Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,817
- 4,568
Madini yenye uzito wa kilogramu 6.93 yenye thamani ya zaidi ya Tsh. milioni 961 yamekamatwa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya yakitoroshwa kwenda kuuzwa nje ya Nchi.
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema hayo akiwa katika machimbo ya dhahabu Wilayani Chunya wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Mbeya.
Mavunde amesema dhahabu iliyokamatwa ina thamani ya zaidi ya Tsh. milioni 961 na kama ingetoroshwa Serikali ingekosa mapato ya zaidi ya Tsh. milioni 68 yatokanayo na mrabaha, service levy na ada ya ukaguzi.
Akiongea na Wafanyabiashara wa Madini katika Soko la Madini Mbeya Mavunde amewataka wasijihusishe na njama zozote za utoroshaji madini kwani kufanya hivyo kunakosesha mapato ya Nchi na kudumaza juhudi za kuleta maendeleo “Mh Rais Dkt. Samia ameonesha dhamira ya dhati ya kuikuza Sekta hii hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha tunafanya biashara hii kwa uadilifu, uaminifu na uzalendo mkubwa”
“Wafanyabiashara wa madini nawatangazia tena kuacha kujihusisha na utotoshaji wa madini, tutachukua hatua kali kwa Watu wote wanaohusika bila kusita”