Polisi na mauaji ya kinyama Kigoma

Polisi na mauaji ya kinyama Kigoma

Sijaona hapo viongozi wa kata wakiongea, wao si ndio waliomuita? au walimuita bila kujua polisi wanaishu gani naye? Na kama walijua si mhalifu kwa nini hawakumtetea wakati anaadhibiwa? Mi naona viongozi wa kata walikuwa waoga mno kiasi cha kushindwa kumtetea innocent people like Festo.
Hili tatizo la uoga limesababisha na litasababisha vifo vingi sana kama hatutabadilika.
 
Naomba sana mnielewe naona mpka sasa mnanirushia shutuma na kunishambulia mimi binafsi, hakuna mahala nimeunga mkono hili la polisi kuuwa na au kutesa, si ubinaadam na kazi yao ilikuwa ni kuchunguza kumpeleka mtuhumiwa mahakamani akahukumiwe.

Nnachosemama mimi ni kuwa hata Raia huwa wanafanya mateso na hadi mauaji kwa wizi hata wa "kufuli" tu na Polisi hawawafanyi lolote hawa Raia wauaji, hawaedeshi uchunguzi wala hatujasikia kushikwa mtu kwa mauaji, Jee, katika hali kama hiyo mnategemea nini kutoka Polisi? mimi sitegemei zaidi wala sioni ajabu ya hawa Polisi kuyafanya waliyoyafanya. Ikiwa Raia wanafanya na kila kitu shwari, utegemee nini kutoka Polisi?

kwa jinsi ulivyowakilisha hiyo hoja yako, ni wazi kabisa utashambuliwa na wadau.
 
Wewe Mama kweli una roho mbaya!
Duuh!
Toka lini mtu ambaye bila hata haya anakiri hadharani kuwa ni mwana CCM akawa na roho nzuri ? Tazama mwenyekiti wao anavyokwapua hadi uji wa mgonjwa ! FaizaFoxy anayo kazi moja, kuutetea utawala wa Kikwete. Tazama anaanza kudai vitendo vya polisi wetu visihusishwe na utawala huu wa kijambazi. Anasahau kuwa hata hao raia anaodai kutenda anayosema hawangefanya hayo kama tungekuwa na utawala madhubuti unaoheshimu sheria. Watu kama FaizaFoxy ndiyo hao wamesaidia kulifikisha taifa hapa lilipo na walivyo na akili mbovu hawajui kila wanachokiandika humu JF, watasoma hadi vijukuu wao na si ajabu huko mbele ya safari moja wao akajiuliza, "hivi huyu bibi yangu alikuwa na akili timamu kweli ?"
 
Polisi wanafanya kazi ndani ya mfumo fulani, makosa waliyofanya Polisi hao wa Kasulu ni matokeo ya mfumo mbaya wa utendaji kazi. Hili Jeshi livunjweeee!!
 
Ngoja nipite Kimya nisije pigwa ban.
 
Wote waliofanya wamelaaniwa tayari,huu ni unyama jamani ndugu,sina hata maneno ya kusema,faiza please please usitafute laana uwe unasoma 2 usicoment post kama hzi,kwa nini unaniharibiaga mood hivi?
 
Ngoja nipite Kimya nisije pigwa ban.
 
Unazidi kujidhalilisha wewe na chama chako...

Kwasababu polisi huwa wanuwa raia wema na majambazi ya kweli yanaachiwa kwsababu huwa yanakula na polisi, so ndiyo maana wananchi wanajichukulia sheria mkononi kwasababu hiyo hiyo ya kwamba haki haitatendeka wakipelekwa polisi...

Wewe kama si kuwa una type Kiswahili humu,ni na doubt sana utanzania wako!
 
Nakuambia badala ya kunishambulia mimi, shambulia hoja zangu, Jee, Raia hawaui wizi mitaani? hujasikia? hujaona au unajifanya punguani?

Huna hoja,hebu nieleze polisi ambaye nilazima amehudhuria mafunzo rasmi na raia wa kawaida ni nani anapaswa kumuongoza mwenzie?So ni sawa kwa polisi kuwa influenced na raia wa kawaida??!!
 
Kazi ya Polisi ni nyingi sana, na mojawapo ni kukamata watu na kuwapeleka katika vyombo vya sheria, hiyo pia ni kazi ya Raia yoyote mwema, kwanini iwe makubwa kwa Polisi na iwe madogo kwa Raia anayeuwa Raia mwenzake? Jee, Raia wanaouwa wapo juu ya sheria? halafu soma vizuri hiyo makala "ofisi ya kata walimfungia chumbani", toka lini ofisi za kata zimepewa majukumu ya kufungia watu?

Tatizo lenu mkiona jina la FF huwa hamsomi hata anachokiandika huwa mnakurupuka, someni mpate faida.
Sheria inasema wazi..

"Allegedly" got to prove it beyond reasonable doubt,mahakama ndiyo yenye kuamuwa...

Ila bongo tofauti, hakuna utawala wa kisheria.

Kwani raia wakiuwa basi polisi na ndo wauwe? unanishangaza sana kwa namna unavyofikiri,yani unable to clasify you...
 
Huna hoja,hebu nieleze polisi ambaye nilazima amehudhuria mafunzo rasmi na raia wa kawaida ni nani anapaswa kumuongoza mwenzie?So ni sawa kwa polisi kuwa influenced na raia wa kawaida??!!

"Asiyeelewa maana haambiwi maana" lakini utanielewa tu, hata kama ni punguani; nnachosema mimi ni kuwa ikiwa hao polisi wanashindwa kuwachukulia hatua hata Raia wa kawaida wanaouwa watuhumiwa wa wizi kila siku, Jee, kwanini iwe ni ajabu kwao kuuwa mtuhumiwa wa ujambazi?
 
Sheria inasema wazi..

"Allegedly" got to prove it beyond reasonable doubt,mahakama ndiyo yenye kuamuwa...

Ila bongo tofauti, hakuna utawala wa kisheria.

Kwani raia wakiuwa basi polisi na ndo wauwe? unanishangaza sana kwa namna unavyofikiri,yani unable to clasify you...

Unajifanya hunielewi lakini unanielewa sana, nnachosema mimi ikiwa Raia wanauwa watuhumiwa wa wizi kila siku na hakuna tunapoona au kusikia Raia wahalifu wauwaji wa watuhumiwa wa wizi wakichukuliwa hatua, utegemee nini?

Halafu nasema, ikiwa kuna watu wanasema hao Polisi ni wa CCM , Jee na hao Raia wanaouwa watuhumiwa wa wizi ni wa vyama vipi na kwanini hawachukuliwi hatua za kisheria?
 
naona badala ya kuzisoma hoja zangu unataka kujuwa uhalisia wangu, unahusu nini? Soma vizuri hoja zangu, labda utanielewa. Sasa nataka ujiulize swali moja, hujawahi kuona watoto wadogo wanatishiwa "kama haujala tutakuitia polisi" jiulize kwanini inafikia kama hivyo kwa walinda usalama?
wanaogopa kuwekewa vijiti kwenye masaburi
 
Unazidi kujidhalilisha wewe na chama chako...

Kwasababu polisi huwa wanuwa raia wema na majambazi ya kweli yanaachiwa kwsababu huwa yanakula na polisi, so ndiyo maana wananchi wanajichukulia sheria mkononi kwasababu hiyo hiyo ya kwamba haki haitatendeka wakipelekwa polisi...

Wewe kama si kuwa una type Kiswahili humu,ni na doubt sana utanzania wako!

Hapo ndipo mnapokosea, chama kinahusu nini? Jee, na wale Raia wanaouwa mitaani wanapomkamata mtuhumiwa wa wizi huwa ni wa chama kipi? Kuweni wa kweli wa nafsi zenu kwanza kabla hamjakurupuka.
 
Unazidi kujidhalilisha wewe na chama chako...

Kwasababu polisi huwa wanuwa raia wema na majambazi ya kweli yanaachiwa kwsababu huwa yanakula na polisi, so ndiyo maana wananchi wanajichukulia sheria mkononi kwasababu hiyo hiyo ya kwamba haki haitatendeka wakipelekwa polisi...

Wewe kama si kuwa una type Kiswahili humu,ni na doubt sana utanzania wako!

Ikiwa wewe unaejifanya hujui kuwa Watanzania wanauliwa kila kukicha kwa kuiba "kufuli" au kuku tu unajifanya Mtanzania, ni Mtanzania yupi asiyeyajuwa hayo? au hayo ni vyema yakafungiwa macho?
 
Kilichonishangaza kwenye kadhia hii ni vile wananchi walivyokuwa wakiangalia live jinsi vijana wale walivyokuwa wakiteswa hadharani tena bila nguo na wao kunyamaza kimyaa. Angalau wangepiga kelele za kulalamikia uonevu.

Namhurumia zaidi huyo mzee wa hao vijana alipokuwa akiangalia mateso ya watoto wake. Mungu awalaani hao watesaji hapa hapa duniani.
 
Back
Top Bottom