Mwili
wa marehemu Mwalimu Casto Sote Kawamba aliyepigwa risasi na Askari wa
Jeshi la Polisi
ASKARI wa Jeshi la Polisi amemuuwa Mwalimu wa Shule ya Sekondari Kitulo
Wilayani Mkete kwa kumpiga risasi mgongoni kwa madai kwamba mwalimu
huyo alikuwa akiendesha Pikipiki bila kuvaa Helment (Kofia ya kuendeshea
Pikipiki).
Akizungumza na
Habarimpya.com kwanjia ya simu Kamanda wa Mkoa wa
Kipolisi Makete Peter Kaiza alimtaja marehemu kuwa ni casto sote
kawamba na kusema kwamba tukio hilo lilitokea karibu na Benki ya NMB
tawi la Makete.
"Mwalimu huyo alikuwa anakwenda kupata huduma za kibenki kupitia
mashine ya kutolea pesa ya ATM akiwa na pikipiki ndipo alipo amuliwa na
Askari mmoja aitwae Jose Msukuma ili asimame kabla ya kukutwa na umauti
huo .
"Kamanda Kaiza alisema kwamba kifo cha mwalimu huyo inadaiwa kuwa ni
kutovaa kofia hiyo na baada ya kuitwa na Askari huyo alikaidi amri na
kutaka kumgonga askari huyo aliye kuwa lindo.
Nae mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Makete Idd Nganya ambaye
ndie mwajiri wa marehemu amesema kuwa mwili wa marehemu bado
umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya makete wakati utaratibu
wakusafirisha mwili huo kwenda kwao Mkoani Mbeya kwa ajili ya mazishi
ukiendelea
Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Makete Dk Michael
Gulaka alisema kwamba walipokea mwili wa marehemu ukiwa na majeraha ya
risasi mgongoni na si kwamba marehemun alimpokea akiwa hai kama
inavyodaiwa na baadhi ya watu
KWA HISANI YA HABARI MPYA.COM