DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limewatia mbaroni watu 116 wanaodaiwa kuratibu mipango ya kufanya maandamano yasiyo rasmi tarehe 9 Desemba mwaka huu, tukio linalotajwa kuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani.
Akizungumza na Wanahabari, Desemba 6, 2025 katika kituo kikuu cha Polisi kilichopo Wilaya ya Nyamagana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbrod Mutafungwa, amesema upelelezi dhidi ya watuhumiwa hao unaendelea, huku jeshi hilo likiimarisha doria katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha Mkoa wa Mwanza unabaki kuwa salama.
Aidha, Kamanda Mutafungwa ametoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha vijana hawashiriki katika maandamano hayo, akisisitiza kuwa siku ya Desemba 9 itumike kama kumbukizi ya Tanzania kupata uhuru wake, badala ya kusababisha uvunjifu wa amani.
“Imeshatolewa taarifa rasmi kuwa maandamano hayo yamekatazwa. Tunawaomba wazazi kuzuia watoto wao kujiingiza katika maandamano hayo. Badala yake, makundi yote ya kijamii yashirikiane na Serikali kudumisha amani na utulivu katika siku hii muhimu ya kumbukizi ya uhuru wa nchi yetu,” amesema Kamanda Mutafungwa.
Kamanda huyo amesema hatua hizo ni mwendelezo wa jitihada za Jeshi la Polisi mkoani humo katika kulinda mali na usalama wa wananchi, ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea kama ilivyoshuhudiwa kwenye vurugu za maandamano yaliyotokea wakati wa uchaguzi wa Oktoba 29 mwaka huu.