Polisi kukosa camera, ni ujinga, uzembe au umaskini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi kukosa camera, ni ujinga, uzembe au umaskini?

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Mnyamahodzo, Aug 2, 2011.

 1. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #1
  Aug 2, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Ukiwapa taarifa Polisi kuwa mahali fulani kuna maiti, kauliwa au kajinyonga, watakuja kichwakichwa bila ya note book ya kuweka michoro wala camera. Watakachokumbuka ni gloves tu. Hivi kwa wao kutokubeba camera ni ujinga, uzembe au umaskini wa Jeshi hilo kutokuwa na camera hata katika ofisi ya Polisi ya wilaya?

  Swali hili lilipata nguvu kubwa sana wiki chache zilizopita baada ya kuangalia kipindi cha "Crime investigation" ktk Discovery channel. Nikiwa nyumbani kwa mwenyeji wangu nalipata fursa kuangalia kipindi hicho pamoja na shemeji yake mwenyeji wangu ambaye ni Pathologist huko Uganda. Katika maongezi baada ya habari hiyo Daktari huyo aliniazimisha kwa siku 2 kitabu cha " Concise Text and Manual of FORENSIC MEDICINE, MEDICAL LAW and ETHICS IN EAST AFRICA". Ndani yake nilikutana na mambo mazuri na mengine ya kustaajabisha. Zipo kurasa nilipiga-copy.

  Katika Section C (Forensic Pathology) Chapter 1,2 & 3 zimeandikwa na watanzania. Katika Chpt 3, Dr Ahmed Makata (wa Wizara ya Mambo ya Ndani) na Dr Martin Mbonde (wa MUHAS, aliyetoa ushahidi wa postmortem katika kesi ya Zombe) wameandika mambo ambayo hadi sasa sijaona kufanywa na Jeshi la Polisi wanapokwenda kuichukua miili ya maiti mbalimbali huku mitaani, barabarani au ktk fukwe za mito, maziwa au bahari. Nanukuu "It is the role of the scene of crime officer to assess situations in which a visit to the scene by a medic is most relevant. Whenever there is apparent inconsistency between the state of the body and the situation at the scene, it is prudent for the scene crime officer to involve the medic rather than risk losing evidence or creating artifacts. Where the medic cannot visit the scene, a detailed and accurate recording of the status of the scene of crime should be done, including the use of sketches, diagrams, still photographs and even video recording."
  Picha zinatakiwa kupigwa kabla ya mwili kunyanyuliwa au kugeuzwa. Na kila unapogeuzwa picha inabidi zipigwe, mazingira nayo yapigwe picha.Na mambo kadhaa wa kadhaa.
   
 2. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #2
  Aug 2, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Neno ujinga nilivyolitumia hapojuu ninamaanisha "kutokujua, kukosa maarifa."
  Sasa kama hawajui, huko CCP wanajifunza nini ili iwasaidie kutunza ushahidi? Katika kesi ya Zombe, umewahisikia picha toka msitu wa pande au kule Sinza zilitolewa kama ushahidi? Hivi Polisi binafsi anakatazwa kutumia camera yake binafsi in-case kituo chake hakina? Je! Polisi wanazo strong rooms za kuhifadhi picha za matukio mbalimbali ktk kila vituo vya wilaya na mikoa? Dr Makata yuko huko Wizara ya Mambo ya Ndani, je anawafundisha hiki alichoandika?
   
 3. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0

  Bado wanaendesha jeshi kwa style ya karne ya 19. Huwa sometime najiuliza kama hawa viongozi wa Polisi wannaagalia zile documenray za CSI na kujifunza kitu. Au ni kufanya kazi kwa mazoea tu.


  Yaan kuna vitu vingine wala haviitaji gaharama kubwa. Ni maamuzi tu na nia. Japo zile documenryza CSI nazo ni za zamani lakini wangekuwa wanajifunza kitu basi mabadiliko na utendaji ungekuwa tofautina ulivyo.
   
 4. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #4
  Aug 2, 2011
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Part of the Quote'''''it is prudent for the scene crime officer to involve the medic rather than risk losing evidence or creating artifacts. Where the medic cannot visit the scene, a detailed and accurate recording of the status of the scene of crime should be done, including the use of sketches, diagrams, still photographs and even video recording'''''

  TO MY SIDE I STILL SEE TANZANIA IN THE TOTAL DARKNESS!!!!!!!!!!! IT IS VERY SHAME TO SEE SUCH SITUATION PERSISTING!!!!!! AT THIS POINT OF TIME I BELIEVE IS AN ERA OF TRUTHFULNESS....SCIENCE AND TECHNOLOGY SHOULD NOT LIVE US BEHIND! HOW CAN WE PROSPER IF WE STILL LIVE LIKE IN THE ERA OF UWIMBOMBO AND ULINDI?????????? THE ERA OF STONE AGE?!

  REALY SHAME!!!!!!!!!!!!!
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Aug 2, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Ni ujinga huu-huu ndio unaofanya watu kama akina Zombe kuwa na dharau za kila kukicha na majigambo
   
 6. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #6
  Aug 2, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Je! Waandishi wa habari na watu binafsi wakipiga picha iwe za kawaida ama video wanaweza kumpa nani kama ushahidi wa mazingira ya tukio ili uwezekutolewa mahakamani na kumtia hatiani muuaji au kumwokoa anayesingiziwa?
   
 7. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #7
  Aug 2, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  HUO NI UJINGA-MBAYA ZAID HATA MAHAKAMA ZINASHINDWA KUHOJI VITU KAMA HIVYO-CHA MAANA WANCHOFANYA NI KUHAMIA KWEYE ENEO LA TUKIO NA KUENDESHEA KESI HAPO -WAKATI WANATUMIA SHERIA ZILE ZILE ZA ENZI ZA MABABU-MWISHO WA SIKU HAKUNA LA MAANA LINALOFANYIKA-NI JAMBO LA AJABU MTU AULIWE eg MWEZI WA 2,THEN MAHAKAMA IENDE LEO KUENDESHA KESI ENEO LA TUKIO ETI ILI KUPATA UKWELI WA MAMBO
   
 8. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #8
  Aug 2, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  <br />
  <br />
  Duh!!
  Nafikiri Kamanda Kova au Mwema wangekuwa mbele yako lingetoka *¿&*¤¿* kubwa. Taratibu, naelewa vinauzi sana, kwasababu tunapata both direct and indirect effects.
   
 9. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #9
  Aug 2, 2011
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Tusisahau kuwa sisi ni watanzania, ambapo kila kitu kinawezekana na kila kitu hakiwezekani. Ni Tanzania ambapo mgonjwa wa miguu alipasuliwa kichwa na mgonjwa wa kichwa alipasuliwa mguu.

  Ni nchi ambayo magari ya zimamoto yanapeleka maofisa wa zimamoto kuangalia jinsi moto unavyoteketeza nyumba, au wanakwenda kwenye ajali ya moto, na kubaini kuwa gari haina maji wala dawa ya kuzimia moto.

  Nchi ambayo wananchi wakipewa pilau na kanga wanapiga kura kumchangua mbunge ambaye haonekani hadi siku itakayofuata kupiga kura

  Nchi ambayo wezi na mafisadi wanasifiwa na kupongezwa, wadokozi na vibaka wanauawa.

  Ambayo, watu wanakaa bila umeme siku tatu halafu wanacheka tu, na wanaendelea kudanywa na wanajua kuwa wanadanganywa na wanakubali........

  kuna mengi tu.


  Jaribu usome ripoti za utafiti kuhusu utendaji wa Polisi, au nenda kwenye ofisi yeyote ya polisi uone jinsi ofisi vilivyokuwa equipped na jinsi polisi wanavyofanya kazi. Unazungumzia kamera, angalia sare zao, viatu vyao, chakula wanachokula, unweza kuona kuwa kamera ni very secondary si ya "lazima". No doubt ni kitu muhimu sana, lakini polisi wanatesa watu, wanaua watu nani atabeba? Unaweza kuwapa taarifa ukashangaa hata kuipokea wanasita.

  Kuna sababu nyingi sana zinazotufanya tusiwe kama nchi zenye polisi wanaotumia kamera.
   
 10. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #10
  Aug 2, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Bongolander, umenena sawa lakini kuna jambo moja tulitafakari.
  Je! Polisi wanakosa vitu vya msingi ikiwa pamoja na vitendea kazi kwasababu hawaombi kwa kutokuweka ktk bajeti zao au ni kwasababu wamenyimwa?
   
 11. NGUVUMOJA

  NGUVUMOJA JF-Expert Member

  #11
  Aug 7, 2011
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,353
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Tambua kuwa tupo Dunia ya 3. Third World.
   
 12. Mlango wa gunia

  Mlango wa gunia Senior Member

  #12
  Aug 8, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 123
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Criminals wengi ndio wameshika nafasi mbalimbali za uongozi,tegemea watadhoofisha investigations in every means kadri wawezavyo,kuboresha investigation ni kujimulika na kurunzi wao wenyewe.
   
 13. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #13
  Aug 8, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Bunduki ndio kwao muimu,yaan ushawai sikia wenyewe wakilaum kuwa hawana kamera???wao wanataka gari au binduki,ffu kamera ya nini???ndo maana wizara inapuuzia kununu
   
Loading...