniani kote.
Ingia online search gold price leo TZ na New York ujionee.