Polisi wakamata dhahabu ya Sh milioni 140 ikitoroshwa, mtuhumiwa atokomea, atelekeza gari

Kwani sheria inasemaje juu ya mahala mtu anaweza kuuza madini yake? Kuna masoko mangapi ya kuuza na kununua dhahabu nchini? Ukichimba dhahabu Chunya ,Je huwezi kwenda kuiuza Kwenye solo la Kahama?
Sheria inaruhusu ukauze popote ikiwa Tu,umekwenda kureport mathalani ofisi ya madini chunya.wao baada ya kuthamini thamani ya madini na kiasi cha royality unachopaswa kulipa,wanafunga seal unapewa certificate ya kusafirishia Hadi huko unapodhamiria ikiwa ndani ya mipaka ya nchi.
 
Kwahio Madini hayana cha kina stamp duty n.k. na je huyu mchimbaji akiuza na mnunuzi kununua na kuuza na kununua..., Je hapo kila mnunuzi anatoa kodi zipi (sababu sio kila muuzaji ni mchimbaji)
Kuna wanunuzi wa aina mbili,dealer na blocker,blocker kwa hio kikanuni blocker anapaswa kununua kwa huyu mchimbaji either awe na PML au wa kawaida tu...baada ya hapo yeye akienda kuuza soko la madini ndio atawajibika kulipa hizo 7.3% sababu kubwa ikiwa n kwamba yeye mara nying ananunua kwa mchimbaji kwa bei pungufu...mfano gram anaweza nunua 95k au 100k afu bei ya sokoni ikawa 120k
Ila kwa dhahabu iliotoka elution hata kama n ya mchimbaji mdogo hio atapeleka soko la madini kuuza otherwise alipie hizo 7.3% na afate taratibu kama ukizosema hapo juu
 
Ina maana jamaa kwenye kizuizi akaacha gari akaanza kutoka mbio vichakan 😀😀😀😀
Uhalif sio mzur ila jamaa kama kapewa mzigo sio wake atakua sio mzoef
Mzigo zaidi ya 140mil unakamatwa tu kama kuku
Uzuri hizi huwa zinachorwa toka site. Mwamba anakuwa kauzwa toka Saza yani ina maana wale barrier wanakuwa wanajua kabisa gari yenye mzigo 😂.

Yote haya ni zao la chuki na dhuluma kwenye machimbo huko. Mtu akitoka na mali kidogo watu wivu tu. Ukienda kule vijana amna kijana anatembelea gari namba C yani ni mwendo wa DV,DW,DX,DY
 
Jamaa huenda aliwaza yangemkuta ya jamaa wa Mtwara😀
 
Uzuri hizi huwa zinachorwa toka site. Mwamba anakuwa kauzwa toka Saza yani ina maana wale barrier wanakuwa wanajua kabisa gari yenye mzigo 😂.

Yote haya ni zao la chuki na dhuluma kwenye machimbo huko. Mtu akitoka na mali kidogo watu wivu tu. Ukienda kule vijana amna kijana anatembelea gari namba C yani ni mwendo wa DV,DW,DX,DY
Kingine ninachowaza na kunifurahisha ni eti jamaa kutoroka 😄😄😄😄
Kama walikua wanajua gari ina mzigo hawakujipanga namna ya kumtia nguvun
 
Kuna wanunuzi wa aina mbili,dealer na blocker,blocker kwa hio kikanuni blocker anapaswa kununua kwa huyu mchimbaji either awe na PML au wa kawaida tu...baada ya hapo yeye akienda kuuza soko la madini ndio atawajibika kulipa hizo 7.3% sababu kubwa ikiwa n kwamba yeye mara nying ananunua kwa mchimbaji kwa bei pungufu...mfano gram anaweza nunua 95k au 100k afu bei ya sokoni ikawa 120k
Ila kwa dhahabu iliotoka elution hata kama n ya mchimbaji mdogo hio atapeleka soko la madini kuuza otherwise alipie hizo 7.3% na afate taratibu kama ukizosema hapo juu
Dealer yeye analipa kodi zipi ? iwapo hio 7.3 itakuwa ishalipwa tayari na mimi Dealer nipo huku Dar nimeletewa mzigo au Bibi na Shangazi zangu wameamua kuyeyusha mikufu yao na kuniuzia na Je wale wanaopeleka nje wana Kanuni zao tofauti ?

Pia yale masoko ya Madini yaliyofunguliwa mikoani je ni bora kuuza kule kwa mchimbaji ? Pili bei ya Mkoa kwa Mkoa kweli itakuwa na utofauti mkubwa au kwa mtu ambaye hachimbi (kanunua) faida inapatikana nje tu (tena black market)
 
Kwan dhahabu na fedha ukiziwekakwenye siti alafu kwenye radio unaweka nyimbo za kikatoliki na bibliatatu nne ndan watakujua kweli
Hao jamaa wanakujua, hawakufuati kama hawakujui mkuu! Taarifa ndio kila kitu ina maana askari washapewa udau kuwa una mzigo kiasi gani na utapita njia gani!

Ina maana hapo walitaka wapoozwe tu na kwa huo mzigo huenda walitaka 10M ndio nchi yetu ilipofikia wether unafanya jambo kwa uhalalali au magumashi lazma kitu kidogo utoe sababu kuna vipengele vingi sana lazma uvipitie.
 
Kwan dhahabu na fedha ukiziwekakwenye siti alafu kwenye radio unaweka nyimbo za kikatoliki na bibliatatu nne ndan watakujua kweli
Huyu atakuwa kuna mtu kamchoma tu,ama huenda wakati anasafirisha askari walimuotea tu,muda mwingine unapotaka kufanya safari zenye maslahi kama hayo unatakiwa ujichanganye na raia
 
Huyu atakuwa kuna mtu kamchoma tu,ama huenda wakati anasafirisha askari walimuotea tu,muda mwingine unapotaka kufanya safari zenye maslahi kama hayo unatakiwa ujichanganye na raia
Ujichanganye na raia kivipi yani?
 
Si umeona hapo muda aliokuwa anasafirisha sio muda mzuri,saa moja giza limeshaingia vizuizi na macho kuona wanakuwa wengi tofauti na mchana
Ahaa angetoka zake mapema maybe ingekuwa salama😂 unakurupua chuma mchana tu kisha unalala giza likiingia
 
What if alikuwa anaenda kuhifadhi nyumbani kwa matumizi ya baadae?, sheria inasemaje kuhusu hili?

Mkuu DIBAJI lazima uwe na leseni ya broker au dealer ili kutunza au kusafirisha dhahabu. Mtu asiye na leseni hawezi kutunza dhahabu nyumbani kwake hata kama kapata kihalali. Ni sheria.
 
Dealer yeye analipa kodi zipi ? iwapo hio 7.3 itakuwa ishalipwa tayari na mimi Dealer nipo huku Dar nimeletewa mzigo au Bibi na Shangazi zangu wameamua kuyeyusha mikufu yao na kuniuzia na Je wale wanaopeleka nje wana Kanuni zao tofauti ?

Pia yale masoko ya Madini yaliyofunguliwa mikoani je ni bora kuuza kule kwa mchimbaji ? Pili bei ya Mkoa kwa Mkoa kweli itakuwa na utofauti mkubwa au kwa mtu ambaye hachimbi (kanunua) faida inapatikana nje tu (tena black market)
Hapo kwa ma dealer sina ufaham vizuri,mmachimbo mwisho wangu hapo sokoni tu..
Well kwa wachimbaji wadogo ambao naona kama dhahabu yako imetokana na elution its better ukaenda sokoni coz mpaka ukamaliza process za elution afisa madin atakua kajua source ya dhahabu
Ila kama ni dhahabu tu ya kukamatisha kwa mercury nadhani its better mchimbaji amuuzie broker kwa sababu mbili,kwanza kuondoa usumbufu make akienda sokoni directly na hana PML au broker licence lazima asumbuliwe.Pili maandalizi ya dhahabu za mercury mwishoni kwenye kuchoma hua n mbovu so ukienda sokoni na 30g wakichoma na gas anaweza jikuta na 25g kitu ambacho hakuna mchimbaji anakipenda (though price inaweza kua nzuri)
Bei hua ni ile ile Tanzania nzima,bei hutolewa kila siku na Benki kuu kwa hio sokoni ukifika tu unakuta na bei ya siku hio (kwa dhahabu tu Gemstones mchezo wake n mwingine kabisa)
Ambao hawachimbi wengi wanafanya black market kuwauzia masonara ndo wanakopigia faida...
NB (Kwa uwelewa wangu mdogo)
 
Kwahio Kisheria ni 7.3 Percent ya Value ya Mzigo vipi huenda pia valuation yao inakuwa ipo exaggerated au wanaangalia soko la dunia kw wakati huo ?

Bei ya dhahabu ni sawa kote duniani, kwa TZ inakuwa monitored na BOT na kila siku wanatangaza bei ambazo zinaendana na soko la dunia, ukiuziwa nje ya bei ya BOT ni ujinga wako umepigwa.
 
Bei ya dhahabu ni sawa kote duniani ukiuziwa nje ya bei ya soko la dunia ni ujinga wako umepigwa.
Yaani nanunua dhahabu Nyarugusu ili nikauze Huko Swiss alafu nimwambie yule mchimbaji aniuzie sawa na soko la Dunia ? Hapo takuwa nafanya Biashara au ninafanya kubalidilisha Pesa, na nikishaipata hio dhahabu mimi nakwenda kuwauzia wale duniani kwa bei gani ?
 
Back
Top Bottom