Polisi Pwani yatoa ripoti ya matukio ya uhalifu kwa mwaka 2020. Makosa ya jinai yaripotiwa kupungua

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,395
2,000
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limeripoti kutokea kwa makosa ya jinai 1,791 mpaka kufikia Desemba 2020 ikilinganishwa na makosa 2,189 yaliyoripotiwa katika kipindi kama hicho mwaka jana.

Ripoti hiyo imetolewa leo Desemba 29, na Kamanda wa polisi mkoani humo, Wankyo Nyigesa alipokuwa akizungumza kuhusu mwenendo mzima wa makosa hayo kwa miaka miwili mfululizo.

Nyigesa amesema makosa ya jinai ya mwaka 2019 yalikuwa mengi na kwamba mwaka 2020 yamepungua kwa tofauti ya makosa 398 sawa na asilimia 18.2.

“Kupungua kwa makosa haya kumetokana na kazi nzuri inayofanywa na jeshi la polisi kwa kushirikiana na wananchi katika kudhibiti makosa ya kibinadamu.

“Makosa hayo ni pamoja na mauaji, kubaka, wizi wa watoto, usafirishaji haramu wa binadamu, unyanga’nyi wa kutumia silaha, wizi wa mifugo, wizi wa magari, wizi wa uvunjaji, wizi wa pikipiki na uhalifu mwingine,” amesema Nyigesa.

Kuhusu ajali za barabarani, Nyigesa amesema waliweka mkakati ya kukabiliana na matukio hayo na kwamba mwaka 2020 wamefanikwa kupunguza ajali hizo kwa kiwango kikubwa.

Amesema, mikakati ya 2021 ni kuhakikisha mkoa unapunguza matukio ya uhalifu wa matukio ya ajali barabarani kwa kuimarisha doria katika maeneo yote na ukaguzi wa mara kwa mara.

Pia amewaomba wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi hilo hasa kupitia askari kata waliopo katika maeneo yao pamoja na vyombo vingine vya usalama ili kuufanya mkoa kuwa eneo salama la uwekezaji.
 

Tigershark

JF-Expert Member
Oct 9, 2018
7,091
2,000
Vp uhalifu wa polisi dhidi ya raia? Hakuna kabisaa pwani kwa mwaka 2020? Hakuna watu waliobambikiziwa kesi au kuuwawa wakiwa chini ya uangalizi wa polisi Pwani?
 

kadendu

JF-Expert Member
Mar 30, 2014
427
250
Kipekee nimpongeze kamanda RCO PWANI ni askari aliyetukuka jeshi la polisi lijivunie kwa huyu askari anaijua vema kazi yake na anaipenda.
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
56,181
2,000
Polisi waweke na idadi ya maaskari Polisi wanaojiua kutokana na wivu wa mapenzi.
Polisi wala rushwa (hapa ni pagumu, maana wote ndio biashara yao, hamna wa kumkamata mwenzake)
Polisi waweke idadi ya Askari waoshirikiana na majambazi na wauza dawa za kulevya na uhalifu mwingine
 

elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
8,697
2,000
Kupungua kwa wizi kunatokana na watu kutokuwa na vitu vya kuibiwa, walianza kutoweka wezi wa mifukoni kwenye daladala na sasa mwezi wa majumbani, mtu mwenye mlo mmoja tu kwa siku utamuibia nini!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom