Kikosi cha Polisi Reli kimeendesha doria za kiusalama kwa kutumia Mbwa wa Polisi katika Kituo cha Treni cha Pugu na Karakana ya Treni, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kuimarisha ulinzi na usalama wa miundombinu ya reli.
Doria hiyo imefanyika Novemba 4, 2026, ikiongozwa na Sajenti wa Polisi Rahabu Mbaruku kwa kushirikiana na Koplo wa Polisi Said Ally, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kudhibiti vitendo vya uhalifu katika maeneo ya miundombinu ya reli.
Aidha, matumizi ya mbwa wa Polisi katika doria hiyo yanalenga kuongeza ufanisi wa shughuli za ukaguzi na ulinzi katika maeneo muhimu ya huduma za usafiri wa reli.
Kikosi hicho kinaendelea kutekeleza doria na operesheni mbalimbali za kiusalama ili kuhakikisha miundombinu ya reli inalindwa na mazingira ya utoaji huduma za usafiri wa reli yanakuwa salama kwa watumiaji.
Chanzo: Torch Media