Polisi wafunga mitaa Arusha, RPC Shana Aonya

Polisi wafunga mitaa Arusha, RPC Shana Aonya

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2016
Posts
757
Reaction score
1,822
Taharuki kubwa imewakumba wananchi wa jiji la Arusha wakati vikosi kabambe vya askari wa jeshi la polisi jijini hapa wakiwa na magari zaidi ya 50 yakiwemo ya maji ya kuwasha walipopita katika mitaambalimbali jijini hapa kwa lengo la kujiweka tiyari kukabili uhalifu kwenye mkesha wa sikukuu ya mwaka mpya

Askari hao walifanya doria katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kujiweka tayari katika kupambana na uhalifu wa aina yoyote unaoweza kujitokeza katika mkesha wa mwaka mpya.

Hata hivyo wananchi walioshuhudia vikosi hivyo vya polisi walipatwa na taharuki baada ya kuonaidadi kubwa ya askari hao waliokuwa wamevalia mavazi rasmi ya kikomandoo wakiwa kwenye magari ya wazi na silaha za moto na mabomu ya machozi wakiimarisha ulinzi na kuwahakikishia wananchi usalama wa kutosha.

Akiongea na vyombo vya habari kamanda wa polisi mkoani hapa ,Jonathan Shana amesema kuwa doria hiyo ya askari ni maalumu iliyolenga kuwahakikishia usalama wananchi wote wa jiji la Arusha katika kipindi chote za sikukuu za mwaka mpya na kuwataka wananchi walale milango wazi polisi watakuwepo kila kona .

Aidha kamanda Shana amewaonya wale wote wenye nia ovu ya kutaka kushiriki kwa namna moja ama nyingine vitendo vya uhalifu kuacha Mara moja kwa kuwa jeshi hilo kupitia vikosi vyake kabambe limejipanga kuhakikisha vitendo vya uhalifu havitokei na wahalifu wanadhibitiwa.

Ameonya iwapo kuna vikundi ama mtu. Binafsi anania ya kufanya uhalifu kuwa atashughulikiwa ipasavyo ikiwemo na atasherehekea mwaka mpya akiwa mahabusu.

Aliongeza kwa kuonya madereva watakaokunywa pombe na kuendesha gari wakiwa na kilevi wachukue tahadhali kwa kuepuka kunywa kupita kiasi ili wasisababishe ajali.

IMG_20191231_140910.jpeg
IMG_20191231_140750.jpeg
IMG_20191231_140840.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi ikikosa vita haya ndio matatizo yatayojitokeza, wanatafuta pakuvalia hayo manguo hawapapati, wanatafuta pakurushia hayo mabomu hawapapati, matokeo yake watayarusha kwa wananchi wanaoshangilia mwaka mpya!.

Wapelekeni huko nchi za watu wakatulize ghasia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unazingua,
Unataka wasioneshe uwepo wao kisha wahalifu wapate moyo wa kufanya uhalifu uje uwalaumu humu mitandaoni Polisi hawafanyi kazi yao.
Kwani wakivaa hayo mavazi, wakaandamana wenyewe kama hivyo walivyofanya bila kumvamia raia mwema wewe wanakudhuru nini?

Sio kila kitu unakimbilia kulaumu. Ni bora wawatishe wahalifu waogope kujaribu uhalifu kuliko wanyamaze wasubiri kuzima tukio na silaha huku hao wahalifu wakiishia jela au mortuary. Kwa kufanya kitisho wame waokoa watu na mali zao.
 
Vyombo vyetu vya usalama viko imara na tayari kikamilifu kukabiliana na yeyote yule atakaye jaribu kutuondolea amani tuliyodumu nayo kwa miaka mingi sisi kama taifa.
 
Huyo jamaa hata alipokuwa Mwanza alikuwa na mbwembe hizo hizo! Hana mamlaka tu nafikiri anahamu azitumie kabisa hizo silaha
 
Wee unataka tanzania ipate maafa yasiosahaulika hawa wakienda huko nje labda wakawe security wa kawaida tena wasiopewa silaha
Nchi ikikosa vita haya ndio matatizo yatayojitokeza, wanatafuta pakuvalia hayo manguo hawapapati, wanatafuta pakurushia hayo mabomu hawapapati, matokeo yake watayarusha kwa wananchi wanaoshangilia mwaka mpya!.

Wapelekeni huko nchi za watu wakatulize ghasia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi ikikosa vita haya ndio matatizo yatayojitokeza, wanatafuta pakuvalia hayo manguo hawapapati, wanatafuta pakurushia hayo mabomu hawapapati, matokeo yake watayarusha kwa wananchi wanaoshangilia mwaka mpya!.

Wapelekeni huko nchi za watu wakatulize ghasia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nguchiro kweli ww kwani waliajiriwa kwaajili ya kupigana nchi za watu?
Mkikabwa mitaani hamuishi kulalamika mbaya zaidi hata kujitetea wenyewe hamuwezi, vitoto viwili vikiwatishia kidogo mnafarakana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom