N
Nguvu kubwa akili kisoda!Taharuki kubwa imewakumba wananchi wa jiji la Arusha wakati vikosi kabambe vya askari wa jeshi la polisi jijini hapa wakiwa na magari zaidi ya 50 yakiwemo ya maji ya kuwasha walipopita katika mitaambalimbali jijini hapa kwa lengo la kujiweka tiyari kukabili uhalifu kwenye mkesha wa sikukuu ya mwaka mpya
Askari hao walifanya doria katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kujiweka tayari katika kupambana na uhalifu wa aina yoyote unaoweza kujitokeza katika mkesha wa mwaka mpya.
Hata hivyo wananchi walioshuhudia vikosi hivyo vya polisi walipatwa na taharuki baada ya kuonaidadi kubwa ya askari hao waliokuwa wamevalia mavazi rasmi ya kikomandoo wakiwa kwenye magari ya wazi na silaha za moto na mabomu ya machozi wakiimarisha ulinzi na kuwahakikishia wananchi usalama wa kutosha.
Akiongea na vyombo vya habari kamanda wa polisi mkoani hapa ,Jonathan Shana amesema kuwa doria hiyo ya askari ni maalumu iliyolenga kuwahakikishia usalama wananchi wote wa jiji la Arusha katika kipindi chote za sikukuu za mwaka mpya na kuwataka wananchi walale milango wazi polisi watakuwepo kila kona .
Aidha kamanda Shana amewaonya wale wote wenye nia ovu ya kutaka kushiriki kwa namna moja ama nyingine vitendo vya uhalifu kuacha Mara moja kwa kuwa jeshi hilo kupitia vikosi vyake kabambe limejipanga kuhakikisha vitendo vya uhalifu havitokei na wahalifu wanadhibitiwa.
Ameonya iwapo kuna vikundi ama mtu. Binafsi anania ya kufanya uhalifu kuwa atashughulikiwa ipasavyo ikiwemo na atasherehekea mwaka mpya akiwa mahabusu.
Aliongeza kwa kuonya madereva watakaokunywa pombe na kuendesha gari wakiwa na kilevi wachukue tahadhali kwa kuepuka kunywa kupita kiasi ili wasisababishe ajali.
View attachment 1308455View attachment 1308456View attachment 1308457
Sent using Jamii Forums mobile app