Badili maisha yako leo: Yajue Mawe Saba na Madini saba tu yanayoweza kukubadilishia au kukuletea unachotaka

Rakims

JF-Expert Member
Jun 4, 2014
4,982
4,481
JINSI YA KUBADILI MAISHA KWA KUTUMIA MAWE NA MADINI

Makala hii itakufundisha jambo ambalo linaweza kubadirisha mlolongo wa maisha yako kwa njia moja au nyingine ikiwa utafuata vema na kutilia maanani kisha ukatendea kazi.

Kila mtu katika maisha hufikia kipindi na kuanza kujiuliza maswali kama ifuatavyo
  • Ni lini na wewe utakuwa mtu mbele ya watu?
  • Rafiki mbele ya marafiki?
  • Mwenye pesa mbele ya wenye pesa?
  • Msemaji mbele ya wasemaji?
  • Mfano mbele ya mifano?
  • Tajiri mbele ya matajiri?
  • Mwenye kutoa huduma mbele ya wahudumiaji?
  • Mwenye kuoa mbele ya wenye ndoa?
  • Mwenye kuibuka mbele ya walioibuka?
  • Mwenye kutamanika mbele ya wenye kutamanika?
  • Mwenye kazi mbele ya wenye kazi?
  • Mwenye kukubalika mbele ya wenye kukubalika?
  • Mwenye Miujiza mbele ya wenye Miujiza?
Jinsi ya kufanikiwa kinyota

Acha kujiuliza na utende leo,

Ninachoenda kufundisha hapa kwenye makala hii basi itamnufaisha kila mmoja kwa level zote za maisha na akapata anachotamani bila kufanya dhulma ya nafsi au roho yake mwenye na kujikita katika ushetani,au mambo yasiyopendeza mbele ya Mwenyezi Mungu na jamii nzima,

Nifuatilie katika makala hii ili kujua ni nini ninachozungumzia

Kwa kuanza nitawakumbusha au kuwarudisha nyuma kwamba kabla ya kuumbwa mwanadamu na vyote vilivyopo ilianza kauli ya Mwenyezi mungu ambayo waislamu tunaitambua kama "Kun faya kun" kuwa na jambo likawa kauli yake Allah (S.W)

Lakini pia kwa wakristo nao pia wanaamini kuwa hapo mwanzo kulikuwa (Neno) neno kwa maana ya kawaida ni kauli inayotamkwa,

Dunia hii inaaminika kuwa iliubwa kwa Mawe au kauli za Mwenyezi mungu au kwa wasioamini uwepo wa roho pia wao husema kuwa Dunia ni mkusanyiko wa maada mbalimbali ambazo zilijichanganya na kufanya uumbaji wa viumbe,

Nachochukua kutoa hapo sehemu zote 3 maana yake ni kwamba (Islam/Christian & pagan) wote wanakubali kwamba kuna maada zilizotumika katika uumbaji.

Elements zipo katika sehemu kuu nne ambazo ni:
  • moto
  • upepo
  • Maji
  • udongo
Sisi tunaoamini katika dini na Mwenyezi Mungu tunaongeza moja Ambayo ni

ROHO

Hivyo inakuwa
  • Moto
  • Upepo
  • Maji
  • Udongo
  • Roho
Kwa mpangilio huu tunaona ya kwamba;

  • Huwezi kupata udongo bila roho.
  • Huwezi kupata Maji bila udongo
  • Huwezi kupata upepo bila maji
  • Huwezi kupata chochote kile bila Chanzo

Kikawaida hata kwa maisha ya leo unakuta huwezi kupata kitu bila ya kitu.
Sasa sisi teyari ni roho ili tuweze kufika popote pale tunapotaka kwenda lazima tufuate vema safari tunayoenda bila kukosea hatua hata moja, na inapotokea mtu akikosea basi hurekebisha.

Ukumbuke chanza chako ni roho na mwisho wako ni roho.

Binafsi huwa naamini jambo moja kwamba Mwenyezi mungu vyovyote vile unavyomjua wewe hakuleta mtu duniani kuja kuteseka bali kuishi na kumuabudu na kisha kurejea kwake zake.

Turejee katika makala yetu ;

Katika hii dunia kuna mawe mengi ambayo yana kazi tofauti tofauti isipokuwa kuna mkusanyiko wa mawe saba na madini saba. Ambayo ikitokea mtu akatumia kwa ufasaha basi pale ambapo anakuwa na tatizo linalomshinda kutatua.

Ikiwa mtu anataka mafanikio kupitia nguvu ya ziada basi moja kwa moja huwa kuna aina saba za mawe na madini anaweza kutumia kwa utaratibu sahihi katika kupata mafanikio ya maisha ikiwa ni pamoja na;

  • Muonekano
  • Pesa
  • Maelewano na watu
  • Makazi
  • Utajiri
  • Afya
  • Mapenzi
  • Kinga
  • Nguvu za miujiza
  • Kazi
  • Marafiki
  • Mafanikio ya miujiza

Aina saba za madini ni:

  1. Lead/Risasi
  2. Tin/Bati
  3. Iron/ chuma
  4. Gold/dhahabu
  5. Copper/ kopa
  6. Brass/ shaba
  7. Silver / Fedha

Aina saba za mawe ni:

  1. Diamond
  2. Ruby
  3. Emerald
  4. Sapphire
  5. Pearl
  6. Onyx
  7. Turquoise
Mbadala wa mawe hayo ni:

  1. Garnet
  2. Agate (Aqeeq)
  3. Moonstone
  4. Amethyst
  5. Quartz
  6. Tourmarine
  7. Peridot
Kwa nini mawe haya yana mbadala. Hii ni kulingana na gharama ilivyo kubwa kwa mawe husika ndio maana huwa tunashauri watu kuanza na hatua moja ikikufungulia milango unaenda hatua ya pili.

Hayo ndio madini na mawe makuu yenye maana pana na kubwa sana na historia iliyo nzuri na kipekee Nitazidi kuendelea kufafafanua na kuupdate makala hii ili kuweza kujua ni jinsi gani mtu unaweza kujikwamua ulipokwama.

Basi kuna madhara makubwa kwa watu wenye kuvaa mawe na madini ambayo hawafahamu maana zake kuvaa madini usiyoyajua ni sawa na kucheza kamari unaweza kubahatisha ukala ama ukaliwa lakini wanaoliwa ni wengi kuliko wanaokula hivyo ni vema kuzingatia kila jambo unalolianza ujue na mwisho wake.
Mingine ni mikosi ambayo itakugharimu muda mrefu kuweza kuiondoa. Jiepusheni na mambo msiyoyajua.

Sasa tukiachana na hayo tuanze na aina moja moja ya madini na kazi zake:


MADINI YA RISASI

Madini ya risasi


madini haya utawala wake upo kwa malaika wa siku ya jumamosi ambaye anaitwa Cassiel au Kasfayaiill, na Jini anayetawala Jumamosi anaitwa,
Abuu Nuhu Au waswahili humuita Maimuna au kiizrael huitwa Aratron.

kama nilivyoweka kuwa ya kwanza kuelezea basi pia ujue ndio madini yaliyokuwa sawia kuliko mengine katika mambo ya kiroho,

Nayo hii inatawala sayari ya Zohari(saturn) na wenye kuzaliwa chini ya sayari hii sote tunafahamu uzito wa hizi sayari na kugharimika katika mambo tunayoyafanya yawe ya heri au shari na miinuko/mihemko,fikra,hisia na maamuzi kutokana na sayari hizi kiroho na kazi zake ni wachache kati yetu wasiofahamu kazi za sayari hizi,

kama unahisi hufahamu hapana unafahamu kabisa mambo ya kiroho yanatawala sana masharti, masharti haya hutokea kulingana na sayari unayofanyia jambo lako hilo kama kuponya,mapenzi,utajili n.k

Kama ilivyo kwa madini haya mazito pia mepesi na machafu ndivyo ilivyo sayari ya Zohari ambayo huleta kwa mtu majukumu makubwa kwenye maisha ya mtu basi madini haya hutoa wepesi ndani ya uzito huo na ufanisi mzuri wa utendaji kwa mvaaji katika maisha yake na kipato chake,

hufanya mtu kuona wepesi wa mambo mengi pia muonekano wa kupenda na wengine huwafanya kuvutia mbele ya watu hasa anapovaa mwanasiasa na humletea mtu manufaa yake binafsi anayoyahitaji,

Sehemu kubwa ya magonjwa ya milipuko yanayoletwa na aura mbovu za watu wenye aura nyeusi vijicho na husda, huzuni, woga, kukosa, kufunga, kutokuwa na maamuzi ya maisha yako binafsi.

Tamaa za ulimwengu kutokana na ushawishi wake yote hayo. Madini haya ukijua siku saa na kipindi cha kuyavaa basi utajionea ajabu,

humzuia aliyevaa kutokana na kutapeliwa hovyo kudanganywa na ujinga ujinga wa kilaghai pamoja na hila za watu na zake mwenyewe,

humfanya mwenye kuvaa kuwa na mawazo ya kitukufu na kumuondolea woga wa imani za kishirikina.

tofauti kubwa ya mtu anaevaa risasi ni kutokuwa na tahadhari ya yale anayoambiwa na kuyasikia mbali na kuyafuata anakuwa hana tofauti na maamuzi ya watu waliozaliwa chini ya sayari hii yaani wenye nyota za mbuzi na ndoo.

Na unapovaa madini haya basi huwezi kufanya kitu kwa kukurupuka wala kuwa na pupa ya mambo mazuri au mabaya,wala kufikiria gharama zake basi hata ikiwa mme au mke wako ni mtu wa kuhuzunika na manung'uniko hovyo,

Basi mtafutie pete ya Risasi kavu hapo utakuwa umemaliza kulingana na siku na saa ambayo wakati anazaliwa sayari hii ya Zohari ilikuwa wapi na katika element ipi udongo au upepo,

Kisha unamvisha saa kama hiyo au unampa aijaribu tu kuivaa saa hiyo ataing'ang'ania moja kwa moja dhiki yako ya manung'uniko yake kwako itakuwa imeisha.
Na huzuni na mengineyo niliyoyataja hapo atanufaika nayo,

Humsaidia mtu mwenye tabia za husda na roho mbaya kukaa sawa kitulivu na huwa mwenye hekima za ajabu na humpunguzia tabia za uchoyo mtu na humuondolea mikosi ya mwilini,

Humfanya mtu kuweza kuishi na watu kwa wema na humuondoshea ubaguzi wa aina yoyote ile.

Humfanya kuona ni nafasi ipi na yai anayoyahitaji anaweza kuyapata vipi huja kama mawazo au maono kichwani.
Mpe mtu aliyekata tamaa ya maisha na watu waliovunjika moyo katika maisha basi kadri siku zitakavyokuwa zikienda utaanza kuona anabadilika hata wagonjwa wenye kujikatia tamaa au visirani basi wavishe Risasi hii basi utamuona kila siku anavyobadilika na kuendelea kupata hamasa nzuri,

Pia kama kuna mtu unamchukia sana na unatamani hata kumuumiza au mtoto au ndugu basi mvishe Risasi taratibu roho yako itaanza kujirudi kwake kwa sharti tu la kujua wakati anazaliwa sayari ya Zohari/Saturn ilikuwa wapi na kwa hali gani ili iweze kufanya maajabu ndani ya siku 1-3 Utanishukuru baadae

Pia madini haya humfanya mtu kujihisi na yeye ni sehemu ya watu waliopo duniani humu na anaweza kufanikiwa kirahisi na hakuna chochote cha kuzuia hilo.

Humsogezea mtu kitu ambacho roho yake hutamani naomba nieleweke hapa ya kuwa unahisi kwamba ukiwa na pesa au tajiri ndio utafurahi hapana.

Kama kwenye utajiri wako huo utapenda kuona umempata mke au mume fulani au wa fulani ndio roho yako itatakata basi itakuvutia uwiano sawa na utampata na utakuwa mwenye furaha.

Pia kama unatamani kumiliki gari ya thamani na huna chanzo chochote cha kuipata basi kazi ya hii sio kukununulia gari hapana hii itakuletea hiyo gari ya thamani na utatumia hadi utakapo choka na kurudisha kwa mwenyewe.

hivyo unatakiwa uwe specific na wish unazoweka hapa ndio wengi hukosea kwenye maswala ya kiroho anatamani kitu bila kukiweka wazi basi matokeo yake anakipata na kushindwa kujua kama anacho,

mfano:
Mtu ni mwanafunzi na anaishi kwao, anatamani awe anakaa peke yake na gari ya kutembelea halafu bado yupo shule.
Hivi vitu atavipata na hata jua kama kavipata sasa anapata nafasi ya kuhama eneo analosoma anahamia mji wa ugenini anapangiwa na wazazi wake au ndugu wa wazazi wake nyumba ya kuishi ili asome huko nje ya mji wake na anapewa gari ya kuendea shule na mafuta hesabu zipo kwa muhusika sasa anakuja kusema nilitamani niwe na nyumba na gari,

nimepata ya kupangiwa na gari ya kuazimwa hapa hukutamani wewe vya kwako ulitamani randomly hivyo kimekuja randomly vile vile.

MADINI YA BATI au PETE ya BATI

Pete za bahati



Bati ni madini yanayosimama siku ya Alhamisi malaika wake ni Sarfayail/Israfil ambaye huyu hupuliza baragumu siku ya hukumu Judgement Day ambapo yeye huamrishwa na Mwenyezi mungu kufanya hivyo siku hiyo,

Roho zote zikafufuliwa Mungu atujaalie tuwe ni miongoni mwa walio bahatika kufaulu siku hiyo. Pia utawala wa chini huku duniani yupo jini au Mfalme anaitwa Shamhuurush Kadhi wa Majini au Bethor kiizrael

Madini haya ya bati kiroho hutumika na wenye nyota zinazo tawala sayari hiyo katika kuwavutia:

  • elimu
  • utajiri,
  • miujiza mbalimbali
  • mafanikio,
  • maendeleo n.k
Ambapo hupendeza sana yakitumiwa siku za alhamisi mchana na jumapili usiku na pia huwaletea wanyonge ufanisi na ulaini wa mambo,

Madini haya humletea mvaaji utajiri bila kutumia nguvu nyingi lakini pia humfanya mtu kujihisi kuwa bora zaidi kuliko wengine, bila kuwa na kiburi cha kufuru

Pia kushinda mambo ya kiserikali kuwaondolea wenye matatizo ya shinikizo la damu na kuwaponya kabisa ingawa ni kwa taratibu sio hapo kwa hapo tusije kushikana uongo.

Kuwasaidia katika biashara safari na kuoa au kuolewa kwa wenye kukosa ndoa na mahitaji yake, vile vile huwaongezea maarifa watu wasiokuwa na mawazo ya kitu chochote.

Yote hayo yoyote anaweza kuyapata kwa kujua tu wakati anazaliwa utawala wa Malaika, Majini na Sayari hiyo ulikuwa kwenye nyuzi Ngapi na katika asili ipi kisha ndio wanaweza kuvaa pete hiyo baada ya kuiosha na maji ya chumvi ya asili

MADINI YA CHUMA:

MADINI YA CHUMA



Madini haya kiroho ni mazuri sana katika ufanisi wake. Madini haya ni kuwa mwenye kuyatumia katika utawala wa sayari ya Mars (Marikh) basi hushinda kila aina ya vita anayopambana.

Ikiwa vita hiyo ni:

  • kimwili
  • kiroho,
  • mashaka yoyote,
  • akitaka mtu kuwa na nguvu maradufu hata katika mapenzi
  • kutokufanyiwa maudhi, hujuma, kuzulumiwa hovyo
  • kutendewa haki,
  • kushinda kesi,
  • kuondowa mikosi,
  • kujikinga na kuvunjika mwili
  • migogoro na dhoruba
  • majanga yoyote
  • kumkusudia mtu yoyote jambo baya.
Basi mwenye kutaka hayo na apate pete hii na aitengeneze au anunue kisha aivae kwa kufuatia siku saa na kipindi alipokuwa akizaliwa ni wapi sayari ya Mars ilikuwa na utawala wake,

Ifahamike kuwa utawala wa sayari hii upo kwa malaika wa Mwenyezi Mungu ambaye ni Samsamail au Jina jingine ni Izrael lakini kwa dini ya kiislam huitwa malaika wa mauti (wanazuoni hutofautiana katika jina lake)

Ambaye malaika huyu ni mtoa roho za viumbe basi na pia kuna jini anaesimamia hapo siku hiyo aneyeitwa Abu Muhriz Al Hamar,
na shetani wa siku hiyo waizrael humuita Phaleg hivyo unaweza kuyafanikisha hayo kwa kujua tu wakati unazaliwa Sayari ya Mars ilikuwa wapi na ndio huko huko utakuwa ukiitumia na siku zake ambazo ni jumanne mchana na ijumaa usiku,

Mfano:
Umezaliwa Jumamosi na sayari hii ilikuwa saa tatu asubuhi basi ikifika siku hiyo jumamosi saa 3 asubuhi unanuia kisha unavaa hata kwa hilo saa moja tu basi majibu utayapata kama kupepesa macho tu, isipokuwa inataka mazingatio katika maandalizi yake kulingana na sanaa yake

MADINI YA DHAHABU:

dhahabu-png.1102271


Haya kiroho hutumika kwa kupata:
  • kiburi cha mafanikio,
  • nguvu,
  • ufahari,
  • kuona haya,
  • kulegeza nyama za mwili,
  • siasa,
  • udereva,
  • utajiri wa vyombo vya moto
  • utajiri wa madini.
Pia dhahabu humsaidia mtu kupata nguvu ya roho kama roho yake ni dhaifu hasa wanawake basi dhahabu humfanya awe na nguvu katika roho yake na nafsi yake kustahimili maudhi na kusamehe,

Pia humuondolea mwanamke kulazimisha au kung'ang'ania jambo ambalo mume wake haliwezi kwa wanaume ambao wake zao hawavai dhahabu basi wajitahidi katika kuwatafutia ili wapande daraja,

Ukifanya hivyo hutakuja kuskia wala kuona mwanamke aliyevaa dhahabu anampiga mmewe au kumfokea labda kama huyo ni shetani sio mke,

Dhahabu huongeza ukarimu wa uzuri wa roho na mwili kwa mwanamke, humfanya amvutie kila anaemtazama,

Pia huongeza umoto katika sehemu za mbele na ulaini wa tupu ya mwanamke,

Malaika wa madini haya anaitwa Rukayail ambaye huusika na doria za mbinguni na jini wa sayari ya madini haya anaitwa Madh'habu na kiizrel anatambulika kama OCH

Sayari ya madini haya ni Jua/ingawa jua sio sayari lakini lugha ya kitaalamu lipo kwenye mpangilio wa sayari,

Basi ikiwa mtu anahitaji kupata moja kati ya mambo hayo nilioyaainisha hapo basi atatakiwa apate pete ya dhahabu na aivae kama nilivyoelezea hapo awali kwa waislam wanaume pete ya dhahabu ni Haramu iwe ya ndoa ama uhawara.

MADINI YA KOPA/COPPER

Pete ya kopa ina maana gani?


Haya ni madini yanayotawaliwa na malaika Anyail na Jini wa sayari ya Venus anaitwa Zawbat na shetani wake anaitwa Succubi au Succubus (Jini mahaba)

kwa yoyote mwenye kutaka mafanikio ya kimapenzi basi yoyote yale basi na atumie pete hii ya Kopa watu watampenda na kumkubali kwa kila hali.

Na hii ni kwa kufuata sharti za uvaaji wake na utendaji wake,

  • Humfanya mtu kuwa na roho nzuri
  • Humletea masikilizano maelewano na heshima kwa wote
  • Humuondoshea chuki
  • Humfanya kuwa na sauti nzuri
  • Humpatisha kila kitu kinacho mfurahisha mwanamke basi atafanikiwa,
  • Huongeza mapenzi kwa jinsia tofauti na yako
  • hukuinua juu kimuonekano
  • Hukufanya uonekana unacho hata kama unapata kwa tabu,
  • Hufanya watu wakuhurumie kwa kila hali na kukupenda pia,
  • Humfanya mtu kusifiwa na kukuthamini,
Ukichanganya hii na bati katika muundo wako, ukaweka stone ya nyota yako basi kila unalotamani utakuwa unalipata ndani ya dakika chake sana au siku chache kwa haraka kwa amri ya Mwenyezi Mungu,

Ukiitumia katika majira ya baridi na mvua basi utakuwa tajiri mwenye kujitosheleza yaani wewe akili yako unahisi ukiwa na nini utajihisi tajiri basi utapata.

Pia ukimtaka mwanamke yoyote au mwanaume yoyote yule kutoka rohoni yaani roho ikakuuma kwa heri ya kutaka kuwa naye basi utampata atakuja mwenyewe bila wewe kumuhangaikia hakikisha mnafunga ndoa au utalaanika,

Yote hayo ni kwa kufuata hawasi zake na taratibu zake na kujua nyota yako ilikuwa wapi katika sayari ya Venus(Zuhura) wakati unazaliwa

MADINI YA BRASS/SHABA

Pete ya shaba


Madini haya utawala wake upo kwa Malaika Mikaiil. Ambapo hutawala siku hiyo.
Jini wa siku hiyo huitwa Burkaan au OPHIEL kiizrael nae hutawala sayari ya Mercury.

Ambayo mtu akivaa pete hii ya Brass:

  • hupata akili nyingi na maarifa zaidi ya mtu wa kawaida
  • huwa na adabu kushinda wengine na malezi mema
  • kuwa mwenye maelezo ya kuvutia
  • kuwa mwenyemwenye kusikilizwa akiongea
  • huwa mtu fasihi zaidi ya kawaida na mwenye kupendeza na mwenye kipato cha kujitosheleza,
Lakini pia ndio madini haya ambayo mtu akiyapata na akataka kupata habari za kiroho za mtu au awe mtabibu au mganga mwenye maono sio mganga mchawi, Basi huweza kuona mengi usingizia hata kujua kesho mtu gani anakuja na atataka nini kwa idhini ya mwenyezi Mungu.

Na vilevile hutambua msaada wake ni nini, Pia hii ni nzuri kwa walimu wanaofundisha watoto ambao huwa na tabia mbovu kama:-
viburi na watukutu.

Pale anapovaa hii basi akifundisha hata watoto wasiokua na uelewa huelewa vema masomo yao na kila siku huonekana ni mwalimu mwenye kupendeka zaidi na wanafunzi,

Na pia pete hii hutumika kuchoma kuua na kutandika Majini ambao ni wakorofi wasiotaka kutoka na wenye kung'ang'ania vichwani kwa watu,
Ikiwa itatengenezwa kwa maarifa yake;

Na pia ikipanguswa usoni kwa mtu mwenye majini au mashetani au uchawi huwa anapona hapo hapo au kuanguka na hata ukiwa umeiweka mfukoni basi utayafanikisha hayo kwa kufuata sharti zake na hawasi zake.

MADINI YA SILVER AU FEDHA

MADINI YA SILVER AU FEDHA



Haya ni madini maarufu sana na hutumiwa na watu wengi sana kupita madini mengine yote na wengi huvutiwa na rangi yake na uzuri wake na pia kuiga kwamba fulani kavaa,

Haya ndio madini pekee yanayoweza kumletea mtu kinga bila kufanya chochote muda wowote saa yoyote akivaa basi anakuwa amekingwa na vijicho na mara nyingi huchafuka mara kwa mara kwa mtu anayepigwa kijicho mara kwa mara.

Bila kuguswa na mafuta wala matumizi mabaya ya mkono uliyovaa pete hiyo ya fedha. Siri moja kati ya siri za fedha ni kuwa ukivaa ikachafuka sana na baadae ikaanza kung'aa yenyewe basi kwa kipindi hicho kirefu ulichovaa huwa inakusafishia nyota yako.

Na kukuweka sawa sisemi hivi kwamba ndio masharti ya uvaaji wake nayatoa hapana kuna adabu za kuvaa silver ukikosea basi hakuna pete inaleta mikosi, nuksi, balaa, chuki, dhalau n.k

Kama hii

Fedha hutawala Mwezi yaani sayari ya Mwezi katika maarifa na pia malaika wake huitwa Jibril (Gabriel) na jini wake huwa anaitwa Marah au kiizrael huiwa PHUL

Huyu ni jini ambaye huwa hakumbi mtu wala kutesa mtu yeye na vibaraka wake au watumishi wake tofauti na wengine wote niliowataja

Na pia yeye huvuta watu kuwapeleka pale ambapo watoto wametupwa na wazazi wao na kumpulizia mtu mawazo ya wapi anaweza kukomboka kutoka katika tatizo lake na mara nyingi huwatokea watu ndotoni akiwa kavaa kanzu au mavazi meupe akiwa na umbile la kimalaika.

Wengine hudhani ni malaika na anakuwa mfupi kiasi maji ya kunde au mwarabu mwenye ndevu nyingi tu nyeupe na hata baadhi ya wakristo akiwatokea huyu huhisi wameshukiwa na roho takatifu yaani Jibril (Gabriel) kumbe ni jini.

Kulingana na muonekano mzuri anaokuwa anatumia kwa muda huo ambaye yupo chini ya uangalizi wa malaika Jibril (Gabriel) dini zote hukubali kuwa Jibril ni roho takatifu,

Basi na katika hawasi zake za kuvaa pete ya fedha;-

  • mtu anaevaa pete hiyo huwa anakuwa kajikinga na mapepo ya kukumba kichwa,
  • Humsaidia mtu kupata mawazo ya kupata riziki,
  • Humfanikishia mazao kama ni mkulima,
  • safari za mafanikio,
  • mapenzi,
  • furaha,
  • amani kupata mambo kwa kishindo na haraka na mafanikio kufanikiwa katika uongozi wa kuchaguliwa na kupata uzazi kwa wasiozaa,

Kumbuka

Yote hayo utayapata kwa haraka sana ikiwa tu utavaa pete hiyo siku ya kwanza iwe ni siku sahihi na saa sahihi ambapo wakati unazaliwa mwezi ulikuwa wapi siku ngapi na ulikuwa vipi basi kila siku utaona maisha rahisi sana.

Lakini kupata kinyume chake ni rahisi na haraka sana kwa wasiokuwa na maarifa.

Hadi kufikia hapa makala yetu imeishia hapa mwenye swali anaweza kuuliza kwenye comment section chini
Kuhusu stone hizo maelezo yake hayana tofauti sana na ya madini haya isipokuwa kwa stone lolote unalotaka unaweza kupata kwa stone yoyote hapo kila kitu utapata ila tu kwa kufuata masharti yake na usawa wake,

kuna stone hapo ukivaa kwa kukosea kufungwa jela wewe ni kugusa tu, na kuna nyingine ukivaa hapo utajiri kwako ni kama kupepesa macho tu,kila unalotaka uaweza kupata kuna zingine ukizichanganya vibaya na madini yake hapo utajikuta kwenye wakati mgumu hata kubakwa na watu au majini.

Angalizo:​

Jiepusheni sana wanaume kuvaa dhahabu kwa maana hizi mila za kuvaa dhahabu kindoa ni za wenzetu waliokosa tamaduni na nidhamu za kiroho hivyo kuvaa dhahabu kunalainisha na kulegeza maumbile.

Ndio maana maumbo ya wanaume wengi waliooa na wanavaa dhahabu ngozi zao huwa zimetepeka hasa mkono wa kushoto na kuleta usoft uliopitiliza hivyo jiwekeni mbali na mambo msioyafahamu

wala kuwa na maarifa nayo, ndio maana ndoa nyingi leo zinayumba kwa maana mke akiongea na wewe unashindana nae kike kwa masuala haya ambayo mtu anakuwa hana maarifa nayo.

Ijulikane kuwa effect za pete hizi zinafanyika siku na saa hiyo hiyo uliyovaa na athari yake itadumu kwa muda mrefu sana hadi ujioshe ndio utaona athari yake imekuondoka,

Usione ajabu leo kumuona mume anafokewa na mkewe analia wewe muangalie tu kidoleni utapata jibu.

FAIDA
Nyota ni kitu kikubwa sana kwenye mambo ya kiroho wengi wanahangaika bila kufanikiwa kiroho kwa kutokujua tu nyota zako.

Nyota zile mnazoona kwenye magazeti kama nilivyoeleza hapo awali hizi mnazoona kwenye magazeti na miezi ya makadirio ya kuzaliwa ni 49% huwa zinawapatia watu wachache muongozo wengine wote hola

Wasiliana nasi​

Ikiwa ni mwenye kupendezewa na makala hizi, basi jihisi huru kuendelea kutufuatilia kupitia email lakini pia kama unahitaji mawasiliano yetu, tunapatikana kwa ajili ya misaada ya mfano wa makala hizi.

Unaweza kutupata kwa kupitia Email, vile vile kwa namba za simu, kupitia fomu ya mawasiliano katika tovuti yetu. Msaada wa kirafiki zaidi unatolewa na team yetu ya huduma kwa wateja na kujibu maswali yoyote ambayo unaweza kuwa nayo,

Ikiwa una maswali kuhusu makala zetu pia unaweza kuacha kwenye comment katika makala husika na kama ni huduma ya msaada wa tiba za kiroho au ushauri ama unahitaji kuagiza ama una suala lolote lingine basi tupo kwa ajili ya kutoa msaada pia.

Usisite kuwasiliana nasi kwa hekima za mawasiliano nifuraha yetu kusikia mahitaji ya wateja ama rafiki wa tovuti zetu za unajimu na RakimsSpiritual na tunatoa huduma nzuri za kumridhisha mwenye shida ikiwa tu atakidhi vigezo vya kuwa mteja ama rafiki wa tovuti hizi asante.

Na kwa maswali ya dharula kuhusiana na makala zetu kwa Members pekee;

Jihisi huru kututafuta masaa 24 ya week kupitia:-

Rakimsspiritual@gmail.com
au
mnajimu@unajimu.com

WhatsApp number

+255 783 930 601

Rakims
 

Attachments

  • s-l300.jpg
    s-l300.jpg
    13.6 KB · Views: 749
  • lead-finger-ring-for-reduce-weight-250x250.jpg
    lead-finger-ring-for-reduce-weight-250x250.jpg
    7.9 KB · Views: 579
  • celtic-tin-bracelet.jpg
    celtic-tin-bracelet.jpg
    14.1 KB · Views: 597
  • engineer-ring-iron-ring-enginneers-stainless-steel-iron-rings.jpg
    engineer-ring-iron-ring-enginneers-stainless-steel-iron-rings.jpg
    12.4 KB · Views: 642
  • dhahabu.png
    dhahabu.png
    114.6 KB · Views: 668
  • kopa.jpg
    kopa.jpg
    25.3 KB · Views: 670
  • blass.jpg
    blass.jpg
    5.1 KB · Views: 589
  • silver.jpg
    silver.jpg
    25.1 KB · Views: 628
Somo zuri sana, endelea kushusha nondo Mkuu. Sikuizi wa vaa mapete wamekua wengi kweli unakuta mtu anapete nne za rangi tofauti na wengi hawajui maana yake ikiwemo mie. Nazani kwa elim hii tutakua tumejifunza kitu
 
Somo zuri sana, endelea kushusha nondo Mkuu. Sikuizi wa vaa mapete wamekua wengi kweli unakuta mtu anapete nne za rangi tofauti na wengi hawajui maana yake ikiwemo mie. Nazani kwa elim hii tutakua tumejifunza kitu
Na itakuwa umefunguka sana mkuu wacha siku ikae sawa niendeleze somo,

Rakims
 
Dunia hii inaaminika kuwa iliubwa kwa Mawe au kauli za Mwenyezi mungu au kwa wasioamini uwepo wa roho pia wao husema kuwa Dunia ni mkusanyingi wa elements mbalimbali ambazo zilijichanganya na kufanya Creation ya viumbe,

Nachochukua kutoa hapo sehemu zote 3 mean kwamba (Islam/Christian & pagan)
Ni elements

Elements zipo katika sehemu 4 ambazo ni:

*moto
*upepo
* Maji
*udongo

Sisi tunaoamini katika dini na Mwenyezi mungu tunaongeza moja Ambayo ni

*roho

Hivyo inakuwa

*moto
*upepo
*Maji
*Udongo
*roho

Hivyo kwa mpangilio huo tu tunaonakwamba

Huwezi kupata udongo bila roho? Sawa sawa?
Huwezi kupata Maji bila udongo!

Huwezi kupata upepo bila maji!

Na huwezi kupata chochote kile bila Chanzo!

Hata kazi huwezi kupata bila elimu,

Naimani tupo pamoja hadi hapo,

Sasa sisi teyari ni roho za Muumba wetu na pia ili tuweze kufika popote pale tunapotaka kwenda lazima tufuate vema safari tunayoenda bila kukosea hatua moja, ili mwisho wa siku tuweze kurudi kuwa roho bila kukosea na kutokukwamia kwenye moto(maybe hell will help you to understand)

Ur source is Spirit and your end is Spirit if your end is in fire that's your choice,

Kwamba:
"Chanzo chako ni roho na mwisho wako ni roho kama utaishia Motoni hayo ni machaguo yako"

Kidogo hapa ulianza kutoa somo na kueleweka

Kwengineko ni ushirikina mtupu
 
Yeah, kila mtu huhisi anachotaka na kukubaliana na akili yake thread haijafika hata robo umeshaona ushirikina,

Rakims
Nilitaka nipate nyama za kuongezea kidogo kutoka kwako kuhusiana na four Elements ulizogusia

Sasa sijui umeharakishwa na nini..!? Unarukaruka Tu..!?
Screenshot_20181030-151900.jpg
 
Kiswahili ni lugha nzuri sana lakini uswahili ndio huwa unaleta mitihani na kupoteza watu
Ucha Mungu ndio chanzo cha maarifa na maarifa Mengi ndio mwanzo wa ushirikina

Tuendelee na somo.........
 
Back
Top Bottom