Polisi Makete waua mteja wa benki

Polisi Makete waua mteja wa benki

Alienda kuchukua pesa,polisi aliyekuwa lindo kama saa moja na robo usiku akamsimaisha kwa kuendesha pikipiki bila helmet.Yakatokea mabishano na hapo polisi akamlipua.
Siijui namna ya kueleza zaidi kwani hata mimi roho inauma habari zaidi soma Francis Godwin Mzee Wa Matukio Daima
 
Polisi walikuwa wanalinda benki. Sasa mwendesha pikipiki asiye vaa helmet na ulinzi wa benki vyakutana wapi? Haya
 
Mungu tunaomba umwinue yule atakaye watetea wanyonge. Damu hii ikalipwe na yule aliyeutoa uhai
 
"Ukihisiwa"jambazi hukumu yake kumbe ni kuuawa kwa risasi hapa Tanzania!Bunge lilitunga na kupitisha lini huu mswaada na Rais alisaini lini kuwa sheria¿Wazee wa "intelejinsia"kweli hamnazo kabisa!
 
Polisi walikuwa wanalinda benki. Sasa mwendesha pikipiki asiye vaa helmet na ulinzi wa benki vyakutana wapi? Haya

Askari epukeni kutumia nguvu za ziada.
Nanyi raia epukeni kugombana na askari hasa mwenye silaha huruhusiwi kugusa kofia au bunduki au hata mkanda wa police, msiendeshe vyombo vya moto kwa mbwembwe maeneo ya benki maana askari akiwa kwenye lindo hupewa risasi sio kwa ajili ya kuua nyati
 
Siku hizi polisi akikuhisi kuwa ni jambazi anakuwasha risasi,mbona tutakwisha!

tena sio anakuwasha risasi kwa sababu wewe ni jambazi ila kwa sababu anataka achukue mihela ambayo atahisi unayo na huwa anawaza hili jitu litakuwa na kuanzia mamilioni.

hawa ndio polisi wa baba riz wanajua kuua na kuchukua mali kama ule wakati wa ukuaji wa empires yani ni kuua na kupokonya na kujilimbikizia chochote kitakachopatikana.
 
hawa ndio polisi wa baba riz wanajua kuua na kuchukua mali.
yani polisi hajui kulenga? halafu sheria yetu ndio inasema ukimuhisi tu mtu kuwa ni jambazi ndio umuue?
watanzania tuna kazi kubwa sana.
 
Inaumiza sanaaaaa, mtasema chadema ndio wamemua.....

( akili ndogo kutawala akili kubwa by mch msingwa)

~ Police wana hali mbaya sana kipesa, vijini na mikoan ni wababe sana, wanatisha wananchi na kudhulu mali zao na uchafu kibao
~ Cha msing afande huyu aliyefanya uchaf huu atendewe haki yake ilikusafisha jeshi la police..... lakin sitachezeshwa danadana tu hapa ( TUSUBIRI)
 
Polisi wameacha kutimiza majukumu yao ya ulinzi na usalama, wamegeuka kuwa wahalifu wakubwa.
Sifa za polisi wa Tanzania ni ulevi, ufuska, wizi, ujambazi, utapeli na uuaji.
 
Kwa mtindo huu basi hakuna haja ya ATM kwamana tutakwisha sasa! Au ni wivu wa askari kuona jamaa kaja kuchukua zake akatanue na yeye kubaki mlinzi na baridi likimpiga!!!.

Tena inaweza kuwa wamesubiri achukue hela kwenye ATM wakamlima risasi na wakachukua hizo pesa, siku hizi polisi wanafanya ujambazi pia.
 
Askari epukeni kutumia nguvu za ziada.
Nanyi raia epukeni kugombana na askari hasa mwenye silaha huruhusiwi kugusa kofia au bunduki au hata mkanda wa police, msiendeshe vyombo vya moto kwa mbwembwe maeneo ya benki maana askari akiwa kwenye lindo hupewa risasi sio kwa ajili ya kuua nyati

IMG_0016.JPG
IMG_0027.JPG


Mwalimu mmoja wa shule ya sekondari kitulo wilayani makete aliyefahamika kwa jina la casto sote kawamba ameuawa kwa kupigwa risasi na askari wa jeshi la polisi Makete

Akizungumza na mtandao huu wawww.francisgodwin.blogspot.com mkuu wa polisi wilaya ya Makete SP Peter Kaiza kuhusu tukio hilo lililotokea eneo la benki ya NMB tawi la Makete jana majira ya saa moja na robo alisema kuwa mwalimu huyo alikuwa anakwenda kupata huduma za kibenki kupitia mashine ya kutolea pesa ya ATM akiwa na pikipiki ndipo alipo uwawa na askari mmoja aitwae Jose Msukuma na kukutwa na umauti huo .

Inadaiwa kuwa kisa cha mauwaji yake ni madai kutovaa kofia hiyo na baada ya kuitwa na askari hao alikaidi amri na kutaka kumgonga askari huyo aliye kuwa lindo.

Nae mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Makete Idd Nganya ambaye ndie mwajiri wa marehemu amesema kuwa mwili wa marehemu bado umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya makete wakati utaratibu wakusafirisha mwili huo kwenda kwao mbeya kwa ajili ya mazishi ukiendelea

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye jina lake limehifadhiwa amesema kuwa askari hao walikuwa wakiomba fedha kwa mwalimu huyo na baada ya kukataliwa ndipo walipo anza kumshushia kichapo na alipo wazidi walilazimka kutumi asilaha na kumpiga begani kwa risasi

Walimu wenzake na marehemu ambao walifika hospitali kujua kuhusina na kifo cha mwalimu mwenzake wameeleza kusikitishwa na tukio hilo na kulifananisha na tukio la kikatili machoni pao.

Mganga mkuu mfawidhi ambaye ni msemaji wa hospitali ya wilaya ya makete Dr Michael Gulaka amesema kuwa wao walipokea mwili wa marehemu na sio majeruhi.
soma kwenye red.
tutaishi vipi na hawa polisi wetu, kiasi cha mshahara wa mwalimu si mnaujua?
 
hawa mapolisi wamekuwa hatari kuliko zaidi ya majambazi,R.I.P brother
 
Back
Top Bottom