MamaBeata
JF-Expert Member
- Apr 15, 2013
- 325
- 112
Nimekuwa safarini siku mbili hizi na nimeshuhudia rushwa nje nje imekuwa kama tuko Nigeria vile. Yaani traffic police wanasimamisha magari halafu hawaji kwenye gari konda anazunguka nyuma ya gari anampa hela. Na hiki kipindi naskia wanatafuta hela ya sikukuu ni wamejaa humo barabarani usiseme.
Kilichoniuma ni kuwa kimsingi polisi ndio wasimamizi wa sheria lakini wanachukua rushwa huku raia wakishuhudia. Hali hii inatisha. Mbaya sana. Hata watoto wadogo wanaona wanajifunza nini? TAKUKURU Wapo na hawaoni haya yanayotokea. Mbaya!!!