Polisi wadaiwa kumlisha sumu mtuhumiwa


Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Messages
42,404
Likes
38,581
Points
280
Bujibuji

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2009
42,404 38,581 280
JESHI la Polisi mkoani Kiliamanjaro, limeingia katika kashfa baada ya askari wake wawili kudaiwa kumlisha sumu mtuhumiwa waliyemkamata na mbao zinazodaiwa kuvunwa isivyo halali na kusababisha kifo chake.

Habari zilizopatikana jana kutoka wilayani Rombo na kuthibitishwa na baadhi ya maofisa wa polisi mkoani hapa, zilidai kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 17, mwaka huu, katika kijiji cha Kiraeni ambako polisi hao wakiwa na pikipiki, walimkamata mtuhumiwa na vipande vinane vya mbao na kisha kumtaka awape rushwa ya sh 400,000.

Kwa mujibu wa mashuhuda waliozungumza na TanzaniaDaima kwa njia ya simu kutoka Rombo, askari hao wanadaiwa kumpa vitisho vya kila aina marehemu aliyetajwa kwa jina la Hubert Massawe na baadaye kupewa sh 100,000.

Mashuhuda hao walidai kuwa baada ya askari hao kupewa kiasi hicho walimshurutisha marehemu awamalizie kiasi kilichobaki na kwenda naye hadi nyumbani kwake ambako hawakuambulia chochote kutokana na kutokuwa na fedha zaidi.

Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz, hakuwa tayari jana kuthibitisha tuhuma hizo baada ya kutuma ujumbe mfupi kwa maandishi kupitia simu yake ya kiganjani kuwa yuko kwenye mkutano.

Naye Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani Rombo, Chuzela Shija, alisema taasisi yake imeanzisha uchunguzi juu ya tukio hilo kutokana na kile alichodai kuwa linahusu tuhuma za rushwa.
Inadaiwa kuwa askari hao baada ya kuona mtuhumiwa ameshikwa na jazba,walimpa maji yaliyokuwa kwenye chupa yanayoamika kuwa ni sumu na kumlazimisha ayanywe.

Kwa mujibu wa mashuhuda hao, mtuhumiwa alichukua maji hayo na kuingia nayo ndani na aliporudi alinza kujisikia vibaya na kukimbizwa katika zahanati ya kijiji cha Kiraeni lakini kutokana na kuzidiwa na sumu hiyo alikimbizwa hospitali ya wilaya ya Huruma na alifariki Novemba 18, mwaka huu.

Machi mwaka huu, askari watatu wa kituo cha polisi cha Tarakea wilayani Rombo walifukuzwa kazi kwa fedheha wakituhumiwa kufanya vitendo vya kulidhalilisha jeshi hilo baada ya kuuza mali ya mfanyabiashara mmoja wilayani Rombo, Genes Shayo, bila ridhaa yake na bila yeye kuwapo.

Askari waliofukuzwa kazi ni pamoja na aliyekuwa dereva wa mkuu wa kituo cha polisi Tarakea, mwenye namba D.3289 Sajenti Joseph, F.3677 PC. Esebius kutoka idara ya upelelezi wa makosa ya jinai na F.6620 PC. Johnson ambaye ni askari wa kawaida.
 
lutayega

lutayega

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2012
Messages
1,252
Likes
89
Points
145
lutayega

lutayega

JF-Expert Member
Joined Feb 29, 2012
1,252 89 145
bora kuishi bila jeshi kuliko kuwa na jeshi ambalo mara zote ndiyo mwanzilishi wa migogoro na fujo. R.i.p masawe
 
Kamkuki

Kamkuki

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2011
Messages
1,125
Likes
138
Points
160
Kamkuki

Kamkuki

JF-Expert Member
Joined Feb 1, 2011
1,125 138 160
Polisi .......? kwanza ni moja ya maajent ya shetwani maana *wanabambikia watu kesi *wanawatanguliza binadam wenzao mbele za haki *ni genge la kihuni flani hivi na sijui kama nchi nyinginezo nako kuna vituko kama vya hawa wa Tz:confused2:
 
Angel Msoffe

Angel Msoffe

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2011
Messages
6,796
Likes
87
Points
145
Angel Msoffe

Angel Msoffe

JF-Expert Member
Joined Jun 21, 2011
6,796 87 145
Sijui km kuna polisi atakayeuona ufalme wa mbinguni,LABDA ATUBU DAKIKA CHACHE KABLA UMAUTI HAUJAMFIKA
 
L

lufungulo k

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2012
Messages
1,754
Likes
820
Points
280
L

lufungulo k

JF-Expert Member
Joined Apr 19, 2012
1,754 820 280
mh mbona ,kilimanjaro kumejaa, rushwa, majungu, magendo na shuhuda wa yote ni gazeti la tanzania daima? maana hiyo habari naiona imekaa kiuhalifu , na kudaiwa rushwa na majungu ya kusababisha kifo. anayetoa habari hizo mwandishi tanzania daima. je anamahusiano mazuri na polisi au ana chuki nao, eti kalazimishwa kunywa maji na polisi ,kayachukuwa kisha kaingia nayo ndani, mh typical majungu.
 
K

katalina

JF-Expert Member
Joined
Apr 4, 2012
Messages
264
Likes
1
Points
0
K

katalina

JF-Expert Member
Joined Apr 4, 2012
264 1 0
Nilizani mleta uzi ungebalance story ili tuone ukweli wake. Je madakatari wanasemaje kuhusu kifo hiki, kimetokana na sumu au kitu gani. Mashuhuda wa tukio wanasemaje. Nadhani ingependeza sana tukapata maoni kutoka pande zote na siyo hivi ulivyoripoti! Hata hivyo nawapa pole wafiwa.
 
BADILI TABIA

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2011
Messages
30,997
Likes
6,428
Points
280
BADILI TABIA

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Joined Jun 13, 2011
30,997 6,428 280
.....kwa polisi wa tz, wala sio jambo la ajabu..
 
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2010
Messages
47,675
Likes
3,321
Points
280
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2010
47,675 3,321 280
....jeshi la wauaji Tanzania....
 
kichwat

kichwat

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2010
Messages
1,823
Likes
47
Points
145
kichwat

kichwat

JF-Expert Member
Joined Mar 4, 2010
1,823 47 145
Sijui km kuna polisi atakayeuona ufalme wa mbinguni,LABDA ATUBU DAKIKA CHACHE KABLA UMAUTI HAUJAMFIKA
hapa tulipofika tunahitaji kutatua matatizo yetu hapahapa duniani, kabla hatujaondoka. habari za 'fulani hataingia ufalme wa mbinguni' hazitupumbazi tena na tusizipe nafasi.
 
Mulhat Mpunga

Mulhat Mpunga

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2010
Messages
26,817
Likes
14,355
Points
280
Mulhat Mpunga

Mulhat Mpunga

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2010
26,817 14,355 280
yani hawa polis wengi wao ni wauwaji kabisa lolg
 
Baba V

Baba V

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2010
Messages
19,499
Likes
218
Points
160
Baba V

Baba V

JF-Expert Member
Joined Dec 29, 2010
19,499 218 160
ukipima kati ya ujambazi wa polisi na wanavyolinda usalama ni heri jeshi hili lisingekuwapo.anayepinga na aje twende sawa
 
Daudi Mchambuzi

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Messages
36,690
Likes
47,374
Points
280
Daudi Mchambuzi

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2010
36,690 47,374 280
Vipande vinne vya mbao wamemuhukumu bwana massawe kifo,
Wale wa kontena zima la pembe za ndovu wanapeta na vyeo wanaongezwa.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Vmark.

Vmark.

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2011
Messages
1,356
Likes
14
Points
0
Vmark.

Vmark.

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2011
1,356 14 0
Haya polisi wa Rombo nendeni pale nyumbani kwangu Mkuu kijijini Maharo nina mbao pia mnibane niwape rushwa pia!
 

Forum statistics

Threads 1,237,195
Members 475,497
Posts 29,280,990