Polisi traffic nawakubali sana

shade

Senior Member
Oct 29, 2010
155
39
Hili naliongea toka moyoni. Naikubali sana kazi ya hawa maafisa wa serikali. Sio mtazamo bali naangalia kujitoa kwao.
Sababu ninayosema hivi ni mazingira wanayofanyia kazi ambayo ni magumu sana.
Mvua ikinyesha ni wao ndio watakao simama barabarani kuhakikisha msongamano unapungua n sheria inafuatwa.
Jua ni lao pia. Kumbuka msimu wa kiangazi vumbi ni jingi sana lakini wao wapo tu.
Usiku wakati watu wanarudi toka maofisini na msururu ni mrefu lakini wao wapo tu. Na utakuta baada ya hapo wanaondoka wakiwa wamechoka bila kuwa n usafiri wa kuwa rudisha ktk makazi yao.
Kwa moyo huu wa uzalendo napenda kusema ninawaheshimu sana.
Tuwape heko na sio malalamiko yetu binafsi.
I salute you all traffic police
 
Pamoja na sifa zao zote, Ila wakati mwingine hekima huwatoka.
Mfano, pale ubungo mataa priority yao kubwa ni mabasi ya mikoani kuliko njia zingine, asubuhi unakuta njia ya kwenda kimara inapewa upendeleo zaidi ya njia zingine, na jioni njia ya kwenda mjini inakuwa inatembea zaidi ya njia zingine just mabasi yapite tu.

2. Siku hizi wamekuwa mawakala wa TRA badala ya kuelimisha madereva, unaweza kukuta kosa ni la kuelekeza tu lakini unakuta anakupiga fine hadi unashangaa.
 
Upendeleo huu kumbe ni wa kila siku, basi kutakua na kitu wanakizingatia, na sio upendeleo Bali ni utaratibu, pole Sana kwa kukerwa.
 
Elimu ya msingi kwa madereva ni kwenye shule za udereva, polisi wanatoa elimu kwa watumiaji wa Barabara km kuna jambo jipya sana, vinginevyo kazi ya msingi ya Polisi wa Usalama barabarani imejikita zaidi kwenye kuchukua hatua zaidi kwa mtindo wa tozo ya papo kwa papo au ikibidi kufikishwa mahakamani.
 
hiyo kazi sio ya kujitolea polisi wengi wanaililia sana ...

trust me wenyewe wanaamini ukitolewa u traffic ukapelekwa gd ni kama umeshushwa cheo
 
Elimu ya msingi kwa madereva ni kwenye shule za udereva, polisi wanatoa elimu kwa watumiaji wa Barabara km kuna jambo jipya sana, vinginevyo kazi ya msingi ya Polisi wa Usalama barabarani imejikita zaidi kwenye kuchukua hatua zaidi kwa mtindo wa tozo ya papo kwa papo au ikibidi kufikishwa mahakamani.
Shule gani ya udereva inakufundisha namna ya kutumia hizi barabara za mpya za morogoro road (kimara-Sokoine drive, Kimara - Morocco, msimbazi, etc).
2. Barabara nyingi, mfano kama wewe ni mwenyeji Dar, kuna kibao gani kinachokuekeza kuwa iwapo unatoka Kilimanjaro hotel hutakiwi kwenda na sokoine Drive - ukielekea station?

3. Kwenye highway za mikoani, say jamaa wanajificha na tochi zao vichakani, wakati mwingine hakuna vibao vinavyoonyesha speed 50 lakini unajikuta unasimamishwa na kupigwa fine.
 
Ww ni trafic mwenzao nn mbona hujaorodhesha kasoro zao wakat nao wamekuwa mabingwa wa kukusanya kodi bila kutoa elimu kwa matumiz ya barabara zaid wao wanakutoza faini mwisho wa mwez wanatangaza et tumekusanya mil kadhaa yan sio kabisa
 
Upendeleo huu kumbe ni wa kila siku, basi kutakua na kitu wanakizingatia, na sio upendeleo Bali ni utaratibu, pole Sana kwa kukerwa.
Kuhusu Morogoro Rd kupendelewa, Mara mbili nikiwa katika mabasi tofauti, niliwahi kuthibitisha upendeleo huo kwa traffic anayekuwa zamu pale ubungo mataa hupigiwa simu na kuomba kusogezwa, tulikuwa Kimara dereva akampigia simu jamaa - traffic kuwa nisogeze nivute nikawahi kupumzika, nilichoshuhudia jamaa alipiga moto na baada kuvuka zile taa za ubungo traffic akazuia magari ya kutoka kimara na kuruhusu yanayotoka external.
 
Mimi nawapenda jinsi wanavyopokea rushwa tu.
Sijanywa chai = Kwani mie mgahawa?
Sijala chakula cha mchana = Eboo kwani mimi Mamantilie?
Fanya maarifa ya dinner mkuu basi = Mimi dereva sio muuza kiosk nenda kale chipsi kuku huko.
Lakini hayo yote ulioainisha ni moja ya ajira zao.
 
hata wakiambiwa kufanya bila mshahara bado watagombania hiyo kazi !! ama ina kagugu - pesa inaingia bila tabu, mtaji ni gwanda tu ambalo mlipa kodi kali gharamia !!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom