Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,777
Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango, leo Agosti 11 atafungua mkutano mkuu wa mwaka wa maofisa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi katika Shule ya Polisi Tanzania – Moshi.
Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime, amesema kuwa mkutano huo utafunguliwa Agosti 11 na utafanyika hadi Agosti 15, 2025 na kwamba lengo la mkutano huo ni kufanya tathmini ya utekelezaji wa majukumu ya Jeshi la Polisi, kuweka mikakati ya kuendelea kuimarisha na kudumisha usalama nchini, ikiwemo ya kuhakikisha Uchaguzi Mkuu wa 2025 unafanyika katika mazingira yenye amani, utulivu na usalama.