Polisi Makete waua mteja wa benki

Polisi Makete waua mteja wa benki

Polisi Tanzania viroba na ganja vitawaponza!
 
wanainchi sasa kilichobaki ni kujilinda wenyewe hii dhana aliyokuwa nayo huyu police ya kudhani ni jambazi huenda ipo kwa wengi wao, hatari sana!
 
Tatizo wanapeleka watoto waliotoka depo kulinda hizi benki. Ukitaka kujua kwamba jamaa wametoka shule ya upolisi na uzoefu sifuri angalia askari yoyote mwenye Nambari za G au H ....kuwa nao mbali kwani busara huwa sufuri!
 
Huko CCP sasa hivi kunamafunzo mapya?

Umeona eeh....

Kwanza naona kuna somo jipya la kutwanga raia, pili shabaha zina-diverge, miguu inakuwa kifua!
 
Duh!ina maana polisi cku hizi wamegeuka majambazi!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Eti nimekosea..!

Umekosea??

Na uhai wa huyo vipi,he must be so so craizy..
 
theni wakampora money nini? tukisema polis ni kama robot iliyokuwa programmed mnabisha...hao walikuwa wanalinda hela tu na sio usalama wa raia na mali zao. rip
 
IMG_0016.JPG
IMG_0027.JPG

Mwalimu mmoja wa shule ya sekondari kitulo wilayani makete aliyefahamika kwa jina la casto sote kawamba ameuawa kwa kupigwa risasi na askari wa jeshi la polisi Makete

Akizungumza na mtandao huu wawww.francisgodwin.blogspot.com mkuu wa polisi wilaya ya Makete SP Peter Kaiza kuhusu tukio hilo lililotokea eneo la benki ya NMB tawi la Makete jana majira ya saa moja na robo alisema kuwa mwalimu huyo alikuwa anakwenda kupata huduma za kibenki kupitia mashine ya kutolea pesa ya ATM akiwa na pikipiki ndipo alipo uwawa na askari mmoja aitwae Jose Msukuma na kukutwa na umauti huo .

Inadaiwa kuwa kisa cha mauwaji yake ni madai kutovaa kofia hiyo na baada ya kuitwa na askari hao alikaidi amri na kutaka kumgonga askari huyo aliye kuwa lindo.

Nae mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Makete Idd Nganya ambaye ndie mwajiri wa marehemu amesema kuwa mwili wa marehemu bado umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya makete wakati utaratibu wakusafirisha mwili huo kwenda kwao mbeya kwa ajili ya mazishi ukiendelea

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye jina lake limehifadhiwa amesema kuwa askari hao walikuwa wakiomba fedha kwa mwalimu huyo na baada ya kukataliwa ndipo walipo anza kumshushia kichapo na alipo wazidi walilazimka kutumi asilaha na kumpiga begani kwa risasi

Walimu wenzake na marehemu ambao walifika hospitali kujua kuhusina na kifo cha mwalimu mwenzake wameeleza kusikitishwa na tukio hilo na kulifananisha na tukio la kikatili machoni pao.

Mganga mkuu mfawidhi ambaye ni msemaji wa hospitali ya wilaya ya makete Dr Michael Gulaka amesema kuwa wao walipokea mwili wa marehemu na sio majeruhi.

IMG_1985.JPG
[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD]Askari wa FFU mkoani Iringa wakimwadhibu kwa kipigo
aliyekuwa mwandishi wa Chanel Ten mkoa wa Iringa
marehemu Daudi Mwangosi (wa pili kushoto) kabla ya
kuuwawa kwa bomu septemba 2 mwaka 2012 katika
kijiji cha Nyololo Mufindi.(picha na maktaba ya mtandao huu)

[/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD]

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
.....................................................................................................................................................................
WAKATI mtuhumiwa wa mauwaji ya aliyekuwa mwandishi wa kituo cha runinga cha Chanel Ten mkoani Iringa Daudi Mwangosi Daudi Mwangos, askari wa FFU mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23) akitarajiwa kufikishwa tena mahakamani leo kwa kesi hiyo kutajwa ,askari wilaya ya Makete mkoa wa Njombe wadaiwa kufanya mauwaji ya kinyama kwa kumpiga mteja wa benki ya NMB kwa risasi. Huku askari askari mmoja nayetuhumiwa kufanya unyama huo akishikiliwa na jeshi la polisi kufuatia mauwaji hayo ya kinyama.

Tukio hilo limekuja huku bado watanzania hasa wakazi wa mikoa ya Iringa na Njombe wakiwa bado hawajasahau mauwaji ya kinyama yaliyomkuta mwanahabari Daudi Mwangosi ambapo kesi hiyo bado ikiendelea kutajwa na wanahabari waliokuwepo eneo la tukio siku ya mauwaji wakisubiri kuchukuliwa maelezo yao kama mashahidi wa kesi hiyo pindi itakapoanzwa kusikilizwa.

Mwandishi wa wetu wa mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kutoka Makete Njombe anaeleza kuwa tukio hilo wamedai kuwa mauwaji hayo ya kinyama yametokea jana jumatano majira ya saa 1.20 usiku baada ya mteja huyo aliyekuwa na usafiri wa boda boda kufika eneo hilo la benki kwa lengo la kuchukua fedha .

Imedaiwa kuwa aliyepigwa risasi anatambuliwa kwa jina la Casto Kawambwa mkazi Mbalizi mkoani Mbeya na kuwa baada ya kupigwa risasi alikimbizwa katika Hospitali ya wilaya ya Makete ambako inadaiwa kabla ya kupatiwa matibabu amefariki dunia .

Kutokana na tukio hilo jeshi la polisi liliwazuia wanahabari kutimiza wajibu wao kwa kupiga picha wala kusogea eneo hilo la Hospitali na badala yake kuweka ulinzi mkali eneo hilo la Hospitali ili kuzuia wanahabari kusogea eneo hilo .

Hata hivyo mmoja kati ya askari ambae jina lake halikufahamika mara moja alisikika akidai kuwa chanzo cha mteja huyo wa benki kupigwa risasi alikuwa akihisiwa kuwa ni jambazi na hivyo baada ya kufika eneo hilo kwa usafiri wake wa piki piki (boda boda ) walihisi kuwa amefika kwa ajili ya kufanya vitendo vya uporaji katika benki hiyo na hivyo askari katika hali ya kujihamia aliamua kumpiga risasi .

Jitihada za kumtafuta kamanda wa polisi wa mkoa wa Njombe ili kuzungumzia undani wa tukio hilo linafanyika na mtandao huu.

Hisani ya Mzee wa Matukio daima




Aaah ukatili kama huu hauvumiliki hata kidogo..

Huyu mwanadam mwenzetu hana kosa lolote,huyo polisi aliyehusika na kifo hiko na yeye pia auliwe..

Kisasi ni haki,alieua lazima pia nae auliwe...

Watashika adabu zao tuh hawa..
 
Utawasikia tu " Ririambiwa risimame rijisarimishe rikakataa"
 
Mungu wangu jamani yaani mtu anaenda kuchukua fedha yake kwenye ATM anapigwa risasi?Kama walihisi ni jambazi kwanini wasingemdhibiti na kumuweka chini ya ulinzi?Kwa staili hii Tanzania si mahala salama pa kuishi tena.
 
So sad, jamani hawa mapolice wetu sasa hivi wanatisha sana, badala yakuwa kimbilio la wananchi wamekuwa wauaji wawananchi!
 
pOLIS wanaolinda bank usiku wanajigeuza trafick baada ya kufanya kazi ya kulinda Bank. Kuna siku moja walinisimamisha pale Posta wakajianya nimevunja sheria nikawakomalia wakaniachia. Ukiwa na gari jamaa anasimama mbele yako na kukunyoshea mtutu.
 
Mawenge ya bangi lindoni hayo...*%$#@&*@^#
 
hawa mapolisi wamekuwa hatari kuliko zaidi ya majambazi,R.I.P brother
kwanza majambazi walio wengi ni Polisi!! Amini usiamini ndugu! Pia ndo wafadhili waku wa ujambazi!! Imeniuma sana!! R.I.P Mwalimu!!!
 
Ole wao wote waliowakabidhi hawa vijana mitutu iliyonunuliwa kwa kwa kodi za marehemu baba/babu zao kuja kutuua ambao tumekufa tayari...ole wao waliowatuma kuja kuchuma dhambi...R.I.P uliyekwisha kulala mauti na poleni ndugu,jamaa na kila aliyeguswa kwa namna moja ama nyingine...
 
Back
Top Bottom